Mabwege uishi miaka mingi 1 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabwege uishi miaka mingi 1

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jacaranda, Mar 6, 2012.

 1. J

  Jacaranda Member

  #1
  Mar 6, 2012
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jua lililokuwa limetawala lilimezwa ghafla na mawingu yaliyokuwa yametanda.kiupepo kilianza kuvuma na kubeba takataka nyepesi na kuzirusha juu na kulifanya angaa litawaliwe na rangi nyeusi ya mifuko ya plastiki.Viatu vyangu nilivyo vaa vilipigwa na vumbi na kuvifanya vionekane kama vimeopolewa toka kwenye kifusi cha udongo wa mererani.Ghafla manyunyu yakaanza kudondoka,nikaongeza mwendo huku nikiwa nimeificha bahasha ya kaki iliyokuwa na vyeti vyangu kwapani,taratibu kimvua kikazidi na hivyo kunifanya nianze kukimbia huku mkono wangu wa kulia nikiwa nimeuweka kwenye mfuko wangu wa suruali kuzuia shilingi mia tatu niliyobakiza isidondoke.

  Nilipofika kituo cha mwenge nilikua nimebakiza shilingi mia tatu kwa hiyo nikakata shauri ya kutembea kwa mguu mpaka ubungo kisha nipande daladala kumalizia safari yangu mpaka mbezi kibanda cha mkaa.Nilipofika maeneo ya Mlimani city Mvua ikazidi kuongezeka kiasi cha kunifanya nisiweze kuona mbele vizuri.Nilipoangalia kushoto nikaona watu wengi wakikimbilia ndani ya maduka ya mlimani city nikajiunga nao.Nilipofika ndani ya jengo la mlimani city nikaifungua bahasha yangu na kuvitazama vyeti vyangu baada ya kuridhika kuwa havijaloana nikatabasamu huku nikijifuta uso wangu kwa handkcheif ambayo ilikuwa ikitoa harufu ya jasho,niilipomaliza nikaikunja nakuiweka kwenye mfuko wa shati nililokuwa nimelivaa,Ambalo kwa sasa lilikuwa limeloana na hivyo kuufanya uchafu uliokuwa umejificha kuonekana vizuri zaidi.Niliponyanyua macho yangu nikagonganisha macho yangu na kikundi cha watu waliokuwa wakinitazama utafikiri nzi aliyedondokea kwenye chakula chao cha gharama.Nikajitazama aikunichukua muda kujua kwa nini walikuwa wakinishangaa.Kwa jinsi nilivyokuwa mchafu sikuwa na tofauti na mchimbaji wa tanzanite aliyeshinda handakini kwa wiki nzima bila kubadirisha nguo,ghafla nikajihisi kama mkimbizi ndani ya nchi nisiyotakiwa."Go to hell" nikasonya kwa sauti ya chini huku nikingia kwenye duka la vitabu liitwalo scholastica

  Nikaelekea moja kwa moja kwenye shelfu lenye novel,nikachomoa kitabu kimoja nikageuza nyuma,nikaanza kusoma muhtasari wake taratibu.wakati nikiendelea kusoma nikasikia sauti nyororo ya msichana ikiimba kwa sauti ya chini nikageuka kumtazama.Nilipigwa na butwaa,nikajihisi kama mtu aliyepigwa na radi,midomo yangu ikabaki wazi,kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nikajiona nimekuwa zuzu.Macho yangu hayakuamini nilichokiona nikayaficha kisha nikakodoa zaidi na kugundua kuwa siko ndotoni.Msichana aliyekuwa amesimama mbele yangu alikuwa ni mzuri sijapata kuona.Alikuwa na uso mzuri uliopambwa na macho yaliyomfanya haonekane kama amelemewa na usingizi,midomo yake ilikuwa imekaa vyema kama ungeilinganisha na ya Angelina Jolly ni wazi Angelina angeonekana kikaragosi.Alikuwa na nywele nyingi zilizoanguka mabegani na baadhi alikuwa amezirushia usoni na hivyo kumfanya aonekane mzuri zaidi.Alikuwa amevalia kitop cha rangi ya pinki kilichoyafanya maziwa yake yaliojazia vyema yajitokeze vizuri na kuonekana kama vichuguu viwili vilivyotenganishwa na kinjia chembamba,nikayatuliza macho yangu kwenye kifua chake huku nikihisi kama nitayaondoa macho yangu wenda pumzi yangu itakata,nikajikuta nikiwaza kama mimi ningekuwa msichana na ninakifua kama hicho basi tayari ningekuwa nishakua milionea,kitopu chake kilikomea juu ya kitovu na hivyo kulifanya tumbo lake lisilo na kitambi kuonekana.Chini alikuwa amevalia kaptura ya rangi nyeusi ambayo ilikuwa imefikaa mpaka magotini na hivyo kuzisitiri hips zake ambazo kwa ukubwa zilizokuwa nao zilikuwa zikipigana na nyuzi za kaptura hiyo kutakaa kuzitatua.Alikuwa ni mrefu wa wastani huku kiuno chake cha nyingu kikimfanya hazidi kuonekana kama malaika aliyedondoka kwa bahati mbaya toka mbiguni.Nilipogonganisha macho yangu na yake, nikaugeza uso wangu kwa aibu utafikiri mtu aliyekamatwa akipiga chabo.Nikayarudisha macho yangu kwenye novel iliyokuwa mkononi mwangu.

