Naungana nawe Mwanakijiji kuwa Marando si TISS na wala hajawahi kuwa agent. Maagent wa TISS tunawafahamu na CHADEMA pia inawajua na wnegine tayari wapo ndani ya Chama.
Mimi nimemfahamu Marando kwa muda na nilijua kuwa atasuport CHADEMA kwenye uchaguzi toka mwezi wa tatu. Ila sikujua kuwa atajiunga rasmi kama Mwanachama.
Sasa tuongelee potentiality ya Marando:
1. kwanza kuwepo kwake kutahakikisha jimbo la Rorya linaenda CHADEMA (atakayebisha kwenye hili asubiri Octoba 31).
2. Ataisaidia sana CHADEMA kurejesha jimbo la Tarime ambalo kwa bahati mbaya sana CHADEMA ina kila dalili ya kulikosa kutokana na migongano isiyo ya lazima (infighting kati ya Mwikabe, heche na Mwera).
3. Mabere atakuwa msaada mkubwa sana kwa SLAA kwa kanda ya Ziwa maana anaheshimika sana.
4. Marando is a reputed public orator na anaweza kuteka masikio na kura za wasomi.
5. Marando hagombei uongozi wowote katika CHADEMA wala nchi so CHADEMA haina cha kupoteza.
Mimi si mshabiki wa personalities za watu ila imenibidi niseme kuweka records straight.
Atavuruga tu kama akipewa uongozi wa ngazi ya juu, lakini akiwa mwananachama wa kawaida as I predict atavurugaje????????
Siyo kweli kuwa mwanachama wa kawaida hawezi kuvuruga. Mifano iko mingi. Anaweza kukiburuza chama mahakamani au kufanya vurugu kwenye chama hasa ikiwa ametumwa na serikali kufanya hivyo. Sasa akiwa tena wakili aliyebobea ni tatizo moja baada ya lingine. Chadema na vyama vingine viunde kamati ya uthibiti, na siyo kumpokea kila mja. Mnamkumbuka Lenin? Better few but Better!
Mrema habebeki, muache kumpakazia Mabeleje waliyoyafanya kwa Mrema mpaka akawa kama alivyo leo hayatajirudia huko Chadema?
Namkumbuka Marando alipotuhamasisha kuandamana kwenda ikulu toka viwanja vya jangwani, nakumbuka tukiwa mstari wa mbele huku tumeshikana mikono tulipofika maeneo ya DIT iliyokuwa Dar Tech FFU waliokuwa wamejipanga mbele yetu barabara ya Bibi Titi wakatoa kitambaa chekundu. Nakumbuka vizuri baada ya mabomu kupigwa tulivyoruka lile geti la Dar Tech na Marando tukajikuta tumo ndani ya uzio wa Dar Tech.
Namkumbuka tena Marando kule Laskazone Tanga alivyoamlisha taa zizimwe na meza ya Mwenyekiti wakati huo Mrema Ikabinuliwa ili uchaguzi uvurugike. Nikiunganisha na sakata lake la kuwania Ubunge wa EAC alivyopigiwa kampeni la nguvu na CCM, mmhuu sijui labda mimi ndiye simwelewi vizuri huyu jamaa.
Lakini all in all sina tatizo na Marando kujiunga Chadema kwa vile naelewa ndani ya Chadema kuna watu makini watakuwa wameangalia pros and cons. Namjua Marando ni mwanamageuzi halisi aliyepotea, atulie aonekane anakijenga chama kama alivyotulia Lwakatare, vinginevyo kama atakuja na lake atajulikana muda si mrefu, Chadema huwa haichelewi kumwonyesha mtu mlango.