Mabasi yale aina ya Icarus

Wakulu naona sisi ni wepesi wa kusahau, sasa watoto wa leo tutawaambiaje hadithi za uhakika?

Nakumbuka nauli kutoka Ubungo hadi Posta ya zamani kati ya 1989 na 1983 ilikuwa kati ya sumni yaani senti hamsini na shilingi moja.

Halafu baada ya 1983 nauli ikaanza kupanda kwa kasi hasa baada ya effects za Vita kuzidi kuumiza na hata Sokoine alipofariki mambo yakaanza kubadilika ghafla sana.

Pia wakati huko soda ilikuwa ni shilingi nne na ikapanda hadi shilingi sita mwaka 1984 mkate mmoja ulikuwa pia shilingi sita.

Mkebe na rula zake pale TANZANIA ELIMU SUPPLIES mtaa wa Makunganya (kama nakumbuka uzuri) duka pekee la vifaa vya elimu kwa wakti huo ikigharimu shilingi kari ya 10 au ishirini.


F3575.jpg
Shilingi kumi ya wakti huo

F1734.jpg


Shilingi ishirini ya wakti huo

Wakti ule ukiwa na noti ya shilingi 10 au 20 basi wewe ni tajiri sana, hasa kuweza kutanua na ice cream za "SNOW Cream" maana ilikuwa na uwezo wa kukuweka hata kwa wiki mbili.
 
Nyakipambo,

Mimi nadiriki mkusema kuwa, asiyejua anakokwenda, hata akipotea hawezi kujua kuwa amepotea.

Hii inamaanisha kuwa kuwa kupotea anaweza, isipokuwa kujua kuwa amepotea ndiyo hawezi, mpaka aambiwe kuwa amepotea, au apate vielelezo vya kumfanya ajue kuwa amepotea.

Nilikuwa najaribu kuangalia signature yako inayosema " ASIYEJUA ANAKOKWENDA HAWEZI KUPOTEA".

Hata hivyo nimeipenda sana.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom