Mabaraza ya Mitihani ya Afrika Mashariki yaungana

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
1,856
4,787
Mabaraza na Bodi za mitihani za nchi za Afrika mashariki kwa pamoja zimekubaliana kuanzishwa kwa umoja wa nchi za Afrika Mashariki katika tathmini ya elimu.

Kufuatia uamuzi huo Katibu Mkuu wa baraza la taifa la mitihani nchini Tanzania, Dkt. Charles Msonde ameteuliwa kuwa Rais wa Umoja huo.
Akizungumza na wanahabari wakati akitambulisha umoja huo, Dkt. Msonde amesema kuwa, umoja huo utasaidia kuongeza ufanisi kiutendaji katika nchi za Afrika mashariki.

"Kwa pamoja leo tutasaini Katiba yetu itakayoongoza umoja huu ambao mimi ndio Rais baada ya wao kunipendekeza na katibu wangu anatokea nchini Uganda huku mhasibu akiwa ni Mkenya", amesema Dkt. Msonde.

Kwa upande wake Katibu wa umoja huo kutoka nchini Uganda, Dan Odongo amesema kuwa umoja huo utakuza na kuimarisha nchi za Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kuzuia udanganyifu katika kipindi cha mitihani ya kitaifa.
 
Sasa hii itakuwaje wakati mifumo yetu ya elimu iko tofauti? Kenya kila kukicha wanabadilisha mifumo yao ya elimu, waliondo kidato cha sita, juzi juzi wamekuja na kingine, sasa ichi hizo tatu zitaelewanaje?
 
Nakumbuka walisema moja ya lengo lao ni kuwa washauri kitaalam kuhusu mitihani
 
Good news.
Hii ni kuelekea kuundwa kwa himaya moja ya elimu (one education area) itakayosaidia ufunguliwaji wa masoko ya ajira na uhuru wa watu kuvuka mipaka huko baadae.
Naunga mkono 100%
 
Sasa hii itakuwaje wakati mifumo yetu ya elimu iko tofauti? Kenya kila kukicha wanabadilisha mifumo yao ya elimu, waliondo kidato cha sita, juzi juzi wamekuja na kingine, sasa ichi hizo tatu zitaelewanaje?
Kuna process of harmonisation imeshaanza mda tu.
Lengo ni huko baadae tuwe na 'common education area'
Mtoto anaweza kusoma primary Tanzania, sekondari Uganda na chou Kenya bila Tatizo lolote!
 
Sasa hii itakuwaje wakati mifumo yetu ya elimu iko tofauti? Kenya kila kukicha wanabadilisha mifumo yao ya elimu, waliondo kidato cha sita, juzi juzi wamekuja na kingine, sasa ichi hizo tatu zitaelewanaje?
Kenya wanabadili kwakuwa wanaenda na wakati na wanajibu mahitaji ya wanafunzi na waalimu, inaweza ikasaidia tukaunda mfumo mmoja kwa ajili ya africa mashariki itakuwa vizuri kuboresha elimu.
 
Kama wanakwenda na wakati mbona kila siku madaraja yanavunjika?
 
Wangeanzia chini au mwanzo, utoaji wa elimu, na sio jinsi ya kutahini. Mifumo ya utoaji elimu ni tofauti, wanatoa ushauri gani juu ya mitihani kwa msingi huo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mabaraza na Bodi za mitihani za nchi za Afrika mashariki kwa pamoja zimekubaliana kuanzishwa kwa umoja wa nchi za Afrika Mashariki katika tathmini ya elimu.

Kufuatia uamuzi huo Katibu Mkuu wa baraza la taifa la mitihani nchini Tanzania, Dkt. Charles Msonde ameteuliwa kuwa Rais wa Umoja huo.
Akizungumza na wanahabari wakati akitambulisha umoja huo, Dkt. Msonde amesema kuwa, umoja huo utasaidia kuongeza ufanisi kiutendaji katika nchi za Afrika mashariki.

"Kwa pamoja leo tutasaini Katiba yetu itakayoongoza umoja huu ambao mimi ndio Rais baada ya wao kunipendekeza na katibu wangu anatokea nchini Uganda huku mhasibu akiwa ni Mkenya", amesema Dkt. Msonde.

Kwa upande wake Katibu wa umoja huo kutoka nchini Uganda, Dan Odongo amesema kuwa umoja huo utakuza na kuimarisha nchi za Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kuzuia udanganyifu katika kipindi cha mitihani ya kitaifa.

Huyo Katibu wa NECTA anadai yeye ndiyo Rais. Haha! Ngoja mtu mmoja amlie timing tu....
 
Back
Top Bottom