Mabomu, risasi za moto vyarindima Dar, Mbeya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabomu, risasi za moto vyarindima Dar, Mbeya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Nov 13, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Ni mpambano mkali Polisi, wanafunzi UDSM, Wamachinga

  [​IMG] 13 wajeruhiwa, walazwa, 46 watiwa mbaroni  [​IMG]
  Polisi akimpiga mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu ch Dar es Salaam jana baada ya kuandamana kushinikiza kupewa mikopo.


  Majiji ya Dar es Salaam na Mbeya jana yaligeuka uwanja wa vita baada ya polisi kutumia mabomu ya machozi na risasi za moto kwa saa kadhaa,

  kuwatawanya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga.
  Jijini Dar es Salaam, UDSM ilikuwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi kwa zaidi ya saa nane, baada ya wanafunzi kugoma kuingia darasani kushinikiza wenzao wa mwaka wa kwanza ambao walikosa mikopo wapatiwe.

  Waliokosa mikopo ni zaidi ya 1,000 ambao walichaguliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), kujiunga na chuo hicho lakini hawakupata mikopo kutoka katika Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELB).
  Katika sakata hilo, Polisi ililazimika kuwatawanya wanafunzi hao kwa kutumia mabomu ya machozi na kuwatia mbaroni 46.

  Baadhi ya wanafunzi hao walibeba fimbo na wengine mabango yenye ujumbe mbalimbali ukiwemo uliosomeka: "Watoto wa vigogo wanapata mkopo ila wa wakulima wananyimwa, hali ngumu ya maisha nchini mpaka lini. Fedha za kuilipa Dowans zitumike kuwasaidia wanafunzi waliokosa mikopo."

  Wanafunzi hao waliendelea kukizunguka chuo hicho na kwenda kupiga kambi katika eneo la jengo la utawala na kuwazuia wahadhiri wao kutoka wala kuingia.

  Baada ya hapo, wanafunzi hao walijikusanya na kuanza kutoka na kuelekea eneo Ubungo Maji na ndipo Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), kilipotumia mabomu ya machozi kuwatawanya na baadhi yao kuwakamata.
  FFU walifika chuoni hapo wakiwa katika magari manane likiwemo la maji ya kuwasha huku askari wa doria wakitanda kila eneo la chuo hicho wakiwa na silaha mbalimbali.

  Mmoja wa wanafunzi hao waliofanya mgomo, Hellen Makawia, alisema madai yao ni wanafunzi wa mwaka wa kwanza kunyimwa mkopo licha ya kwamba wamechaguliwa kujiunga chuoni hapo.
  Alisema serikali iliwatangazia kuwa bajeti yake haijitoshelizi jambo ambalo wamelipinga na kuhoji: "Iweje serikali ikubali kuilipa kampuni ya Dowans.

  Je, hizo fedha wanazitoa wapi. Na ni kwa nini deni hilo lisitumike kuwasaidia wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na chuo ambao kwa sasa wamekatisha masomo yao na kurudi mkoani."

  Bruno Thomas, alisema mgomo wao utaendelea mpaka kieleweke kwani wanachotaka ni kuona haki ikitendeka na sio serikali kutumia vyombo vya dola kuwapiga kwa mabomu.

  Alisema askari hao wamewaingilia uhuru wao na kuingia ndani ya chuo hicho na kuanza kuwapiga kwa mabomu licha ya kwamba mgomo wao ni wa amani.

  "Serikali iliweza kuongeza bajeti yake katika Wizara ya Nishati na Madini, iweje ishindwe kuongeza bajeti ya mikopo kwa wanafunzi ili waendelee na masomo?,” Alihoji Thomas.

  Aliwatuhumu polisi kwa kuwapekua na kuwaibia vitu mbalimbali zikiwemo simu za mikononi.
  Wakiwa katika eneo la utawala, wanafunzi hao walitaka kauli ya Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mkandala.
  Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo (Utawala), Profesa Yunus Mgaya, alisema zaidi ya wanafunzi 1,000 walipata nafasi ya kujiunga

  chuoni hapo, lakini walikosa mikopo kutoka Bodi ya Mikopo.
  Profesa Mgaya alisema bajeti ya serikali iliyotengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi ni kidogo na kwamba isingeweza kutosheleza idadi ya wanafunzi wote.

  Mgaya alisema awali wanafunzi hao waliandamana hadi serikalini ambapo walijulishwa kuwa suala lao ninafanyiwa kazi ambapo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alilitolea tamko na kueleza kuwa bajeti ya mwaka huu haitawezekana kuwabeba wanafunzi wote na kuwataka watafute utaratibu mwingine wa kujisomesha.

  Alisema baada ya kauli hiyo, kikundi cha wanafunzi wachache kilikutana na kufanya shinikizo la mgomo kushinikiza suala hilo.
  Profesa Mgaya alisema baadhi ya wanafunzi walikutana juzi ambapo katika kikao chao waliridhia kugoma na ndipo jana wakahamasisha wenzao kutoingia darasani.
  Profesa Mgaya alisema wanafunzi hao walikuwa hawaingii darasani na kwamba walikuwa wakizungukazunguka chuoni hapo kwa kuwa walikuwa hawana usajili.

  46 WASHIKILIWA

  Kamanda Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, alisema katika tukio hilo wanawashikilia wanafunzi 46 na kwamba hawatarajiwi kuachiwa hivi karibuni kwani wanaendelea na mahojiano na baada ya hapo watachukuliwa hatua kali.
  Alisema walilazimika kutumia mabomu kutuliza ghasia na kwamba njia waliyoitumia ni sahihi kwa sababu wanafunzi walishindwa kutii agizo la kuacha maandamano.

  Wambura alisema wanafunzi hao walitakiwa kufuata utaratibu katika kufikisha malalamiko yao kwa mamlaka husika na sio kufanya vurugu.
  Jijini Mbeya, Polisi walipambana na kundi la wamachinga, ambao walianzisha vurugu kubwa na kufunga barabara Kuu ya Tanzania - Zambia

  (Tanzam), katika eneo la Mwanjelwa, wakipinga kuondolewa katika eneo hilo bila kupewa eneo lingine la kufanyia biashara, hali ambayo ilisababisha Jeshi la Polisi kuingilia kati na kuanza kuwafyatulia mabomu ya machozi na risasi za moto kwa siku nzima ya jana.
  Vurugu hizo zilianza saa 3:00 asubuhi, baada ya mgambo wa Jiji kufika katika eneo hilo na kujaribu kuwakamata baadhi ya wamachinga

  waliokuwa wameweka biashara zao kando kando ya barabara na kuwauzia wapita njia.
  NIPASHE lilishuhudia vijana waliochanganyika na wamachinga hao wakifunga barabara kwa mawe makubwa na kuchoma matairi ya magari

  barabarani, huku Polisi nao wakijitahidi kufungua barabara hiyo bila mafanikio.
  Hali ilizidi kuwa mbaya baada ya Polisi kuanza kufyatua mabomu ya machozi na kusababisha wamachinga hao kujibu mapigo, kwa kuwarushia askari mawe hali iliyosababisha watu kadhaa kujeruhiwa na baadhi yao kukimbizwa hospitalini.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2011
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ...inasikitisha!!
   
 3. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Haya yote yana mwisho tu!
   
Loading...