johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 84,004
- 142,029
Hahahaa..... Umeshapanic bwashee!Umetumwa na Mabeberu, huu uharo sio type yako
Kwanini mkuu?!
Hamna kitu kinauma kama Kumuona David Molinga anacheza Yanga wakati hata kupiga dana dana hawezi
Bunge la sasa unalisikilizia wapi mkuuHayo mabunge yailkua hot sana... Uchoki kuyasikilza wala kuyaangali...
Wabunge kinga zao zilikua zinaheshimika wanajadili mambo kwa uwazi bila vitisho... Mawaziri tumbo joto...
Cc: mahondaw
Mkuu Yohana Mbatizaji, John the Baptist, kwanza naunga mkono hoja, haya ni maendeleo makubwa.Haya ni maendeleo makubwa kwa bunge kama taasisi.
Maendeleo hayana vyama!
Serikali inayojitambua haiwezi kusubiri kuwajibishwa na bunge!Na hilo halishangazi kwa sababu, mabunge yaliyopita, hususani Bunge la Awamu ya 4 ililiachwa litekeleze wajibu wake!!
Kila ilipokuwa inaletwa Ripoti ya CAG, wabunge walikuwa wanaichambua kwa uhuru mkubwa, na pale penye matatizo, wabunge walikuwa wanaiwajibisha serikali!!
Kinyume chake, hivi sasa hata kuandaa Ripoti ya CAG kwenyewe ni kupoteza pesa tu!!! Ripoti serious kama ya CAG imebaki kufanyiwa mzaha tu huko bungeni!!
Sio kusubiri iwajibishwe na bunge bali bunge kutekeleza wajibu wake!!! Hapo kabla Bunge lilikuwa linachambua ripoti mbalimbali kwa mapana na marefu na hivyo kuna madhaifu ya kutisha!Serikali inayojitambua haiwezi kusubiri kuwajibishwa na bunge!
Hii ni topic pana sana. Ni topic ukiiandikia thesis inaweza kukupatia PhD. Ila inahitaji utafiti mpana sana katika swala la "legislature and legislative processes" watu wa political science wanajua.Tulishuhudia katika bunge lililoongozwa na mh Msekwa mawaziri Prof Mbilinyi Dr Ngasongwa na Dr Kitine wakijiuzulu kwa shinikizo la bunge.
Tukawashuhudia tena akina Karamagi, Dr Msabaha nk wakijiuzulu kwa shinikizo la bunge awamu ya mzee Sitta.
Kadhalika alipoingia mama Makinda kitini pa Spika ndio tulishuhudia bunge likishinikiza kutumbuliwa kwa rundo la mawaziri kwa mpigo kwenye kamati ya operesheni tokomeza wakiwemo Dr Nchimbi, Dr Mathayo na wengine waliofikia watano au sita.
Katika awamu ya sasa ya Spika Ndugai hakuna waziri amewahi kuguswa utumbuaji unafanyika serikalini direct bila kusubiri shinikizo la taasisi yoyote.
Ila jambo jema ni kuwa sasa wabunge wanashughulikiana wenyewe ili kuimarisha taasisi yao. Tumeyaona ya Nassari, Tundu Lisu na hata yule Rais wa bunge la Afrika mh Masele
Haya ni maendeleo makubwa kwa bunge kama taasisi.
Niishie hapo
Maendeleo hayana vyama!
Ahsante mkuu!Hii ni topic pana sana. Ni topic ukiiandikia thesis inaweza kukupatia PhD. Ila inahitaji utafiti mpana sana katika swala la "legistlature and legislation processes" watu wa political science wanajua.
Inabidi vilevile kutafiti utendaji wa serikali hizo pindi mawazili hao wakiwajibishwa na bunge, pia mienendo ya wabunge wa mabunge yale pindi mabunge yale yakiwajibisha mawazili.
Nadhani walioshule, hii wakiitengeneza vizuri inaweza kuwasaidia kutafiti na kuandika thesis zao.