Mabasi na matumizi mabaya ya Air Cinditioner

Bado niko na haya mabasi yetu. Nafikiri wahudumu/madereva/kondakta wa mabasi makubwa yenye AC kuna kitu hawaelewi. Kazi ya AC au air conditioner sio kuleta BARIDI bali ni ku regulate hali ya hewa ili iwe ya kawaida ambayo watu wote wataishi kwa raha, sio baridi wala sio joto. Ndio maana kitufe cha AC kina settings tofauti kuanzia ndogo hadi kubwa.

Sasa kuna baadhi ya mabasi huwa sijui wanaona ni sifa kufungulia AC mpaka mwisho. Yaani utakuta kwenye basi kuna baridi utafikiri upo ndani ya deep freezer! Abiria unakuta wamejikunyata humo ndani kama vifaranga vya kuku huku wengine wakilazimika kuchomoa masweta, mitandio au migolole. Wengine wanasafiri na watoto au wagonjwa basi tabu tupu.

Mbaya zaidi unakuta basi linatokea sehemu yenye joto mfano dar kwenda arusha lakini AC iko pale pale -mwanzo mwisho! Wahusika badilikeni acheni ushamba.
Mimi sasa ndio huwa napenda hivyo ,maana wengine sisi ni Mr.mijasho!
 
Kwani ukiisha panda Bus lenye full Ac na midomo mna zuiwa kuongea........si una waambia wapunguze.
Ajabu jingine hili ushindwe kuwalalamikia wahusika hapo kwenye Bus uje kulalamika JF.
 
Unawaita washamba wakati hujui umuhimu WA baridui kwenye gari.baridi inasaidia kupunguza kuchoka na kuleta usingizi.ni sehemu ya usalama barabarani.jaribu kutembea nchi za ulaya na America uone matumizi ya baridi.ukipanda mabasi ya huko hakuna kuongea Kwa Sauti wala kupiga story na mtu. Ni Kimya to.ukileta za kibongo unashuswa hapohapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ahahahaha, kwahiyo ukilazimisha kupiga story kama bongo wanakushusha kweli!?
 
Kabla ya safari wanatangaza utaratibu utakaotumika ndani ya basi ikiwa pamoja na kuongea na simu lazima utumie headphone na mambo mengine, so kila mtu anakuwa na time yake
 
Aisee basi lenye A/C to the max. ndio mwake mwake.
 
Bado niko na haya mabasi yetu. Nafikiri wahudumu/madereva/kondakta wa mabasi makubwa yenye AC kuna kitu hawaelewi. Kazi ya AC au air conditioner sio kuleta BARIDI bali ni ku regulate hali ya hewa ili iwe ya kawaida ambayo watu wote wataishi kwa raha, sio baridi wala sio joto. Ndio maana kitufe cha AC kina settings tofauti kuanzia ndogo hadi kubwa.

Sasa kuna baadhi ya mabasi huwa sijui wanaona ni sifa kufungulia AC mpaka mwisho. Yaani utakuta kwenye basi kuna baridi utafikiri upo ndani ya deep freezer! Abiria unakuta wamejikunyata humo ndani kama vifaranga vya kuku huku wengine wakilazimika kuchomoa masweta, mitandio au migolole. Wengine wanasafiri na watoto au wagonjwa basi tabu tupu.

Mbaya zaidi unakuta basi linatokea sehemu yenye joto mfano dar kwenda arusha lakini AC iko pale pale -mwanzo mwisho! Wahusika badilikeni acheni ushamba.
Juu ya kichwa chako chini ya sehemu ya vifurushi kuna kitufe cha kupunguza au kuongeza baridi sehemu yako, hata hivyo kuna baadhi ya abiria wakiingia tu ndani ya basi hufungua dirisha ili watoe nje vichwa. Wewe ukienda Mbeya au Njombe utakufa sijui barabara ni utamwambia Mungu apunguze baridi?
 
Ukitazama kwa juu yako ya siti uliyokaa kuna air ventilation uwe unafunga kama hauhitaji huo ubarid.

Sent using Jamii Forums mobile app
hata akifunga baridi itarudi kupia majirani zake, gari ni moja tu na ni behewa moja hivyo baridi ndani ya gari lote ni sawa,. atakachokwepa ni upepo kumpuliza
 
Nakuunga mkono, mm juzi nilipanda bus toka singida mpaka dar ni shiida kama tupo kwenye theluji? Halafu wahusika tunawaeleza ndo kwanza wakaongeza mpaka mwisho , sasa mm kila nusu saa kojo likawa linabana tuuuu[emoji849]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado niko na haya mabasi yetu. Nafikiri wahudumu/madereva/kondakta wa mabasi makubwa yenye AC kuna kitu hawaelewi. Kazi ya AC au air conditioner sio kuleta BARIDI bali ni ku regulate hali ya hewa ili iwe ya kawaida ambayo watu wote wataishi kwa raha, sio baridi wala sio joto. Ndio maana kitufe cha AC kina settings tofauti kuanzia ndogo hadi kubwa.

Sasa kuna baadhi ya mabasi huwa sijui wanaona ni sifa kufungulia AC mpaka mwisho. Yaani utakuta kwenye basi kuna baridi utafikiri upo ndani ya deep freezer! Abiria unakuta wamejikunyata humo ndani kama vifaranga vya kuku huku wengine wakilazimika kuchomoa masweta, mitandio au migolole. Wengine wanasafiri na watoto au wagonjwa basi tabu tupu.

Mbaya zaidi unakuta basi linatokea sehemu yenye joto mfano dar kwenda arusha lakini AC iko pale pale -mwanzo mwisho! Wahusika badilikeni acheni ushamba.
Siyo kila AC ni Air conditioner, zingine ni air cooler

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mi sipendagi zenye miziki/ TV
utakuta wameweka bongo muv ya kingwendu na bambo sauti mpaka mwisho, wkat mi nataka niskize nyimbo za ed sheran na passenger
 
Mkuu unatumia kinywaji gani nikununulie? Wahusika wa mabasi wabadilike katika hili jamani, unasafiri saa 12 asubuhi, AC kwenye basi kama upo kwenye freezer! Ni bora wakafahamu matumizi sahihi ya AC, hata ukifunga air ventilation kwenye siti yako kama basi limeshajaa baridi haipunguzi chochote.
Naunga mkono hoja yako na ya mtoa mada. Kuna siku nilijikunyata kama kifaranga aisee.
 
Back
Top Bottom