Mabasi yatokayo Ubungo ndani, sasa kuzungukia Shekilango

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,481
TANGAZO KWA UMMA

Kuanzia Tarehe 08/04/2016 Siku ya Ijumaa Mabasi ya Mikoani yanayotoka ndani ya Kituo chetu cha Ubungo Yataanza kutumia Mzunguuko uliyosanifiwa wa Shekilango kwa kuzunguuka nyuma ya Kituo cha Mafuta cha Total (Nyuma ya Soko la shekilango) wakati wa kuanza safari zao za Mikoani.

Eneo lililokuwa limeachwa wazi kwa muda lililokuwa linayapitisha Mabasi kwenye barabara za BRT litafungwa rasmi ili kuwezesha Mabasi ya DART ambayo yameanza mazoezi kutokuwa na muingiliano na chombo kingine cha Usafiri kwenye barabara hizo. Uwazi utakaofungwa ni ule uliopo mkabala na Geti la kutokea na ule wa geti la Kuingilia. Aidha eneo la wazi kwenye Kituo cha DART Ubungo maji ambalo lilikuwa linatumiwa na Watumishi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Kuingia kwenye Jengo hilo Utafungwa pia.

Waliokuwa wakitumia uwazi huo wanashauriwa kutumia Usanifu wa mzunguuko ulioko eneo la Kimara Kibo (Rombo) kufanya tendo la kubadili uelekeo (Turning)

TAFADHALI SAMBAZA UJUMBE HUU KWA WENGINE
 
na ukitoka mkoani kama hujashuka stop over kimara utaiona kupitia madirishani hawaruhusiwi kushusha abiria kimara mwisho kwa mabus ya mkoani
 
hv kona za pale nyuma ya kituo cha mafuta,bus zitaweza? Na wamei consider vp risk ya soko kuvamiwa na mabasi? kwanin lakn tz? Dah
 
pale nyuma ya kituo cha mafuta ile road ni nyembamba mno kwa mabasi
 
Hii nchi ina wendawazimu wengi! Wahamishe kituo hapo Ubungo wafanye taratibu zingine. Hii nchi ina mazingaombwe kha!
 
Tatizo letu kuu ni kutokuwa na uwezo wa kufanya long-term plan na mwisho wake ndio huu wa kutafuta pa kutokea baada ya mambo kupandiana, eeh Mungu tusaidie! Botha hakukosea alipozungumzia juu ya Mwafrika Vs mipango ya maendeleo!
kweli kabisa hakuna coordination kwenye mipango yetu. kwa mfano ndiyo maana kila siku tuko busy kuhamisha nguzo za umeme na mabomba ili kupanua barabara.
 
Sasa jamani kale kabarabara cha pale total hizo bus za mikoani zitaweza kweli kuzunguka?
Pili,vp kuhusu daladala za Sinza nazo? Pale tutegemee ajali nyingi sana na baada ya muda wahusika watabadili uelekeo wa mabus yawe yanaenda kugeuzia round about ya kigogo sambusa kupitia mburahati au la yakageuzie bondeni hotel "kwa macheni"
 
Yawe yanaishia mbezi

na ndio haya aliyosema Meya wa jiji kuwa ni makosa wamefanya kuvunja Ubungo kabla ya kujenga kituo cha mikoani mbezi kama walivyoapanga awali.

huu ni usumbufu kwa watumiaji wa barabara wote, yaani magari yanayoingia ubungo maji waende U-TURN Kibo!!!!!!!!!!!!.

Walipojenga barabara na kuweka zile U-TURN walitegmea nini, au ramani zipo vichwani mwa watu fulani badala ya kwenye makaratasi ili wasome na kuzielewa???

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
hii kitu sijui tumeiga wapi,,,,kwhiyo kwa kuzungusha watu hivo ndo tunapunguza foleni.??
 
Ujanja ni kwenda mbezi na kupanda magari madogo yanayoenda mikoani ili kuepuka usumbufu
 
TANGAZO KWA UMMA

Kuanzia Tarehe 08/04/2016 Siku ya Ijumaa Mabasi ya Mikoani yanayotoka ndani ya Kituo chetu cha Ubungo Yataanza kutumia Mzunguuko uliyosanifiwa wa Shekilango kwa kuzunguuka nyuma ya Kituo cha Mafuta cha Total (Nyuma ya Soko la shekilango) wakati wa kuanza safari zao za Mikoani.

Eneo lililokuwa limeachwa wazi kwa muda lililokuwa linayapitisha Mabasi kwenye barabara za BRT litafungwa rasmi ili kuwezesha Mabasi ya DART ambayo yameanza mazoezi kutokuwa na muingiliano na chombo kingine cha Usafiri kwenye barabara hizo. Uwazi utakaofungwa ni ule uliopo mkabala na Geti la kutokea na ule wa geti la Kuingilia. Aidha eneo la wazi kwenye Kituo cha DART Ubungo maji ambalo lilikuwa linatumiwa na Watumishi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Kuingia kwenye Jengo hilo Utafungwa pia.

Waliokuwa wakitumia uwazi huo wanashauriwa kutumia Usanifu wa mzunguuko ulioko eneo la Kimara Kibo (Rombo) kufanya tendo la kubadili uelekeo (Turning)

TAFADHALI SAMBAZA UJUMBE HUU KWA WENGINE
KUMBE WENYEWE MKOOO.......? HILO ENEO LA UBUNGO MBONA HALIKIDHI MAHITAJI.......? KUKOKUKO KAMA HALINA MWENYEWE ZAIDI NI WIZI WA MCHANA KWA KUTOZWA USHURU USIOJULIKANA UNABORESHA NINI HAPO, HAKUNA MABANDA YA KUJIKINGA NA MVUA WALA JUA. HAKUNA VIBAO VINAVYOELEKEZA WALA NINI, FUNGENI ENEO HILO HALILINGANI NA HADHI YA JIJI LA DSM. HIVI MGENI TOKA NJE ANAPOSHUKA HAPO NA AKAKUMBANA NA MAZINGIRA MABOVU KAMA HAYO MNATOA PICHA GANI.....?
 
Back
Top Bottom