Mabasi ya Mikoani na Bongo Fleva

Mel James

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2015
Posts
367
Reaction score
299
Habari ya jion wakuu! Poleni na miangaiko ya leo. Nimeona niaandike habari hii maana binafsi ni mpenzi wa safari sana hasa wikiend uwa napendelea kusafiri. Mabasi mengi ya mikoan wanapendelea sana kuweka hii miziki ya bongo flavior sijui fleva.

Kwa upande wangu sikatai miziki isiwekwe hasa hii ya nyumbani lakini nawaomba sana wenye mabasi kuwa makini. Bongo fleva nyingi wanaimba matusi tena makubwa na hata uchezaji mwingine kwa kweli sio vizuri kuangalia mbele ya wazazi au watoto. Kwenye mabasi yenu watu wanasafiri na watoto wao wengine wazazi wao.

Unaweza kukaa kwenye siti na mzee mtu mzima kama mzazi wako ila unaona aibu hata kuangalia nyimbo mnazoweka. Mamlaka husika za usafiri tunaomba muingilie kati hili swala. Angalau wekeni miziki basi yenye staha kidogo hata kama wanaimba mapenzi ila wametofautiana level ya maneno hata video zao.

Wenye mabasi pia kuweni waungwana hasa makonda na madereva wekeni nyimbo ambazo hata nyie mnaweza kuangalia na watoto wenu au wazazi wenu nyumbani. Asanteni.
 
Mabasi mengi wanaajiri makonda mbumbumbu
Ila kuna mabasi makondakta wanajielewa playlist ya muziki Hadi unasinzia
 
[emoji849][emoji849][emoji849]
 
Kwenye basi huwezi kumridhisha kila mtu, bora wapige hiyo hiyo.
Niliona basi la ABC wana ubunifu wa aina yake, wana ABC TV inaonesha vipindi mbalimbali ambavyo mtu yeyote anaangalia.
 
Ngoja upande ya kwenda Ar na moshi uwekewe nyimbo za kimasai. Utakoma
 
Kuna bus ilo kila safari play list ni ile ile.hadi nime badili gari ina kera
 
Asavali wangekua wanaeka miziki ya kijaluo tu, haya maneno mingi ingekua imejam..😎😎
 
Mimi ndo ninadhani nimechoka kabisa na zile screen na speaker kwa ujumla. Ninatamani mchina asiziweke. Huwa ninaona kelele tu.

Kuna baadhi ya nchi mchina anaweka hizo burdani, lakini, hazifunguliwi kwa wote kiujumla kama hapa kwetu. Kuna earphones unachomeka kwa juu, mle kwenye kibeba mabegi ya ndani, mnamokaa vitundu vya kiyoyozi. Basi ukitaka unavaa unasikiliza midundo mliowekewa.

Angalizo
Dunia imebadilika sana aisee. Ukiwa kwenye basi , unaweza kudhani wenzako wanakereka kama wewe. Cha kushangaza kuna watu, tena adults wanashabikia kweli hiyo miziki na zile movie za kinigeria na zile zilizotafsiriwa kwa Kiswahili. Loh! Zile movie zikianza ndo balaa, sauti ya juu na mtafsiri ndo anapayuka kinoma. Yani hata una gazeti huwezi kusoma.

Siku hizi wengi tunamiliki simu, wasiweke hayo mambo. Nikitaka mziki ninasikiliza kwa simu yangu kupitia ear/headphones.
 
Asante mkuu ni kweli tunatofautiana nilishangaa hata kuona abiria wengi tu wamesimama na wengine wamekalia ndoo kama tupo enzi za kina leyland wakiona trafik wanaambiwa kaeni chini nao wanakaa kwenye mizani sogeeni nyuma na wanarudi kama wanasafiri bure.
 
Nadhn mmiliki han kosa ..dereva na kondakita ndio tatizo wanaenda kudownlod ngoma csizo na maadili ..wanaboa mbay duh bm Kochi wanaongoza maderev hawana aibu Ni majingambaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…