Mabomu yatumika soko la Nguzo nane-Shinyanga!

Mabomu yatumika soko la Nguzo nane-Shinyanga!

Hussein J Mahenga

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2012
Posts
756
Reaction score
661
Wanajf,naombeni nianze kuuliza swali hili,hivi serikali yetu haina njia za kidiplomasia kutatua ama kupata suluhu ya migogoro inayokuwa inajitokeza kati ya wananchi na serikali?

Nilichokishuhudia leo takribani masaa mawili yaliyopita,katika soko la Nguzo nane mjini Shinyanga,ni dhahiri kuwa serikali yetu ni ya kibabe.Hivi na wafanyabiashara wadogowadogo wamekuwa wa kufukuzwa kwa mabomu? Hivi haya mabomu hayana gharama hata yatumike kiholela namna hii!

Wanajf,nasikitika sana,kitendo cha serikali kuwafanya wananchi kuwa kama wanyama,hata Mungu hapendi.Wanajf mnasemaje katika hili?
 
Haaa, Polisi!!!.........hao ndo zao, wanashindwa kukamata majambazi na mafisadi waliosababishia taifa hasara na wimbi la umaskini kwa wananchi wanashambulia raia wema kwa mabomu na silaha za moto.
 
serikali yetu ipo kwenye kampeni ya kisirisiri kuwazoesha raia wake mabomu ili wayazoee
 
Wanajf,naombeni nianze kuuliza swali hili,hivi serikali yetu haina njia za kidiplomasia kutatua ama kupata suluhu ya migogoro inayokuwa inajitokeza kati ya wananchi na serikali?

Nilichokishuhudia leo takribani masaa mawili yaliyopita,katika soko la Nguzo nane mjini Shinyanga,ni dhahiri kuwa serikali yetu ni ya kibabe.Hivi na wafanyabiashara wadogowadogo wamekuwa wa kufukuzwa kwa mabomu? Hivi haya mabomu hayana gharama hata yatumike kiholela namna hii!

Wanajf,nasikitika sana,kitendo cha serikali kuwafanya wananchi kuwa kama wanyama,hata Mungu hapendi.Wanajf mnasemaje katika hili?
ungekuwa na nia njema unge anza kwa kueleza chanzo cha tatizo kuliko kuanza kwa kulaumu kabla hata yakutoa ripoti kamili.kitendo cha kulaumu upande mmoja katika mgogoro flani bila kuwa au kutoa taarifa za kutosha juu ya chanzo,historia,na hatua ambayo mgogoro ulikuwa umefikia ni ushabiki unaolenga kuchochea zaidi migogoro.ushabiki wa namna hii ni bora ukaachwa na watu wote wastaarabu kwani kuchochea migogoro na uhasama ni jambo baya kuliko mambo yote.
 
Mwambieni huyo kiongozi wenu aje ajifunze huku songea kuna jamaa anaitwa JJM mkuu ni full diplomasi hatumii hata unyasi anakuja kwa mguu mnachonga mnaelewana kesho mnahamia alipowaelekeza . Hakuna cha mabomu wala polisi kimyakimya staili.
 
Back
Top Bottom