franklin12xx
Member
- Sep 24, 2014
- 28
- 31
Hakika naanza kuamini kuwa CCM wanaanza kuona bao la mkono mwaka huu halipigiki hivyo wanajaribu kuwaogopesha wananchi kwa njia hizi baada ya kuona upinzani kwa hakika mwaka huu umepata nguvu ya aina yake na kuungwa mkono na wananchi wa kawaida wengi na ambao ndio wapiga kura wa nchi hii.
Hili swala haliingii akilini maana kwanza maandamano hayapo kila siku na ratiba ilishatolewa kuwa siku flani atakuwa dar, then mbeya, then arusha, and then mwanza. Wananchi wamechoshwa na mambo ya kunyimwa haki zao za msingi na CCM na tumaini lao lipo upinzani na kwa bahati nzuri, mtu aliyesimamishwa (Lowassa) ni kipenzi cha watanzania hivyo kwanini wananchi wanyimwe haki yao ya kikatiba kumlaki, kumshangilia na kumsikiliza mtu ambaye ndiye tumaini lao.
Haingii akilini clouds wanapotangaza kwa mfano "dar live kutakuwa hapashikiki leo - wakiwa wanatangazwa wasanii kama diamond, ali kiba na wengine wengi" je si panakuwa na msisimko na watu wengi, kwasababu huyo ni kipenzi cha watu na wameshatangaziwa siku maalum hivyo polisi jukumu lao ni kulinda amani maana ni kiu ya wengi, au Obama alivyokuja watu pia Obama alivyokuja watu si walikuwa wengi sana, ila taarifa ilitolewa mapema na watu walijitokeza kumwona mtu aliyeandika historia marekani kama mtu mweusi wa kwanza kuwa rais wa marekani.
Vivyo hivyo kwa Lowassa, ni tumaini la wengi ambao wamechoshwa na ukoloni wa mtu mweusi (CCM), hivyo watu hawana budi kujitokeza kumlaki mtu wao. Je na kwanini matangazo ya polisi au nguvu ya polisi inatumika kwa upinzani tu, je Magufuli wakati anatambulishwa polisi mbona hawakurusha mabomu au kwasababu anafunikwa kila mahali.
Hii si haki na hakika hii hali ikiendelea amani ya nchi hii itatoweka maana watu wamechoshwa na wimbo wa kila siku wa CCM, kuwa ni chama kitakacholeta maendeleo. Tangia uhuru mnatawala nyinyi tu, zaidi ya miaka mnatawala ninyi tu lakini :
1. Zaidi ya nusu ya watanzania hawana maji safi na salama wakati maziwa na mito ni baraka yetu.
2. Zaidi ya nusu ya watanzania bado hawajafikia na umeme majumbani mwao.
3. Rushwa iliyokithiri katika ofisi za serikali.
4. Ramani za majiji zipo ila rushwa iliyotawala hasa dar es salaam, ramani hizo hazifuatwi na ndio tatizo la migogoro ya ardhi, mafuriko kila mvua zikinyesha, maji machafu kutuama kila mahali.
5. Elimu duni pamoja na ukosefu wa vyumba vya madarasa, vyoo na madawati wakati misitu imejaa.
6. Kodi zinaongezeka kila kukicha wakati matokeo ya ukusanyaji huu ni kulisha vigogo pamoja na kulipa posho za vikao na safari badala ya maendeleo ya watanzania.
7. Dawa mahospitalini ni tatizo, huku deni MSD ni shida zaidi wakati mabilioni BOT na Tamisemi yanakwapuliwa tu huku wahusika hawashugulikiwi.
8. Kupitisha mambo bungeni kwa lugha ya "wanaoafiki waseme ndio na wasioafiki waseme hapana" kwa kupendelea maslahi ya CCM "wakoloni weusi"
Hivi kweli watanzania hawa wenye shauku kubwa la maendeleo wasijitokeze kumlaki mtu ambaye wanaamini ndiyo tumaini lao. Ifike mahali utashi utumike badala ya mashinikizo toka kwa viongozi wasio waadilifu na wasioitakia mema nchi hii. Mwaka wa mabadiriko ndio huu, tarehe 25 October, piga kura yako kwaajili ya maendeleo ya nchi hii.
Mungu ibariki nchi yetu. Viva Lowassa!! Viva Ukawa.