Mabasi yaendayo kasi hayooo...!!!

KAMPUNI ya Bia Tanzania kupitia Bia ya Kilimanjaro Premium Lager hatimaye inatarajia kukabidhi mabasi mapya ya kisasa kwa timu za Simba na Yanga siku ya Ijumaa asubuhi.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema jana kuwa maandalizi yote yamekamilika na makabidhiano hayo yatafanyika katika viwanja vya ofisi za TBL Ilala.

“Zaidi ya wageni 100 wamealikwa kwenye hafla hii itakayofanyika Ijumaa hapa TBL na kati ya hawa wageni kutakuwa na baadhi ya mashabiki wa timu hizi mbili kwa hivyo tunatarajia makabidhiano ya aina yake,” alisema Kavishe.

Kwa mujibu wa ratiba, baada ya makabidhiano, kila timu itaondoka na basi lake na wachezaji na mashabiki na kupita katika matawi yao kwa msafara maalumu utakaoambatana na burudani mbalimbali huku mashabiki wa timu hizi wakitarajiwa kuyapokea mabasi hayo na kuwashangilia wachezaji wakipita katika matawi.

Hivi timu zingine hazihitaji hayo mabasi? kwa nini Simba na Yanga tu?
 
Haya mabasi yametolewa na wadhamini wa ligi nayo yalitangazwa kuwa watapewa timu zinAzoshiriki ligi. Ulikuwa na ulazima gani kuweka uzi huu??? Mod tunaomba hawa watu hawana shughuli mzuie uongo kama huu aende kwenye maandamano bana!!

eeeeeeh hahahahaaaaaa...!!
Duh una hasira mpaka sisimizi wanaruka!!
Vipi wewe ni askari unataka kuja kunilipua na bomu kwenye maandamano...!!!!
 
Yanga ina undugu na CCM kupitia vyama vilivyoitangulia kama TANU n.k. Enzi za mkoloni ili kuzuia watu wasijipange kudai uhuru ilikuwa hairuhusiwi kukusanyika bila ruksa, ikabidi ianzishwe timu ya mpira(Yanga) kama mbinu ya kukusanyika. Simba ilikuwa ina damu ya wakoloni ikiitwa sunderland.
Nashukuru kwa taarifa lakini mbona kama naona tofauti, Yanga ndiyo koloni la Manji anaifanya atakavyo, hata kumsajili Twite hakumshirikisha kocha, mwaka juzi akaiingiza Yanga hiyo hiyo kwenye balaa la kumsajili Keneth Asamoah asiye na tija wakamfukuza baadaye.

Mimi naona Simba (Mnyama) ndiyo inayopaswa kuitwa timu huru, inayomilikiwa na watanzania wenyewe bhana...
 
Hii ndo taabu ya watu kukimbilia kuanzisha thread wakiwa hawana taarifa kamili. Acheni kudanganya!
 
huo ni uomgo,and u shud be ashamed of yourself,hayo mabasi yamenunuliwa na mdhamini wa Simba sc na Young Africans(bia ya Kilimanjaro) kwa ajili ya simba na yanga.................

Hahaha aaaa....!!
Umekasirika....Pasuka basi....!!
 
Mtibwa 3 yanga hawajapata kitu.....Simba tano yanga hawajapata kitu.....basi lao liko nyuma la simba mbele kama kawa
 
Haya si ni yale ya mchina? Model hii wala siyo yale yanayosemwa kuwa ni mabasi ya kasi, hili lina uwezo wa kubeba abiria 120? Acha uzushi wewe!!!!
 
nakumbuka ule wimbo unaosema."bibi mbeleee bwana nyuma":bump2:
 
kukasirika sidhan kama nimekasirika..........lakn a real gentleman/lady hawez kuwa bold kiasi hiki kwa kusema uongo,just use wisely your precious time sir!

Inaelekea huwa hucheki wala hutaniani na mmeo/mkeo , gf/bf wako .........!!!
Hahahahaha..........!!!
Sasa kama umeumia si kamuone dakitari....:yawn:
 
Haya si ni yale ya mchina? Model hii wala siyo yale yanayosemwa kuwa ni mabasi ya kasi, hili lina uwezo wa kubeba abiria 120? Acha uzushi wewe!!!!

Vipi huwa yanaenda speed ya 20 km/h ndiyo speed ya mwisho .......!!!
 
Siyo hayo wewe, acha kudanganya watu!!! Mabasi ni haya hapa bwana!!!
 

Attachments

  • basi liendalo kasi.jpg
    basi liendalo kasi.jpg
    47.1 KB · Views: 31
Kale weekend yako bhana wacha niendelee kucheka na wengine.....!!
Mimi siyo mshabiki wa Simba wala Yanga.

nakutatakia vicheko vyema sana Kimbweka,pia nashukuru kwa taarifa yako kuhusu kutokuwa mshabiki wa Simba wala Yanga ,nakuhakikishia taarifa yako nimepokea,,,,,
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom