Jamani mabondia wanacheza kulingana na uzito, maungo hayo mnayoyasema ni ya mabondia wa uzito wa juu kuanzia Light Heavy Kilo 79.37 au paundi 175 na kuendelea mpaka Heavy Weight kuanzia kilo 90 au paundi 175 na kuendela . Duniani kote kuna mabondia wa uzito mbali mbali ikiwemo wa chini. Mfano hawa wanacheza katika uzito wa Bantam ambao ni kilo 53.524, unategemea mchezaji wa uzito huu awe amejazia kama Evander Hollified! Kama mtamkumbuka Willy Isangura bondia wa Tanzania ambae sasa ni kocha alikuwa anachezea uzito wa juu yaani zaidi ya Kilo 90 au zaidi ya paundi 175, hamkuona alivyojazia.
Sasa si afadhali ya hawa kuliko wanaopigana katika uzito wa "straw" kilo 46, Mini Fly Kilo 47.6, Junior Fly Kilo 48.9, Fly kilo 50, Superfly/Junior bantam Kilo 52.16, na hawa bantam kilo 53.52.
Kwa kifupi bondia wa uzito wa bamtam duniani kote hawezi kuwa na umbo kama la Tyson au Evander. Tuwape moyo hawa vijana jamani tusiwabeze.