Mabunge ya Msekwa, Sitta na Makinda yaliwawajibisha mawaziri Bunge la Ndugai linawajibisha wabunge haya ni maendeleo makubwa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,750
139,541
Tulishuhudia katika bunge lililoongozwa na mh Msekwa mawaziri Prof Mbilinyi Dr Ngasongwa na Dr Kitine wakijiuzulu kwa shinikizo la bunge.

Tukawashuhudia tena akina Karamagi, Dr Msabaha nk wakijiuzulu kwa shinikizo la bunge awamu ya mzee Sitta.

Kadhalika alipoingia mama Makinda kitini pa Spika ndio tulishuhudia bunge likishinikiza kutumbuliwa kwa rundo la mawaziri kwa mpigo kwenye kamati ya operesheni tokomeza wakiwemo Dr Nchimbi, Dr Mathayo na wengine waliofikia watano au sita.

Katika awamu ya sasa ya Spika Ndugai hakuna waziri amewahi kuguswa utumbuaji unafanyika serikalini direct bila kusubiri shinikizo la taasisi yoyote.
Ila jambo jema ni kuwa sasa wabunge wanashughulikiana wenyewe ili kuimarisha taasisi yao. Tumeyaona ya Nassari, Tundu Lisu na hata yule Rais wa bunge la Afrika mh Masele

Haya ni maendeleo makubwa kwa bunge kama taasisi.

Niishie hapo
Maendeleo hayana vyama!
 
Mbona tulishaambiwa kitambo! Katika awamu hii, Mhimili mmoja umejichimbia chini zaidi kuliko ile mingine miwili iliyobakia! Kwa sasa ni mwendo tu wa kupigwa nje na ndani.
 
Sio wabunge tuu, Bali hili bunge la Ndugai limeshughulikia mpaka walio nje ya Bunge wameipata.
CAG ameitwa kwa mwendo wa fanfan bungeni na kidogo angechelewa angechotwa kwa pingu na suruali kupigwa Tanganyika jeki.
Wengine wa nje ya bunge ni ndugu yangu Pascal Mayalla ambaye aliwekwa kati sio mchezo. Habari chini ya kapeti ni kuwa "kaka" Wakudadavuwa alitupia maneno ya faraja kumpunguzia machungu alipotoka msambweni.
Tunamshukuru "kaka" Wakudada kwa huduma hiyo kwa msukuma wetu JF
 
Na hilo halishangazi kwa sababu, mabunge yaliyopita, hususani Bunge la Awamu ya 4 ililiachwa litekeleze wajibu wake!!

Kila ilipokuwa inaletwa Ripoti ya CAG, wabunge walikuwa wanaichambua kwa uhuru mkubwa, na pale penye matatizo, wabunge walikuwa wanaiwajibisha serikali!!

Kinyume chake, hivi sasa hata kuandaa Ripoti ya CAG kwenyewe ni kupoteza pesa tu!!! Ripoti serious kama ya CAG imebaki kufanyiwa mzaha tu huko bungeni!!
 
Serikali inayojitambua haiwezi kusubiri kuwajibishwa na bunge!
 
Serikali inayojitambua haiwezi kusubiri kuwajibishwa na bunge!
Sio kusubiri iwajibishwe na bunge bali bunge kutekeleza wajibu wake!!! Hapo kabla Bunge lilikuwa linachambua ripoti mbalimbali kwa mapana na marefu na hivyo kuna madhaifu ya kutisha!

Kinyume chake, hivi sasa hicho kitu hakipo! Kwa maana nyingine, Bunge linashindwa kutekeleza wajibu wake na wala sio kwamba Ripoti za CAG hazioneshi uozo sehemu mbalimbali!

Na ni kutokana na ukweli huo ndio maana sio tu kupitia Bunge bali hata kupitia Magu mwenyewe, hakuna mmoja wao aliyewahi kumwajibisha waziri yeyote kwa mambo yanayoashiria ufisadi ama ubadhirifu unaotajwa na CAG! Kama yupo nikumbushe!
 
Naunga mkono hoja. Bunge hili ni awamu ya mgogo hasira ni kwa wabunge wa upinzani. Ugomvi ni ndani kwa ndani ya nje hayawahusu
 
Tulishuhudia katika bunge lililoongozwa na mh Msekwa mawaziri Prof Mbilinyi Dr Ngasongwa na Dr Kitine wakijiuzulu kwa shinikizo la bunge.

Tukawashuhudia tena akina Karamagi, Dr Msabaha nk wakijiuzulu kwa shinikizo la bunge awamu ya mzee Sitta.

Kadhalika alipoingia mama Makinda kitini pa Spika ndio tulishuhudia bunge likishinikiza kutumbuliwa kwa rundo la mawaziri kwa mpigo kwenye kamati ya operesheni tokomeza wakiwemo Dr Nchimbi, Dr Mathayo na wengine waliofikia watano au sita.

Katika awamu ya sasa ya Spika Ndugai hakuna waziri amewahi kuguswa utumbuaji unafanyika serikalini direct bila kusubiri shinikizo la taasisi yoyote.
Ila jambo jema ni kuwa sasa wabunge wanashughulikiana wenyewe ili kuimarisha taasisi yao. Tumeyaona ya Nassari, Tundu Lisu na hata yule Rais wa bunge la Afrika mh Masele

Haya ni maendeleo makubwa kwa bunge kama taasisi.

Niishie hapo
Maendeleo hayana vyama!
Hii ni topic pana sana. Ni topic ukiiandikia thesis inaweza kukupatia PhD. Ila inahitaji utafiti mpana sana katika swala la "legislature and legislative processes" watu wa political science wanajua.

Inabidi vilevile kutafiti utendaji wa serikali hizo pindi mawazili hao wakiwajibishwa na bunge, pia mienendo ya wabunge wa mabunge yale pindi mabunge yale yakiwajibisha mawazili.

Nadhani walioshule, hii wakiitengeneza vizuri inaweza kuwasaidia kutafiti na kuandika thesis zao.
 
Hii ni topic pana sana. Ni topic ukiiandikia thesis inaweza kukupatia PhD. Ila inahitaji utafiti mpana sana katika swala la "legistlature and legislation processes" watu wa political science wanajua.

Inabidi vilevile kutafiti utendaji wa serikali hizo pindi mawazili hao wakiwajibishwa na bunge, pia mienendo ya wabunge wa mabunge yale pindi mabunge yale yakiwajibisha mawazili.

Nadhani walioshule, hii wakiitengeneza vizuri inaweza kuwasaidia kutafiti na kuandika thesis zao.
Ahsante mkuu!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom