johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,607
- 141,431
Tulishuhudia katika bunge lililoongozwa na mh Msekwa mawaziri Prof Mbilinyi Dr Ngasongwa na Dr Kitine wakijiuzulu kwa shinikizo la bunge.
Tukawashuhudia tena akina Karamagi, Dr Msabaha nk wakijiuzulu kwa shinikizo la bunge awamu ya mzee Sitta.
Kadhalika alipoingia mama Makinda kitini pa Spika ndio tulishuhudia bunge likishinikiza kutumbuliwa kwa rundo la mawaziri kwa mpigo kwenye kamati ya operesheni tokomeza wakiwemo Dr Nchimbi, Dr Mathayo na wengine waliofikia watano au sita.
Katika awamu ya sasa ya Spika Ndugai hakuna waziri amewahi kuguswa utumbuaji unafanyika serikalini direct bila kusubiri shinikizo la taasisi yoyote.
Ila jambo jema ni kuwa sasa wabunge wanashughulikiana wenyewe ili kuimarisha taasisi yao. Tumeyaona ya Nassari, Tundu Lisu na hata yule Rais wa bunge la Afrika mh Masele
Haya ni maendeleo makubwa kwa bunge kama taasisi.
Niishie hapo
Maendeleo hayana vyama!