Mabishano yaibuka mahakamani kushikiliwa kwa Manji

Donep

Member
Feb 22, 2017
35
53
Sakata la kushikiliwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini, Yusufu Manji limeendelea kuchukua sura mpya, safari hii yakiibuka mabishano Mahakama Kuu baada ya Serikali kukana kumshikilia.

Yusuph.jpg


Mabishano hayo yameibuka jana kati ya mawakili wa Serikali na mawakili wa Manji baada ya mfanyabiashara huyo kufungua maombi juma lililopita akihoji uhalali wa kushikiliwa na Uhamiaji.

Manji aliyefungua maombi hayo mahakamani hapo kupitia Wakili wake Hudson Ndusyepo, anaiomba mahakama iiagize Uhamiaji afikishwe mahakamani ili mahakama iamue uhalali wa kushikiliwa kwake na kisha iamuru aachiwe huru.

Kutokana na maombi hayo, Jaji Ama-Isario Munisi, aliwaamuru wajibu maombi kuwasilisha hati zao za kiapo kinzani dhidi ya maombi hayo na kupanga kuyasikiliza jana mchana.

Wajibu maombi ni Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam.

Hata hivyo jana Serikali katika majibu yake kupitia hati ya kiapo kinzani cha Ofisa Uhamiaji, Anorld Munuo, ilikana kumshikilia mfanyabiashara huyo. Mbali na kiapo hicho, Wakili Mkuu wa Serikali, Oswald Tibabyekoma, alisisitiza kuwa mfanyabiashara huyo hashikiliwi na yuko huru.

Maelezo hayo ya Serikali yalipingwa vikali na mawakili wa Manji, Alex Mgongolwa na Hudson Ndusyepo, ambao kwa nyakati tofauti walisisitiza kuwa hadi jana mfanyabiashara huyo alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan, kwa matibabu, akiwa chini ya ulinzi wa maafisa Uhamiaji.


Chanzo: Mwananchi
 
Kama Mimi ningekua Magufuli, ningehakikisha baada ya kuindoka madarakani wore mnanikumbuka na kugundua kuwa nilikua kiongozi mzuri wa aina take.
Ili kufanikisha hilo ningehakikisha napambana kuhakikisha Makonda ndiye anakuwa rais ajaye.
Lazima mtani miss tu.

Hiyo ndiyo falsafa ya viongozi wa kiafrika
 
Mara Nyingi Serikali za Kibabe na Jeuri zikiweka Watu Kizuizini ( Sio Mahabusu) huwa zinakanusha kuwashikilia.

Manji yupo Kizuizini sio Mahabusu

....Hao uhamiaji wana mamlaka ya kumuweka mtu kizuizini? Haya ndiyo mambo ambayo Lissu amekuwa mstari wa mbele kabisa kuyapigania kwa faida ya watanzania wote.
 
Viongozi wa kiafrika wakishaka madaraka wanaona kama wamezununua hizo nafasi na kuwa mali yao.....
 
Yaani hii Tanzania serikali inaboa sana .... tz haina furaha sabb ya serikali ... yaani tunazidiwa na Syria na hata somalia.... sisi ni wa153, inakuja Burundi na mwisho sijui Africa ya kati.... kuna kosa kubwa sana kwenye utawala wetu... hutujawahi kuwa vitani(civil war) lakini watz hawana furaha kwa nn???? Na JPM ndo kaja kuharibu kabisaaaa.....angejua jana kawaumiza wangapi kwa maneno yake na kuwanyima furaha wengi angejirekebisha.....
 
Awamu ya tano itasalia kwenye historia kama awamu mbovu kabisa ya utawala kuwahi kutokea katika nchi ya Tanzania.
 
nilishuhudia kabisa maafisa wawili wa uhamiaji wapo nje ya wodi kwa ajili ya Manji. Tena niliambiwa wanapokezana zamu. Kuna wakati baadhi ya watu wanaokuja kumjulia hali Manji huhojiwa na hao jamaa. Sasa hii ni kituko leo kukana kwamba hayupo kizuizini
 
Back
Top Bottom