Maboresho ya mitaala ya elimu Tanzania

mchumi boy

Member
Jun 4, 2016
70
31
Nimekuwa nikifuatilia tatizo la vijana wengi kukosa ajira serikalini na kwenye sekta binafsi hpa nchini nikaja kubaini kuwa sababu kubwa ni udhaifu wa mitaala ya kufundishia nayo ni chanzo cha tatizo kwani mitaala iloyopo inamfanya mwanafunzi afikiri kuajiriwa tu na serikali (white collar jobs)Kwani Kuna masomo yangetiliwa mkazo yangeweza kuwasaidia wanafunzi wengi kujiajiri tofauti na ilivyo sasa. napendekeza masomo yafuatayo yapewe kipaumbele sana Biashara na Ujasiriamali, kilimo na ufugaji, na ufundi kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari, hyo itasaidia kuondokana na dhana za kuajiriwa na serikali.
 
Mm dunia hii sijawahi kusikia mambo ya vijana kujiajiri, huwa nayasikia huku Africa, hata economic theories tunazosoma sijawahi kusikia kabisa watu kujiajiri ovyo ovyo, labda kama kuna mtu anadhani anajua vizuri hii theory ya kujiajir iko wapi, iliwahi kuandikwa na nani. Nachojua kuna entrepreneurship knowledge inatolewa lakin haijawalenga vijana wanaomaliza shule, ambao hawana ujuzi zaidi ya theory, zaid hawana mitaji. Kama kuna mtu anajua kuhusu hii dhana kwa mataifa machanga kama kwetu anisaidie.
 
shule zote za ufundi hali mbaya, yamebakia majina tu na kilichobaki ni veta kwa level ya chini
 
Back
Top Bottom