TheChoji
JF-Expert Member
- Apr 14, 2009
- 4,973
- 15,305
Bado niko na haya mabasi yetu. Nafikiri wahudumu/madereva/kondakta wa mabasi makubwa yenye AC kuna kitu hawaelewi. Kazi ya AC au air conditioner sio kuleta BARIDI bali ni ku regulate hali ya hewa ili iwe ya kawaida ambayo watu wote wataishi kwa raha, sio baridi wala sio joto. Ndio maana kitufe cha AC kina settings tofauti kuanzia ndogo hadi kubwa.
Sasa kuna baadhi ya mabasi huwa sijui wanaona ni sifa kufungulia AC mpaka mwisho. Yaani utakuta kwenye basi kuna baridi utafikiri upo ndani ya deep freezer! Abiria unakuta wamejikunyata humo ndani kama vifaranga vya kuku huku wengine wakilazimika kuchomoa masweta, mitandio au migolole. Wengine wanasafiri na watoto au wagonjwa basi tabu tupu.
Mbaya zaidi unakuta basi linatokea sehemu yenye joto mfano dar kwenda arusha lakini AC iko pale pale -mwanzo mwisho! Wahusika badilikeni acheni ushamba.