Machangudoa waundiwa vikundi vya ulinzi Moshi

Machangudoa waundiwa vikundi vya ulinzi Moshi

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,606
Wananchi wa Kata ya Mawenzi, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wamelazimika kuunda vikundi vya ulinzi katika mitaa yao nyakati za usiku kwa lengo la kutokomeza biashara ya uchanguduo na uhalifu uliokithiri katika kata hiyo.

Hayo yamebainishwa na wananchi hao katika mkutano uliotishwa na diwani wa kata hiyo, Hawa Mushi, kwa lengo la kujadili changamoto zinazowakabili katika maeneo yao na kutoa maazimio.

Janeth Mbwambo, mkazi wa eneo hilo, amesema tatizo la machangudoa kuzagaa katika maeneo ya kata hiyo limekuwa kero nyakati za usiku pamoja na vijana wanaofanya uhalifu pia wamesababisha watu kuwa na hofu ya usalama wao.

Mkazi wa kata hiyo, Mary William, amesema pamoja na juhudi zinazofanywa za kuimarisha ulinzi bado hali imekuwa mbaya kwa kata yao huku akidai kuwa kama hawataimarisha ulinzi wao wenyewe tatizo hilo litaendelea kuwepo.

Diwani wa kata hiyo amesema wamejitahidi kupambana na uhalifu na machangudoa lakini bado tatizo limekuwa likiendelea na kwamba wataingia katika ulinzi wenyewe ili kukomesha kabisa jambo hilo.

“Tunaingia katika mapambano wenyewe ili kuwakabili machangudoa pamoja na uhalifu unaofanywa na watu kutoka nje ya kata yetu na si wakazi wa eneo husika, hali hiyo imeichafua sana kata yetu,” amesema Diwani Mushi.
Akijibu kero za wananchi hao kuhusu kelele za mziki nyakati za usiku, Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya amesema suala hilo limeshatolewa maelekezo kwa mkurugenzi wa manispaa hiyo.

Amesema kama mtu hataweza kufuata masharti ya kupiga muziki usiku, vyombo vyake vya muziki vitachukuliwa na kupelekwa katika halmashauri hiyo na akiendelea kukaidi atafungiwa na faini yake ni kiasi cha Sh.1 Millioni.

Akizungumzia suala la wafanyabiashara maarufu kama wamachinga Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Jaffar Michael, amesema suala lao limeshapitishwa bungeni kwamba ili waweze kutambulika wanatakiwa kila mmoja ajisajili.
Amesema jambo hilo litasaidia kuepusha migongano na itawaepushia kufukuzwa na kupigwa na baadhi ya mgambo, na sheria hiyo inatakiwa ianze Julai Mosi mwaka huu kwani watakuwa wanatambulika kisheria.
 
changu.jpg

Diwani wa eneo hilo, Hawa Mushi amesema wamejitahidi kupambana na uhaligia katika ulinzi wenyewe ili kukomesha tatizo hilo.

FRIDAY, JULY 14, 2017

Moshi. Wananchi wa Kata ya Mawenzi,
Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wamelazimika kuunda vikundi vya ulinzi katika mitaa yao nyakati za usiku kwa lengo la kutokomeza biashara ya uchanguduo na uhalifu uliokithiri katika kata hiyo.

Hayo yamebainishwa na wananchi hao
katika mkutano uliotishwa na diwani wa kata hiyo, Hawa Mushi, kwa lengo la kujadili changamoto zinazowakabili katika maeneo yao na kutoa maazimio.

Janeth Mbwambo, mkazi wa eneo hilo,
amesema tatizo la machangudoa
kuzagaa katika maeneo ya kata hiyo
limekuwa kero nyakati za usiku pamoja
na vijana wanaofanya uhalifu pia
wamesababisha watu kuwa na hofu ya
usalama wao.

fu na machangudoa lakini bado tatizo limekuwa likiendelea na
sasa watain

Mkazi wa kata hiyo, Mary William,
amesema pamoja na juhudi zinazofanywa za kuimarisha ulinzi bado hali imekuwa mbaya kwa kata yao huku akidai kuwa kama hawataimarisha ulinzi wao wenyewe tatizo hilo litaendelea kuwepo.

Diwani wa kata hiyo amesema wamejitahidi kupambana na uhalifu na
machangudoa lakini bado tatizo limekuwa likiendelea na kwamba wataingia katika ulinzi wenyewe ili kukomesha kabisa
jambo hilo.

