Mabasi Kuruhusiwa Kusafiri Usiku?

Mabasi Kuruhusiwa Kusafiri Usiku?

Ngoja tulimalize hili la Route ya Tegeta Escrow - Mikoani kwanza....
 
Kiuchumi:
Kwa mfano unatoka iringa jioni unafika dar usubuhi
unafunga mzigo mchana kutwa,jioni unakwea basini.
Mapedekezo
dar ira
dar moro
dar tan
dar dom
dar ms/r chug
(kwa usiku ni salama zaidi ya mchana)
ok?
Mwaka 1993 wakati serikali inatangaza rasmi magari ya safiri mchana baada ya basi la Yarabi Salama kutoka Dodoma kwenda Dar kupata ajali, wengi walisema mchana ni salama kuliko usiku, kama ni mchana tu wanakimbia namna hiyo pamoja na torch zipo, je usiku si itakuwa balaa.

Kibiashara kama ulivyoainisha juu, usiku ni bora zaidi kuliko mchana lakini kwa safari za kijamii, mchana ni bora kuliko usiku kwa kuwa akifika huko anakokwenda kama ni safari ya Mwanza to Dar au Mbeya to Arusha anapata muda mzuri wa kupumzika usiku alafu asubuhi anaendeleza mishemishe zake lakini kwa safari za Iringa - Dar au Iringa - Dom au Dom - Dar hizo iwe usiku au mchana yote sawa tu
 
Kiuchumi:
Kwa mfano unatoka iringa jioni unafika dar usubuhi
unafunga mzigo mchana kutwa,jioni unakwea basini.
Mapedekezo
dar ira
dar moro
dar tan
dar dom
dar ms/r chug
(kwa usiku ni salama zaidi ya mchana)
ok?

Naomba kuongezea, Dsm - Pwani (Kibaha, Bagamoyo, Kisarawe)
 
Hapo sawa. Kama ni ajali mbona hata mchana zipo wadau. Usiku safi sana. Na ss tusafiri usiku cyo wasafiri wa ungo tu.
 
SAFI ! mfano safari ya DAR -SINGIDA ni masaa 10-11 ,kuna sababu gani ya magri yote kuondoka saa 12alfajiri! magri mengine yangeondoka saa 7-8 yanafika saa sita ! Hata kama ni mwanza wanapumzika masaa 4 ,saa 1030 yanaondoka kwenda Mwanza! saa 3 ,Mwanza
Hii itakuwa safi sana, kwani miaka ya nyuma.mbona ilikuwa hivo?
Kwa upande wa usalama naamini watakuwa wamefanya utafiti na yawezekana si mikoa yote mf. Dar - Moro mpaka Dodoma hakuna shida sana, au Dar - Arusha hapo ni mfano tu but kuna njia.zingine ambazo asilimia kubwa miji na vijiji vipo karibu karibu so suala la usalama upande wa ujambazi linaweza kuwa tofauti na kama kule bukoba kutokea kahama kwenye lile poli kubwa sana na ambalo ukipita mchana unaweza kudhani ni usiku, pia magari kusafiri kwa ukaribu karibu inaweza kusaidia kwa upande huo.
Lakini kwa upande wa barabara sisi tz tuna barabara (long way) nzuri kuliko jirani zetu kenya lakini wao ambao hata suala la ujambazi kwa kuteka mabasi lipo juu bado wanasafiri usiku na mie napenda sana maana huwa kutoka mwanza kwenda NRB ukifika border sirare unaenda migori saa 2000hrs unapanda eridoret au acasia unaingia NRB saa 0600hrs unafanya mambo yako na jioni unafanya asif ulivokuja. Sasa sie hapa uwoga weeee, hata moro dar napo unasubiri kuche dooo…!!.
Ikianza hii itaongeza maendeleo na uchumi kukua japo wenye nyumba za wageni wajiandae kufanya biashara zingine AU ziwe za shortime -hahahaaaa.
 
kama mchana tu yanapata ajali namna hii hiyo usiku itakuaje?
 
Tatizo ni kwa Watz Hapa nipo kwenye Basi linaanza safari SAA 4:00 usiku kuelekea nchi Fulani EA
 
Ki uchumi 24hrs opareshen ni muhim sana.ki usalama kwa hapa kwetu ni majanga
 
Kama mchana tu ajali kibao watu wanapoteza viungo na umauti, usiku kwakwel tutakwisha kbs wa ruhusu xmass hii waone ars na mbeya watu wavyokufa
 
Hivi kama kweli serikali yetu imeshindwa kudhibiti vibaka wanaoteka magari, itaweza kutulinda au kushinda vita ikitokea nchi jirani imevamia. Au tutakubaliana na wavamizi vita ipigwe mchana tu. Tatizo ni mwanga/giza au ni raslimali watu?.
Kwanza naamini wezi na watekaji ni serikali wenyewe.
Kama la kwanza c sahihi basi viongozi wetu husafirisha mizigo haramu mf pembe za ndovu usiku.
Lakin watz tujue kuwa uchumi wetu unakuwa tu jua likiwa on. Likiwa off na uchumi wetu unakuwa off.
Mataifa mengine uchumi unakuwa 24hrs.
Intelligence hivi ipo na inafanya kazi?
Hivi gharama iko wapi? Kuweka jeshi na polis barabaran usafiri ukawepo 24 hrs au kusimamisha usafiri kwa masaa 6 hadi 12?
Sijui lini nchi hii itapata viongozi?
 
Sasa tutegemee maambukizi ya kasi ya gonjwa la ukimwi

Hebu hainisha huo ukimwi utaongezeka kivipi?
Ukiishia tu kama ulivoandika me bnafsi ctakuelewa mfano,
Me nasema ukimwi hautaongezeka kwa sababu watakao lala guest watakuwa wachache sana, km wafanyabiashara wengi wao watakuwa wanafika Dar alfajili wanafikia k/koo kukisanya mzigo jioni wapo ubungo kurudi mkoa, hapo guest atalala saa ngapi?
Tena hata hivo hii itasaidia kwa wale vilaza wanaopenda kudanganya wake zao kuwa ooh nimekosa usafiri ikanibidi nilale, utaulizwa mbona magari yanasafiei hata usiku…!!
 
Back
Top Bottom