  Mawazo yangu hayakuwa tena kwenye kitabu,moyo wangu ulijihisi kumpenda ghafla huyo msichana,lakini nilijua kamwe siwezi kumpata na jambo jingine lilikuwa wazi baada ya kumuona huyo msichana sitaweza tena kumpenda msichana mwingine mpaka siku sura yake itakapotoweka katika fikra zangu.Ufunuo huu ulinifanya niwe mnyonge moyoni mwangu huku sehem nyingine ya moyo wangu ikihisi furaha fulani ya ajabu ya japo kumuona,"Hicho ni kitabu cha Mario Puzo Godfather?" sikutegemea kuongeleshwa na yule msichana,nikajikuta nimenyanyua uso na kumkodolea macho kisha nikakigeuza kitabu nilichokuwa nimekishika na kukiangalia nikakutana na maandishi makubwa yalioandikwa Godfather Mario Puzo.Ghafla tumbo langu likatoa miungurumo ambayo ilisikika na kunifanya nione aibu nikakumbuka kuwa mchana wa siku hiyo nilikuwa sijala kisa kutokuwa na hela."Ndi ndi............" nikajikuta nimekabwa na kigugumizi akanikatisha na kuniambia "you should buy it.it is a very nice novel" sauti yake nyororo ikaamusha hisia fulani akilini na mwilini mwangu,nikahisi kama viungo vyangu vya kiume vinasimama taratibu.nikakishusha kitabu mpaka katikati ya mapaja yangu ili kujisitiri.nilipomuangalia nikamuone bado anakiangalia kitabu ambacho kwa sasa kilikuwa kimeshafika mapajani mwangu.
  AISEEE NIMECHOKA TUTAENDELEA
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Mar 6, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 68,260
  Likes Received: 22,915
  Trophy Points: 280
  Paragraphs, please.
   
 3. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 26,365
  Likes Received: 4,799
  Trophy Points: 280
  lol hebu endelea mkuu..
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,138
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  duh. . . .
   
 5. Wonder Woman

  Wonder Woman Senior Member

  #5
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeipenda story yako. Nzuri sana.

  Si kwa ubaya ..
  Ila umetumia neno "NIKA"karibu kila sentence na sehemu nyingine umetumia neno hiilo zaidi ya mara tatu kwenye sentence moja. Kama una plan kuwa muandishi WA vitabu just be careful with that word . Otherwise great job.
   
 6. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 24,925
  Likes Received: 1,982
  Trophy Points: 280
  Mtafute Shigongo kipaji unacho cha utunzi wa story.
   
 7. Ec mwakisopile

  Ec mwakisopile Member

  #7
  Mar 6, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  nice story
   
 8. Crucial Man

  Crucial Man JF-Expert Member

  #8
  Mar 6, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 3,097
  Likes Received: 248
  Trophy Points: 160
  ulipo taja the god father,mh umenikumbusha,the last don na the ometra.hivi vitabu vya mario puzo navipenda sana.
   
 9. J

  Jacaranda Member

  #9
  Mar 6, 2012
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekusoma
   
 10. J

  Jacaranda Member

  #10
  Mar 6, 2012
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umemkumbuka Don Dominiko na Don Vittorio
   
 11. data

  data JF-Expert Member

  #11
  Mar 6, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 13,122
  Likes Received: 2,939
  Trophy Points: 280
  Shigongo iz in da haasss...
   
 12. mtzedi

  mtzedi JF-Expert Member

  #12
  Mar 6, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 978
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  ww ni nomaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 13. Fabolous

  Fabolous JF-Expert Member

  #13
  Mar 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 1,246
  Likes Received: 324
  Trophy Points: 180
  Mkuu stori nzuri sana. Usisahau kutuletea tena inapoendelea.
   
 14. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #14
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu, utaendelea saa ngapi??! Hebu taja muda tujue kabisa...lol
  Ila huyo msichana wako siku akivaa suruali nitakuwa simpendi tena! Jitahidi next time avae gauni au skirt atakuwa mzuri zaidi...Haahaaahaaaa!!
   
 15. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #15
  Mar 7, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  editor wake si wewe?
   
 16. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nice story
   
 17. Wonder Woman

  Wonder Woman Senior Member

  #17
  Mar 7, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani lazima niwe editor wake ku suggest kitu? .
   
Loading...