“Tunaingia katika mapambano wenyewe ili kuwakabili machangudoa pamoja na uhalifu unaofanywa na watu kutoka nje ya kata yetu na si wakazi wa eneo husika, hali hiyo imeichafua sana kata yetu,” amesema Diwani Mushi.

Akijibu kero za wananchi hao kuhusu
kelele za mziki nyakati za usiku, Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya amesema suala hilo limeshatolewa maelekezo kwa mkurugenzi wa manispaa hiyo.

Amesema kama mtu hataweza kufuata masharti ya kupiga muziki usiku, vyombo vyake vya muziki vitachukuliwa na kupelekwa katika halmashauri hiyo na akiendelea kukaidi atafungiwa na faini yake ni kiasi cha Sh.1 Millioni.

Akizungumzia suala la wafanyabiashara maarufu kama wamachinga Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Jaffar Michael,
amesema suala lao limeshapitishwa
bungeni kwamba ili waweze kutambulika wanatakiwa kila mmoja ajisajili.

Amesema jambo hilo litasaidia kuepusha migongano na itawaepushia kufukuzwa na kupigwa na baadhi ya mgambo, na sheria hiyo inatakiwa ianze Julai Mosi mwaka huu kwani watakuwa wanatambulika kisheria.

My Take najua Wachaga Mnapenda Pesa Ila tafuteni kihalali.

Credits: Mwananchi
.
 
Huko moshi kuna nini lakini??
Mara kuharibu mashamba ya watu
Mara kununua madiwani
Yan tabu tupu

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Kama hapo malindi club wamejaa tele hawa machangudoa

Sent from my LG-H340n using JamiiForums mobile app
 
Sio ishu bhna. Sisi wengine tunatumia huduma zao. Apa mtasababisha tupandishiwe bei tu

Sent from my SM-G950F using JamiiForums mobile app
 
Mungu
Onesha
Shilingi
Ilipo pambana Na Bali yako

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 
Ni ujinga kupambana na mambo ambayo huwezi kuyaondoa kirahisi!

Biashara ya Ukahaba na Utumwa ndio biashara kongwe duniani.

Wafanye shughuli zingine za kuwaletea wananchi wao maendeleo
 
Machanguo wengi siku hizi wamehamia mitandaoni kama Hitwe, WhatsApp, Badoo, Fbook n.k, hivyo machangudoa nao wanaenda na muda
 
Hawa wametumwa, ngoja tuhamie kwa wake zao na mabinti zao wakati wakiwa kwenye ulinzi
 
Huko moshi kuna nini lakini??
Mara kuharibu mashamba ya watu
Mara kununua madiwani
Yan tabu tupu

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
Wizi
Bangi
Mirungi

Ushirikina

Ndio maana watu wakiondoka hawataki kuoa Moshi wanaogopa kufa mapema
 
Kwani uchangudoa ni kosa kisheria? sio kwamba naunga mkono uchangudoa, ila wao kama viongozi wanapaswa kufuata sheria na katiba ya nchi. Pia wakumbuke hawana mamlaka ya kumhukumu mtu zaidi ya mahakama.
 
Ni ujinga kupambana na mambo ambayo huwezi kuyaondoa kirahisi!

Biashara ya Ukahaba na Utumwa ndio biashara kongwe duniani.

Wafanye shughuli zingine za kuwaletea wananchi wao maendeleo
Huku mtaani kwetu walikuwepo lakini saizi hakuna ujinga huo

Only failures wanasema haiwezekani

Saizi usiku huku kitaa hakuna cha kahaba wala changuduo kwakuwa hao wakazi wameamua basi watatokomeza
 
Kwani uchangudoa ni kosa kisheria? sio kwamba naunga mkono uchangudoa, ila wao kama viongozi wanapaswa kufuata sheria na katiba ya nchi. Pia wakumbuke hawana mamlaka ya kumhukumu mtu zaidi ya mahakama.
Chukulia mfano mtaani kwenu ikifika usiku wajipange ,huoni madhara kwa jamii inayowazunguka haswa vijana wadogo ?

Hao wakazi wapo sahihi na pili ni kosa kisheria ndio maana wakikamatwa huwa wanapandishwa mahakamani
 
Back
Top Bottom