Mabinti walioungana mwili kusoma Jangwani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mabinti walioungana mwili kusoma Jangwani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 30, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MUNGU hatupi mja wake na ulemavu si mwisho wa maisha, kwani sasa wanafunzi wawili wa kike yatima na wakazi wa hapa ambao wameungana kiwiliwili watajiunga na sekondari ya Jangwani ya Dar es Salaam baada ya kufaulu vizuri mtihani wa kitaifa wa darasa la saba ambao matokeo yake yalitangazwa hivi karibuni.

  Wanafunzi hao Maria na Consolata Mwakikuti wenye umri wa miaka 13, wamesema ndoto yao ni kuona wanakuwa wataalamu wa kompyuta waliobobea.

  Hata hivyo, walezi wa wanafunzi hao, wameomba wanafunzi hao wasomeshwe na Serikali katika shule binafsi ya Nyota ya Asubuhi iliyopo Kidabaga wilayani Kilolo, Iringa, kutokana na hali yao ya kimaumbile ilivyo.

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Getrude Mpaka, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mkoa wa Iringa ya kuchagua wanafunzi wanaojiunga kidato cha kwanza, alisema jana kuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imepanga wanafunzi hao wajiunge Jangwani kwa sababu shule hiyo ina rasilimali za kuwawezesha kusoma kwa ufanisi.

  Hata hivyo hakuzitaja. Kwa mujibu wa mmoja wa walezi wa wanafunzi hao, Dk Allesandro Nava wa hospitali ya Misheni ya Ikonda wilayani hapa, ili waweze kusoma kwa ufanisi, wanafunzi hao wanahitaji nyumba maalumu, chombo maalumu cha kuwapeleka na kuwarudisha shuleni na kuishi na mlezi kipindi chote cha shule.

  Hata hivyo, Mpaka aliwahakikishia walezi na wanafunzi hao kwamba wanafunzi hao wanaweza kusoma katika mazingira yao wakiwa Jangwani.

  “Nichukue fursa hii kuwaomba wadau wawasaidie watoto hawa kupata mahitaji yao yote muhimu ili waweze kutimiza ndoto zao,” Mpaka alisema wakati akitoa zawadi kwa wanafunzi hao baada ya kufaulu.

  Zawadi hizo zilizotolewa kwenye hafla ya kuwapongeza iliyofanyika katika ukumbi wa hospitali ya Ikonda mbele ya walezi wa watoto hao waliopoteza wazazi wao wote wawili wakiwa wachanga ni pamoja na mablanketi, mashuka, vifaa vya shule na vyakula.

  Katika mtihani huo, wanafunzi hao ambao mmoja huandika kwa kutumia kifua cha mwenzake kama dawati na mwingine akitumia dawati wawapo darasani, wote walipata alama 151 huku wakitofautiana katika somo la Sayansi ambapo Maria alimzidi Consolatha kwa kupata alama 31 dhidi ya 29.

  Taarifa iliyotolewa na Dk Nava ilisema jitihada za madaktari wa ndani na nje ya nchi za kuwatenganisha hazikufanikiwa kwa kile ambacho kimekuwa kikielezwa, kwamba wakitenganishwa, lazima mmoja au wote wapoteze maisha.
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  "Jangwaani shule yetu,
  jangwaani twaipenda,
  jangwani yasifiika,
  popote tanzania..
  Tuwe na midomo mifupi na kusema kidogoo...
  Taamka..
  Maneno machache, yaliyo na hekima na busaraa."
  nilikuwa najaribu kukumbukia my school song.

  Wakasome jangwani.
  Kuna hostel hivyo watakuwa wanaishi humo humo ndani ya chuo.
  Pia
  Huwa kuna misaada wanapelekewa watoto wenye matatizo kama hayo pale.
  Matron atakuwa mlezi wao na natumai watapata support kwa wanafunzi wenzao.
  Nawapa hongera na mungu awabariki sana.
   
 3. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  mmh maajabu ya Muumba hayo....Mungu atawasaidia ...
   
Loading...