Mabasi yatozwa faini kwa kupandisha nauli ubungo

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,280
2,000
Hali ya usafiri katika kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo (UBT), imerejea katika hali ya kawaida baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), kuruhusu mabasi ya Coaster kutoa huduma na kupiga faini ya shilingi 250,000 mabasi ambayo yalijaribu kutoza nauli tofauti na bei iliyopangwa na mamlaka hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na msemaji wa Chama cha Kutetea Abiria (CHAKUA), Gelvas Rutanguzinda, alisema hali ya usafiri imeimarika baada ya mamlaka husika kusimamia na kuchukua hatua kwa wale wanaokiuka sheria ya usafirishaji.

“Mamlaka zimeanza kuchukua hatua kali dhidi ya mabasi yanayopandisha nauli kinyume cha taratibu. Kuna mabasi mawili yamepigwa faini kutokana na kukiuka sheria za kupandisha nauli, mabasi ambayo leo yalipandisha nauli yalilazimishwa kutoondoka katika kituo hiki na kuwarudishia abiria kiasi cha fedha ambayo iliongezwa na mabasi hayo kulazimika kutozwa faini ya Shilingi 250,000 kwa kila basi, na ni yale yanayofanya safari za Arusha, ambayo ni KVC Safari na Ibra Line ,” alisema Rutanguzindu.

Aidha alisema abiria wapatao 10 wa basi la Ibra Line na 38 wa KVC Safari walikatiwa tiketi kwa bei ya Sh, 40,000 badala ya 32,000, lakini walirudishiwa nauli zao baada ya mamlaka husika kuyazuia mabasi hayo kuondoka kituoni.
 

lyinga

JF-Expert Member
Nov 18, 2013
2,498
0
Serikali kama kweli wangekuwa wanawajali wanachi wake wangefufua usafiri wa treni ni mamilioni mangapi wanapoteza kwa kuangalia pua badala ya kuangalia mbele mimi naamini usafiri wa treni ungalikuwapo hata sisi makabwela tungesheherekea sikukuu na pamoja na nandugu jamaa na marafiki nazungumzia mikoa ya kaskazini ambapo reli ilikuwepo zamani wakaiuwa we embu fikiria upo wewe mwenza wako na watoto km wanne mnataka kwenda kula sikukuu mkoani nauli kila kichwa elfu45 mpaka 50 hapo hamjala bado ya kurudia kama ingelikuwa usafiri wa treni ingeyupa nafuu sana kwa mimi naona mamlaka za usafiri tz hazijasimama vizuri mahali pake zimejaa siasa na umimi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom