Mabweni UDSM yalanguliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabweni UDSM yalanguliwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Oct 11, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,534
  Likes Received: 81,951
  Trophy Points: 280
  Mabweni UDSM yalanguliwa

  na Mobini Sarya
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu

  WIMBI la kuuza vyumba vya kulala wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) sehemu ya Mlimani, limeshika kasi hivyo kuwafanya wanafunzi wengi wanaotokea familia maskini kushindwa kumudu gharama ya kupanga.

  Inadaiwa vyumba vilianza kuuzwa sh 100,000. Hivi sasa chumba kimoja kinauzwa hadi sh 300,000 kupitia kwa mawakala ambao ni wanafunzi wanaokula na wahusika.

  Taarifa hizo zinadai biashara hiyo inayowahusisha wasimamizi wa vyumba na madalali, imeanza siku chache baada ya chuo hicho kufunguliwa Septemba 29, mwaka huu, hivyo kuwalazimu watoto wa maskini wanaoshindwa bei hiyo kuamua kupanga mitaani.

  Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu, mmoja wa wabunge katika serikali ya wanafunzi (Daruso), alisema hivi sasa biashara hiyo inafanyika bila kificho.

  “Unakuta tangazo kwenye ubao wa matangazo kwamba chumba kinauzwa shilingi kadhaa kwenye jengo fulani na ghorofa namba fulani, lakini mtu huyo hakamatwi,” alisema mbunge huyo ambaye jina lake limehifadhiwa.

  Inaelezwa kwa kawaida mwanafunzi anatakiwa kuomba chumba kupitia mtandao wa chuo na kupewa na kisha kulipia sh 50,000 kwa muhula mmoja na iwapo atashindwa chumba hurudishwa kwa kitengo kinachohusika ili apewe mtu mwingine.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,534
  Likes Received: 81,951
  Trophy Points: 280
  Waungwana,

  Lazima kupambana na hawa mafisadi. Wapigwe picha wakichukua rushwa za kutoa vyumba vya UDSM na ziwekwe hapa JF na kupelekwa polisi ili kuwakomesha mafisadi hawa ambao wanataka kutumia nafasi zao kujitajirisha. Hawa wanaokula na wakubwa wakibanwa ni lazima watawataja wanaokula nao pale UDSM na hivyo kuwachukulia hatua zinazostahili ikiwa ni pamija na kuwafukuza kazi na kuwafungulia mashtaka.
   
 3. PgSoft2008

  PgSoft2008 JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2008
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ni wazo zuri sana lakini kutokana na nature ya business yenyewe sidhani kama waweza kuwapiga picha kirahisi,

  They do no have offices (hao madalali).
  hakuna follow-up ya mgawanyo wa hivyo vyumba (rooms allocations)
  Ukienda kwa taratibu husika unakuta vyumba vimejaa (yaani tayari allocated) Infact unanunua chumba kwa mwanafunzi mwenzio na sio ofisi husika.

   
 4. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2008
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,788
  Likes Received: 6,296
  Trophy Points: 280
  Mkuu BAK, vyumba pale mlimani havijaanza kuuzwa leo. Mimi niliuziwa chumba na aliyekuwa vice president wa DARUSO (Ephraim Mafuru, sasa ni kibosile flani ndani ya VodaCom) mwaka 1997.

  So, biashara hii viongozo wa DARUSO ndo vinara wenyewe na wala haitaisha kesho.

  Pia wanaouza vyumba huwa ni wamiliki 'halali' ambao wamepata vyumba kwa utaratibu uliopangwa lakini kwa kuwa hawataki kukaa chuo, wanaamua kuuza.
   
 5. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kutokana na mimi ninavyofahamu ni kwamba wanafunzi wenyewe ambao wanashida ya fedha wengi wao ndio wauzaji wakubwa wa rooms.
  Vilevile wardens wa halls ni wala rushwa wakubwa mabao wanahongwa na wanafunzi hadi laki tano ili tuu apate room katika baadhi ya halls of residence kwenye hiko chuo na wengine hata kuwa na vyumba hadi vitano then wanaviuza.
  Its a profitable business hapo chuoni na ambao hawana fedha ndio wanaishia kuumia!
  DARUSO wenyewe ni mafisadi wakubwa coz wanapatana na baadhi ya wardens na kuuza rooms maana wengi wao DARUSO wana occupy rooms kwenye hall linaloitwa Extension!
   
 6. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kutokana na mimi ninavyofahamu ni kwamba wanafunzi wenyewe ambao wanashida ya fedha wengi wao ndio wauzaji wakubwa wa rooms.
  Vilevile wardens wa halls ni wala rushwa wakubwa mabao wanahongwa na wanafunzi hadi laki tano ili tuu apate room katika baadhi ya halls of residence kwenye hiko chuo na wengine hata kuwa na vyumba hadi vitano then wanaviuza.
  Its a profitable business hapo chuoni na ambao hawana fedha ndio wanaishia kuumia!
  DARUSO wenyewe ni mafisadi wakubwa coz wanapatana na baadhi ya wardens na kuuza rooms maana wengi wao DARUSO wana occupy rooms kwenye hall linaloitwa Extension!
   
 7. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2008
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,498
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Sinyolita,
  Mimi nakumbuka nimemaliza shule UDSM mwaka 1999, Mafuru nadhani alikuwa hata hajaanza shule, au alikuwa first year! Hiyo mwaka 1997 hata Kitila Mkumbo alikuwa bado hajashika uongozi. Huyo Mafuru mimi namfahamu na tumesoma wote pale shuleni kwa mwalimu nyerere, Pugu high school. Jamani naomba tuache siasa za kuchafuliana majina, simply mwenzako ameweza kuwa kibosile fulani kwenye system. Kwa ulivyowakilisha ujumbe wako, ni wazi kuwa mafuru hakuwahi kukufanyia kitu cha namna hiyo, ila pengine tu humpendi kwa sababu zako unazozijua!
   
 8. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  As long as there's a demand there'll always be a supply. That's enterpreneurship if you ask me. The problem that needs to be addressed is shortage of accomodation. These students sublet the rooms on their own free will au?
   
Loading...