Machimbo mapya yafumuka Kahama. Polisi wapiga mkwara

Slave

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2010
Posts
5,313
Reaction score
2,657
Leo inaweza kuwa siku ya sita tangu mwanakijiji mmoja alipogundua dhahabu katika eneo la shamba lake. Dhahabu nayo haina siri muda mfupi tu baadae eneo hili la mwime ya ilindi watu wengi walifulika eneo hili. Wengi wamenufaika si wachimbaji tu hata akina mama ambao walikuwa wanauza vyakula. Hata hivyo polisi wamekataza eneo hilo kuendelea kuchimba wakidai uchimbaji huo wametakiwa wachimbaji wawe na kibali maalum. Muda huu naandika post hii polisi wapo eneo husika wakisubiri nguvu zaidi kwa ajili ya kuwatawanya wachimbaji.
 
huo ni ukuda; kwanini wasiwaache wananchi wakafaidika na mali zao!!!! Polisi inabidi wakae hapo kulinda usalama wa hao raia na si kuwazuia kuchimba kile wanachoamini kuwa ni haki yao..
 
huo ni ukuda; kwanini wasiwaache wananchi wakafaidika ni mali zao!!!! Polisi inabidi wakae hapo kulinda usalama wa hao raia na si kuwazuia kuchimba kile wanachaamini kuwa ni haki yao..

simu yangu camera mbovu,ingependeza sana kama ningeambatanisha picha.kuna mtu mmoja ameniambia kuwa eneo hilo mpaka sasa matajiri wameanza kulinyatia kwa vigezo vya kukata leseni.
 
Tangazo toka polisi wanasema ifikapo saa 3:00 wasione mtu.nanukuu tunawata akina mama mtoke mapema tubaki na hawa
 
Mkuu Slave!

Ebu funguka basi!

Maeneo gani ya kahama ilipofumuka hiyo dhahabu je ni ya vikole au kwenye mwamba?

Nataka nije na metal detector kama 100 nitengeneze 'dollar'
 
Mkuu pambaneni na hao polisi ili mpate hayo madini!
 
naogopa kitakachotokea hapo. polisi wenyewe si ndio wale wezi wa meno ya tembo wnanchi wameisha
 
Mkuu Slave!

Ebu funguka basi!

Maeneo gani ya kahama ilipofumuka hiyo dhahabu je ni ya vikole au kwenye mwamba?

Nataka nije na metal detector kama 100 nitengeneze 'dollar'

sehem hii inaitwa mwime ya ilindi kuna mama mmoja alie kuwa nae anachimba alipata dhahabu kwa msaada wa metal detector jiwe linalo zaniwa kufikia thamani tsh 50ml nimejifunza jambo hapo kuwa na hivyo ving'amuzi vya dhahabu unafanya kazi bila wasi.
 
Muda si mrefu utasikia asilimia 5 dar halafu 95 ulaya kanda ya ziwa 0.00000000000000
 
Leo inaweza kuwa siku ya sita tangu mwanakijiji mmoja alipogundua dhahabu katika eneo la shamba lake. Dhahabu nayo haina siri muda mfupi tu baadae eneo hili la mwime ya ilindi watu wengi walifulika eneo hili. Wengi wamenufaika si wachimbaji tu hata akina mama ambao walikuwa wanauza vyakula. Hata hivyo polisi wamekataza eneo hilo kuendelea kuchimba wakidai uchimbaji huo wametakiwa wachimbaji wawe na kibali maalum. Muda huu naandika post hii polisi wapo eneo husika wakisubiri nguvu zaidi kwa ajili ya kuwatawanya wachimbaji.

Mwenye eneo ndio mwenye haki hapo,apewe taratibu zote za kupata hati miliki ya ardhi yake.Kama Serikali imejifunza kutokana na makosa,sasa imlinde mwenye eneo angie kama mwekezaji wa ndani,na apewe vibali vinavyostahili,apewe misamaha na msaada utakamuwezersha kunufaika na kilichopatikana katika eneo lake.
 
Tangazo toka polisi wanasema ifikapo saa 3:00 wasione mtu.nanukuu tunawata akina mama mtoke mapema tubaki na hawa
ina maana ata na mwenye shamba hatakiwi kuwepo katika eneo hilo!!!!!,
 
nasikitika sana ninaposikia dhahabu imevumbuliwa mahala.....maana haitomnufaisha mwananchi......na huyo mwenye shamba nae mbona kiazi? Kashindwa kuchimba mwenyewe kimya kimya?
 
Hili nalo neno,ila naweza sema huyo mwenye shamba ni reflection ya watanzania wote
 
sehem hii inaitwa mwime ya ilindi kuna mama mmoja alie kuwa nae anachimba alipata dhahabu kwa msaada wa metal detector jiwe linalo zaniwa kufikia thamani tsh 50ml nimejifunza jambo hapo kuwa na hivyo ving'amuzi vya dhahabu unafanya kazi bila wasi.
Mkuu vip metol detector kwa sasa zinapatikana wapi na vipi kuhusu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom