Umuhirindahu
JF-Expert Member
- Feb 2, 2014
- 349
- 170
Wana JF naomba kuuliza, ili basi la abiria likidhi vigezo vya kuitwa "luxury" inatakiwa liweje?nauliza kwakuwa jana nilisafiri kwa basi kutoka Arusha kuja Dsm kwa basi linalojinadi ni luxury,ndani lina "seat-two by two" tatizo ni mvua ilipoanza kunyesha,tulilowa njia nzima,gari halina mziki wala nini,TV zipo za kichovu na hazikuwashwa safari yote,nauli tuliyolipishwa ni ya Luxur,mdada ambaye ni konda/mhudumu majibu yake ni ya nyodo mwanzo hadi mwisho wa safari,jina la basi linaanzia D...........s!!!!
Dar Express si useme tu
Luxury Buses zilikufa na SCANDINAVIAN EXPRESS ,Now days hakuna tena Luxury Buses Bali tuna Two setter buses zilizo batizwa jina la luxury
This was a really luxury bus
Usafiri wa Dar-Mbeya-Dar kuna Ndenjela Jet...kuanzia makonda wao wa kike na madereva utafikiri wamepitia kozi za huduma kwa wateja...Huwezi juta kutumia usafiri wao...kwao mteja ni mfalme, wanamheshimu, wanamjali na kumsikiliza...
Scandinavia it was a luxurious thing from unapo nunua tiketi..aina ya tickets. Passengers lounge..kila kitu ulikuwa classic.... Bus zako zilikuwa ni luxury za sina 3 Marcopolo Andare ulikuwa ya chini na Parradisso was the most luxurious with Frige.coffee maker..toilet..full AC na kwa like la Dar-Nairobi.ilikuwa ukifika Kibaha wapatiwa breakfast ndani ya bus,ukifika Chalinze pili,biscuits na soda.tena zikiwa na nembo ya Scandinavia.. Baada ya kula korogwe. .wapewa pili Maji soda na napkins za Scandinavia... Hata km mko watano kwa bus halipakii njiani na mtaawachiwa AC to Nrb..Those were luxurious buses si sasa!!!!!!