Mabomu ya Polisi yatanda Ubungo


Nakubaliana na mdau hapa!
 
Hakika watarudi tu, labda wawe wanawavizia ghafla ghafla.
Nchi hii shida kweli serikali ya ccm inamaamuzi ya kuangalia upande mmoja tu sijui hii namna wamekopi wapi?
 

Nakubaliana nawe lakini Watanzania wabishi, hata ukuwapatia nafasi nzuri ya kufanyia biashara hawatakwenda huko; tatizo letu atuheshimu sheria. Nawapa pole lakini wafuate sheria siyo kila mahali unafanya biashara tu hii siyo sawa.
 
Tutegemee roba za mbao zaidi mitaani.
 
Sheria mbona haitekelezwi kwa jengo la Tanesco ambalo liko ndani ya hifadhi ya barabara?
 

Jogi, ni serikali gani ambayo ingeingia madarakani na kuwaacha wamachinga wafanye biashara kwa style ile wanayofanya kama ile ya ubungo, ambapo hata pa kupita panakosekana? Hata ingekuwa ni serikali ya CHADEMA bado ingefanya hivyohivyo? Kuhusu hostel za mabibo kujengwa zilikojengwa hili jambo tulilihoji sana wakati ule tunatia mgomo Mlimani city isijengwe badala yake zijengwe hostel.
Ukweli ni kwamba mabibo hostel isingeweza kujengwa chuoni kwa kuwa ile ni investment binafsi ya NSSF. Kama NSSF wakiamua kubadili matumizi ya zile hostel, udsm watatakiwa kuondoa wanafunzi wao. So isingewezekana kuruhusu shirika binafsi lijenge kwenye eneo la chuo kama makubaliano si kuzikabidhi hizo hostell chuoni in the future kama ilivyo kwa mlimani city.
Kuhusu kugawana eneo la basi terminal sina idea yoyote, but naambiwa ile basi terminal inahamishiwa kibamba, sijui hili lina ukweli gani.
 
watarudi na kuruhusiwa kufanya biashara zao utakapokaribia uchaguzi mkuu mkuu 2015...!
 
Kuwaondoa ni sawa, kwa usalama wao wenyewe na raia wengine.
Lakini wazingatie kuwa hawa ni Machinga (Marching-Guys).

Ugomvi wangu ni mbinu za kuwatoa hapo, wanawatisha na mabaki ya mabomu ya Arumeru
 

pumba ulizochangia ni bora ungewapa kuku wakutagie mayai.
 
Nipo maeneo ya ubungo hali si nzuri hata kidogo
 
Iache ipigwe hiyo mijitu ya dar isiyopenda mabadiliko wao kutwa wameshikilia ccm kama vle walichanjwa chale za matak.oni na mwalimu nyerere au kawawa.
Badilikeni ndugu zangu wa dar saa ya ukombozi ndio sasa jamani.!
 
Nipo maeneo ya ubungo hali si nzuri hata kidogo
Kuna machinga wenye uchu wa maisha Dar? Machinga wako mikoani, wanaojua thamani ya kila senti wanayoipata. Hao ndio hata polisi hualika majeshi mengine kuwasaidia. Maana wanajua wanachokipigania. Sio hawa watoto wavivu waliokimbia shamba na kuingia Dar es Salaam.
 
hatimaye serikali imewaondoa wafanyabiashara wanaofanya biashara zao katika eneo la ubungo songas pembezon mwa barabara ya mandela.
 
Eti hamuondoki kwa kuwa kuna stand ya daladala,kota za tanesco n.k pia eti muonyeshwe pa kwenda! Kwani nani aliwaonyesha mje hapo Ubungo? Huo ni ubishi wa kizamani,umeme utakapolipuka mtageuza kibao na kulaumu serikali! Acheni hizo!
 
Hz ni njama maaskari wanaongozwa na Serikali ya CCM wanamalizia hasira zao kwa kuona kuwa CDM wanakuja moto juu c mmeona wenyewe huko Arumeru Mashariki na majimbo mengine wajiandae na waache kuwaharibia wananchi wa kipato cha chini au kwa sbb wao wana sehemu za kudaia posho hy kazi isiwape kiburi wananchi tukiamua tunaweza ohoooo.
 

Mkuu kuwahamisha wamachinga katika eneo lenye biashara ni KUKOSA AKILI YA BIASHARA..

Nilipiga kelele sana (hawa vichwa ngumu wa serikalini) wakati wanawaondoa wamachinga manzenze, mahakama ya ndizi na hata ubungo si support kabisa huu ujinga nitaeleza kwanini

a. Umajinga unatoa ajira isiyo rasmi kwa vijana wengi sana Tanzania dawa si kuwaondoa bali kuondoa zile nyumba, taasisi etc zilizokaribu na centres za wamachinga mfano. mazense serikali ilitakiwa inunue na kuhamaisha makazi ya watu pale na kuweka soko kubwa pale vilevile ubungo jengo la tanesco na maujinga yao waondoke wamachinga watengenezewe utaratibu wa kuwa na soko lao pale..

b. Turnover, in terms of cash transaction and services provided per day maeneo ya machinga ni kubwa sana ni uhai kwa taifa na kwa wananchi wake hasa kodi kwakuwa mazao na huduma zinauzwa maeneo hayo..

Serikalini tatizo lao hawajawahi kufanya kazi za biashara mtu amekuwa officer wa kufukuzia allowances hawezi kujua business preposition na faida itokanayo ndio maana wanaweza kuja na amri za kijinga kama hizo..ndio maana tunataka rais mmachinga sio professional politicians ..soma signature yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…