Mimi ni mkazi wa mikoa ya kusini lakini ktk pita pita zangu nikapata safari ya kwenda Mwanza,nakumbuka tumetoka Ubungo dereva akiwa na mwendo wa kistaarabu sana.
Lakini tulipo anza kuicha Dar nikagundua kumbe jamaa alikuwa anahofia traffic tu mara akaanza kuweka gia za ajabu mwendo wa kasi usiopimika mpaka ikabidi nitafute mkanda upo wapi ndo nikagundua magari ya huko hayana utamaduni wa kuhimiza watu wavae mikanda,kwa kuhofia usalama wangu ikabidi nitafute kiti chenye mkanda lakini nikakuta abiria wenzangu wakanidharau sana kwa kitendo changu hicho.
Hata hivyo sikujali sana nikaamua kuvaa na nakutulia,sijakaa sawa tukawa tumefika Singida kutokana na dereva "kufukia matuta" mara kuna jamaa jirani yangu akalia kwa sauti kuu "mamaa" kumbe tayari kagonga kule juu sehemu ya kuwekea mizigo midogo midogo na kupasuka kichwa na damu nyingi zikamvuja sana!
Sikutaka kuongea kitu chochote ila kumsaidia jamaa apate nafuu,kuanzia hapo jamaa wakawa wapole baada ya abiria kuwapigia kelele nyingi!Naomba polisi watatue hali hii