Mabele Marando aliondokaje Usalama wa Taifa?

Status
Not open for further replies.
Mabere Nyaucho Marando alikuwa mwajiriwa wa UWT tangu enzi za Mwl Nyerere.Mabere Marando alikuwa ni miongoni mwa watu wa mwanzo kudai mfumo wa vyama vingi kabla ya mfumo huo kuruhusiwa rasmi.

ila nasikia usalama wa taifa huwa hawastafu!
 
nadhani ile hati ya kuwa mwanausalama hawaitumii iapsavyo, na hiyo ni baada ya kuwa usalama imekuwa ikiajiri watoto wa vigogo tu wasio na sifa
 
ile dhana nzima ya kuwa mwanausalama imepotea
 
Mrando kuwepo ndani ya Chadema ni usalama kwa chadema pia, huwezi kujua awzee wametulia naye kwa amani kabisa , lazina kuna jambo. Ila kwa jinsi ccm ilivyo chokwa kazi ya usalama wa taifa itakuwa kunangalia nani wa kusimama naye tena kwani UWT hawana chama ni serikali.
 
UWT imeshikilia kazi moja kubwa ya kulinda serekali ya CCM isiondoshwe madarakani.
The Following User Says Thank You Ngongo For This Useful Post
Sigma
(Today)
 
Wakuu,

Hivi kwanni tusijiulize ni nani anaewapa CDM taarifa za ndani na SIRI za UWT kama sio watumishi wa chombo hicho wenye nia njema na nchi yetu?

Nadhani mtakumbuka gazeti la MWANAHALISI lilipoanika mawasiliano ya Zito, Zoka, na Rostam. Ni dhahiri Uwepo wa Kamanda Marando ktk CDM ni turufu muhimu sana ktk Kampeni ya kuchukua Nchi yetu.
 
Marando pambana na ikiwezekana uwataje wanaohusika na ununuzi wa mitambo iyo,km ulikuwa usalama wa taifa i dnt care coz n past nw and ushakuwa mtetez endelea kufumbua macho watanzania,2015 chadema w wll make it!
 
Aliondoka Usalama wa Taifa akipunga Mkono ! Usalama Wa Taifa ni Kazi tu , na wakifika umri wa kustaafu wanastaafu na kula pension kama waajiriwa wengine.

Ni Ujinga kama si wehu kusema eti hawastaafu !
 
Nadhani yeye mwenyewe atakuwa na majibu mazuri zaidi; ila kumbukumbu zangu zinaonyesha kuwa mara baada ya Mzee Mwinyi kushika kiti cha ikulu, mojawapo ya mambo aliyotaka kuhakikisha ni kuwa watu wa usalama wa taifa ni watu wake wa karibu. Kwa hiyo Mzee Timothy Apiyo aliondolewa Ukatibu Mkuu ikiwa ni pamoja na maafisa wengi sana wa usalama wa taifa; nadhani Marando alikuwa ni mmoja wa maofisa hao kwa vile ni kipindi hicho hicho ndicho alichoanzisha NCCR. Kuna marafiki zangu ambao walikuwa huko TISS walioachana nayo kipindi hicho, na wengi wao ni wafanyabiashara binafsi Dar, na wengine wao wakiwa wamehamia ughaibuni. Mtu imara ambaye najua kuwa ilikuwa ni lazima abaki pale kutokana na utaalam wake kwenye mambo ya ujasusi ni jamaa mmoja aliyekuwa akiitwa Walingozi. Jamaa huyu alikuwa ni professional pekee katika medani hiyo ya ujasusi na wala sijui leo atakuwa kawekwa wapi. Bwana yule alikuwa anajua kudakua habari kutoka katika mazingira yoyote tena kwa ufasaha mzuri bila makosa yoyote; alichohitaji ni kuwa na clear objective tu basi mengine yote atakukwapua bila wewe mwenyewe kujua
 

Una uhakika na unayoongea hasa hili la kulinda viongozi na chama tawala kising'olewe madarakani???kama ndio na wale uwt mliokua mkidai wanareport kwa "rais slaa" wanamlinda nani na chama gani??

Naungana na wewe kwenye uwt yetu kujikita kwenye economic intelligence and espionage,tiss lazima wajipange na kutafuta namna ya kuusaidia uchumi wa tanzania,lakini wakifanya hivyo tukumbuke tuna wanasiasa uchwara hapa nchini ambao hawatasita kudai kwamba jamaa wanakisaidia chama tawala kutekeleza sera zake,ndio matokeo ya mfumo wa vyama vingi tulioingia kichwa kichwa hayo,lakini kiukweli uwt/tiss wanatakiwa kujikita katika kufanya ujasusi wa kiuchumi na pia kudhibiti ujasusi wa kiuchumi dhidi ya tanzania ambao nina hakika tunafanyiwa sana na jirani/wapinzani wetu kiuchumi,hapa nawazungumzia RWANDA,KENYA na UGANDA

Lakini ninazo taarifa kwamba tiss walishafanya mipango kabambe ya kuutendea haki uchumi wetu lakini wakakumbana na vikwazo kibao mfano kulikuwa na proposal za kusaidia makampuni ya wazalendo lakini baada ya kufanyika vetting ikaonekana kuwa baadhi ya hao wanaoitwa wazalendo wenye makampuni hawakuwa na mpango wowote wa maana wa kuusaidia uchumi wetu zaidi ya wengi wao kuwa ma opportunist tu ambao hawafai hata kuwasaidia kwani wanaongoza kwa kudodge Tax, ni wahujumi uchumi wetu tu tiss wakakwama,kwa hiyo wakati mwingine tusiwasakame sana tiss,sisi wenyewe hatuko tayari kuusaida uchumi wetu kwa kutimiza wajibu wetu-kulipa kodi wabongo hatupendi,huo ndio ukweli hata wakija chadema watauface

 

Ama kweli... kwa ufafanuzi huu.. na ww hawavumi lakini wamo....
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…