Kiwalani finest
Senior Member
- Jul 6, 2024
- 116
- 85
Machawa Wanatuharibia Taifa kwa Kuendeleza Ufisadi na Kupewa Rushwa Kama Watoto wa Ndege
Katika hotuba yake, Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Tanzania alisema tarehe 05/10/2024, “Tusimung’unye Maneno.”
Dkt. Philip Isdor Nzabayanga Mpango, Makamu wa Rais, akimuwakilisha Rais Dkt. Samia, alifunga kongamano kuhusu Uhuru wa Kidini Barani Afrika lililofanyika Arusha, akisema, “Mimi naamini yafaa sote turudi kwenye utaratibu wetu mzuri wa kusemana na kuonyana kwa upendo au kidugu.”
Ni muhimu kusoma Katiba ya CCM ya 1977, toleo la 2022, ibara ya 15(07), pamoja na Kanuni za Utumishi za Wafanyakazi wa CCM na Jumuiya zake toleo la 2019, uk. 73. Pia, tuzingatie Mwongozo wa CCM wa mwaka 1981, uk. 46, ibara 59, na Kitabu cha Awamu ya Tatu ya Mradi wa Kukiimarisha Chama, uk. 07, kwa msisitizo. Kitabu cha Sera ya CCM ya Kujitegemea Kimapato na Kiuchumi, uk. 03, ibara 06, kinatuonyesha kuwa sisi wanasiasa tunapaswa kutenda wema, ambayo ni kufuata na kutii ilani, katiba, kanuni, miongozo, na taratibu tulizokubaliana.
Katika siasa, tunakutana na matatizo ya watu wanaoitwa "Machawa," ambao hawana imani katika maandiko ya kimfumo, bali wanaamini katika kulishwa ubwabwa na kujikomba. Wanapokutana na sisi wanaoshikilia ukweli, huwa na hofu ya kupoteza nafasi zao za kulishwa ubwabwa, na hivyo wanajikita katika kukandamiza ukweli.
Machawa hawapaswi kupewa nafasi tena; lazima tueleze ukweli. Wameikosea nchi na kupotosha ukweli kiasi kwamba wameaminisha watu kuwa siasa ni uongo, jambo ambalo si kweli. Ukweli ni kwamba Machawa ndiyo waongo wakuu, wakitafuta maslahi yao binafsi kwa tamaa za njaa zisizo na uzalendo. Wanapompinga mtu anayekumbusha umuhimu wa kufuata sheria na maandiko ya kimfumo, wanajionyesha kama wanafiki.
Wana nafasi ya kuomba radhi Mwenyezi Mungu na kutubu kwa kueneza ujinga katika jamii, na kuifanya jamii idharau ilani, viapo, katiba, kanuni, miongozo, na taratibu, kiasi cha kuaminisha watu kuwa mambo haya ya kisheria ni kwa ajili ya masikini na watumishi wa umma.
Hii ndiyo sababu Machawa wanaweza kutoa taarifa za uongo na bado wakapewa vyeo, wakauza ofisi za chama na kuendelea kuwa madarakani. Shekhe Hilali Shaweji Kipoozeo, akitoa mawaidha huko Oman tarehe 26/08/2017, alisema, “Tawba maana yake hasa ni mtu kujijua ana makosa; akijijua tu kuwa ana makosa, tayari kinachofuata ni tawba, na ni kitu muhimu kweli kweli.”
Ni maumbile ya mwanadamu kukosea, na hakuna mwanadamu aliyekamilika. Bwana Mtume Mohammad (SAW) alisema, “Kila mwanadamu ni mkoseaji,” lakini bora ni wale wanaobadilika na kuleta tawba.
Hebu tubadilike sasa ili tutende tawba. Mliojipatia vyeo kinyume na utaratibu, mlifanya kufuru. Tubuni kabla Mwenyezi Mungu hajawaueni. Mnaosema uongo na kueneza ujinga wa kuwa siasa ni uongo, mkaishi mkilindana kwenye kutenda maovu na kuviza haki za wanyonge, tubuni kwa kula visivyo stahili huku mkiwachukia wasema kweli, kisha kwa unafiki wenu mnajifanya kwenda nyumba za ibada ili muonekane kama waumini wapenda haki kumbe ni mafirauni wapenda batili.
Shekhe Walid Alhad Omar Kawambwa, Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam, akizungumza mbele ya jeneza la marehemu Dida kabla ya kuswaliwa, alisema tarehe 05/10/2024, “Tuambiane ukweli.” Nikiwa kimya kabisa, nikaona ukweli katika ulimwengu wa kiroho.