Umesema amesota saaana, kwa hiyo ameamua kujishikiza kwa muda tu. Siku akipata kazi ya kufanya kwa saa 4 au 5 kwa siku tena kwa mshahara mnono na marupuru, maovertime kibao basi ataondoka mbio hata haina haja ya kuwaaga hao wadosi eeenh!
Pole zake. Ila wahenga wanasema '..ukiona shida zinazidi neema inakaribia..' So mwambie akaze
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Mimi niliacha kazi mwezi mmoja tu kwani manyanyaso yao sikuweza kuyabeba kabisa. Niliona afadhali nikae nyumbani kuliko hao wa..du. Ningeweza kuwazaba kibao. Na baada ya hapo nikapata kazi sehemu wao inabidi waje waombe biashara. niliapa sintokaa niwape biashara labda hiyo sehemu niwe nimeondoka. Na siku moja nikakutana na bosi akaniuliza mbona hutupi biashara, au ulikasirika sana ulivyoondoka kwetu. Mimi nikamjibu wala, ila biashara hawatopata kupitia mikono yangu.