Maboresho ya JF - 2019

Mzee baba
Naomba usisahau kuweka jukwaa la VIUMBE HAI na HADITHI NA SIMULIZI
 
Mara elfu kitufe cha Like kisiwepo.lakini Cha Dislike kiwepo

msisahau
Shida tunazozipata za ku Subscribe nyuzi yani sometimes hata uki View au ku like et unaunganishwa nao hiyo Inaboaaa

Uwezekano wa kuwepo na Thems tofauti,mtu uwe unajichangulia cyo mnatuchagulia Mara muweke blue Mara Nini, HAPANA them ziwe tofauti tofauti.

Then mfanye modify kwenye ku log in account mbili tofauti kwenye device 1.
hiyo nayo ni kero,

mwisho,mkiwa na maboresho ya ghafla muwe mna tu notify hata kwa emali zetu kuliko kutuachia presha

hhhh Mambo mengi mengineyo watachangia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu bora mfanye kama mimi jf yangu vi imoji havipo bora mviweke peupe kama watsap.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muiweke strong dhidi ya mashambulizi ya mtandaoni.

Maana mwakani uchaguzi mkuu, na kama unavyojua hakuna ITV, Star Tv wala taarifa za habari, hivyo JF ndio chanzo pekee kikuu cha habari kwa tulio wengi.

Mdumu sana!
Mkuu Ukifika Uchaguzi Tegemea Hilo, Hata wakiboresha vipi, Wakishindwa kuishambulia JF watalazimisha kufuta zile nyuzi ambazo kwao zitakua hawazipendi kuziona... Tegemea Hilo kutokea Hilo kwa asilimia 98.

Hii inanipa picha kutokana na wakubwa wanavyotutawala na Chama Chao.
 

Mkuu, nimeshatuma ombi uniunge JUKWAA LA WAKUBWA lakini ukani-ignore hukunipa hata jibu mkuu.

Kama kuna malipo ya kulipia sema basi nilipie uniweke huko, mambo mengine tunahitaji ku-share sio vizuri kufungua threads kwenye majukwaa ya kawaida kiongozi.

Natumai unafanyia kazi ombi langu mkuu. Na naomba kujua nikihitaji kuwa na rank kama gold au platinum member naomba taratibu zake na malipo yanakuwaje please.

Natanguliza shukran kwenu. Thanks.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…