Mabomu yatapigwa,misimamo itabaki

Mabomu yatapigwa,misimamo itabaki

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Kwenye msimamo wa moyoni,bomu au kutekwa au kuswekwa rumande au kuteswa au kushambuliwa kwa silaha nyinginezo, si lolote. Watu watafanyiwa madhila ya kila aina lakini watabaki na misimamo yao.

Watachagua wawapendao. Yatatokea yote lakini msimamo wetu kama watanzania wamoja na wenye misimamo kinzani itabaki. Wa kupenda chama tawala watatuwepo. Na wale wa upinzani hawatakosa. Msimamo wa kupenda hotuba,rangi za vyama,sera na mavazi yake chama fulani hautakosa.

Nchi haiwezi kuwa haina tofauti za kimtazamo na kisiasa.Hata enzi za chama kimoja upinzani ulikuwepo,seuse sasa? Siasa ituimarishe;isitubomoe.Itujenge kifikra,weledi na ubunifu.Tusonge mbele pamoja kama nchi.Hatahivyo,matukio ya mashambulio hasa katika harakati za kisiasa yapaswa kukomeshwa haraka sana.

Wananchi wakiendelea kupuuzwa maombi yao ya kuondolewa kero hii,watapuuza watakachoambiwa. Ikifikia hapo,nchi itakuwa hatarini. God forbids! Serikali na Vyombo vyake vya Usalama inaweza kutenda mema yake ya kawaida. Tunaisubiri itende na haki ichukue mkondo wake kadiri Sheria zetu zituongozavyo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.
 
Mmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmh yataka moyo sirahisi kama unavyo sema ila 2po pamoko
 
Back
Top Bottom