Mabeki tatu kumbe wamo kwenye mauno...

Asili100

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
240
181
Habari za mapumziko marefu wakuu?

Katika haya mapumziko na mimi nilipata kualikwa pahala kwenye family day ya moja ya makampuni makuuuuuubwa tu hapa nchini na jinsi tulivyoshehereheshwa naweza kusema wenzetu hawa si haba katika msuko suko huu wa uchumi (makampuni mengi yamekata garama kama hizi za mwisho wa mwaka) basi wao wameokota dodo kwenye mnazi kwa kupata faida mara dufu dufu, maana si kwa kula na kunywa kule, watoto wakafurahia michezo na wasanii wakaalikwa (naambiwa haijawahi kutokea).

MC wa family day ile alikua Masanja wa ze komed, basi ikawadia muda akasema jamani pamoja na kufika kwa wingi leo hapa na watoto lakini tuukumbuke uwepo wa hawa dada zetu wa kazi tunaowaachia watoto mchana kutwa huku sisi tukiwa maofisini tukizitengeneza hizo shilingi. Basi likaandaliwa shindano, wadada hao wapande pale wajiachie wawezavyo kwa kunengua nyimbo zitakazikua zinapigwa na DJ na kutakua na mchujo hadi apatikane mshindi ambae ataondoka na hela taslim (ingawa wote waliopanda jukwaani takribani wadada 40 hivi walipewa zawad za ujumla).

Masanja akawashukuru kwa kazi yao ngumu huko majumbani na akawaambia leo wako off, wajiachie wasiogope maboss wao maana leo ni siku ya furaha.... ikapigwa Salome pale ya bwana Dai, watoto wanapiga step kama walikuwepo kwenye mazoezi ya ule wimbo, ikafika ile sehemu ya 'chambua kama karanga salomeeee' doooooooooh mauno yakamwagwa hapo wallah si nikapigwa na butwaa.... chini wanaenda, pembeni wanaenda, facial expression ndio kabisaaaa, kuna mama jirani yangu alishangaa kumuona dada wake akiumudu wimbo tena akaropoka ''huyu sofi kajulia wapi hizi step''....

Mbaba mmoja yakamshinda huko alipokua akajinyanyukia kwenda kumtunza m,oja wa wadada (mpaka naandika huu uzi sikujua kama yule alikua mfanyakazi wake au kama alipata ruhusa ile toka kwa wife) nadhani mkewe alimwelewa kama wa kwangu alivonielewa pale niliporopoka yangu, sijui kama huu mwaliko nitaupata tena mwakani. Ila vitoto vilinikosha kwakeli Masanja alichangamsha sherehe ile kwa ile segment.

My take;
Tuna vipaji vingi sana huko majumbani mwetu, tunavipotezea tu. Msiishie kuwatumia tu kwa kazi na maujira madogo, vumbueni na mambo kama haya. Ingawa nilimskia dada pembeni yangu akisema kuanzia jumamme naondoka na rimoti, hii itakua tv inamuharbu. Vipi nawe mtazamo wako ndugu juu ya hili.
 
Kama mama mwenye mji hawezi kukata mauno kama beki 3 wake kibarua cha beki3 kinaota nyasi maana me uwa hatucheleweshi mambo
 
Wanajua kuliko hata mama wenye nyumba, nyie waoneni hivyo hivyo tu
 
Aiii nakumbukaga nikiwa mdogo mama alimfukuza maana yule dada ningempata ukubwani....... yaani anaweza kuganda huku kiuno kikienda kama mtu anayepepeta mchele na ungo
 
Back
Top Bottom