Mabalozi wa Nyumba Kumi Kuwa Makada wa CCM Tu ?

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,373
6,084
Naona kuna utaratibu mpya umeanza kwa mtu akitaka kuwa balozi wa nyumba kumi lazima awe kada wa CCM na awe na wanachama hai wa CCM wasiopungua 50.
Je kwa wale ambao si wana CCM ina maana hawatakuwa na mabalozi wa nyumba kumi ? Viongozi wa vyama vya upinzani inabidii muangalie kwa makini suala hili ikiwezekana kuanza kuweka mabalozi wa UKAWA. Mabalozi ni muhimu kwa uhai wa vyama mitaani haswa inapokuja wakati wa uandikishaji wa wapiga kura.
 
Sehemu ambapo mwenyekiti ni chadema, mbona huwa wapo mabalozi au vitongoji wa CDM mkuu...
Mbali yakuwa mwenyekiti ni CCM ina maana wanachama wa chadema hawawezi kuwa na balozi wao haswa kwenye masuala ya chama ?
 
Mi nazani balozi anashindanishwa yani cdm ccm cuf wananchi wanamchagua balozi anayewafaa hizo unazotilia wasiwasi wewe ni sifa za mgombea wa balozi wa ccm
 
Hata hueleweki mkuu kwahiyo unalazimisha hao mabalozi wawe wa chadema au unataka nini mkuu, maana hizo nafasi ni za kuchaguliwa na sio kuteuliwa.
 
Mi nazani balozi anashindanishwa yani cdm ccm cuf wananchi wanamchagua balozi anayewafaa hizo unazotilia wasiwasi wewe ni sifa za mgombea wa balozi wa ccm
mbona kwasasa Tanzania nzima kuelekea uchaguzi wa CCM wanahakikisha kila mtaa wanapatikana mabalozi wa CCM
Naona kuna utaratibu mpya umeanza kwa mtu akitaka kuwa balozi wa nyumba kumi lazima awe kada wa CCM na awe na wanachama hai wa CCM wasiopungua 50.
Je kwa wale ambao si wana CCM ina maana hawatakuwa na mabalozi wa nyumba kumi ? Viongozi wa vyama vya upinzani inabidii muangalie kwa makini suala hili ikiwezekana kuanza kuweka mabalozi wa UKAWA. Mabalozi ni muhimu kwa uhai wa vyama mitaani haswa inapokuja wakati wa uandikishaji wa wapiga kura.
 
Hao ni wao ccm cdm hawawausu we nenda kwa m/kiti selikali mtaa au wajumbe wa s/mtaa
 
Hakuna cheo cha balozi katika muundo wa serikali za mitaa. Cheo cha chini mwisho ni mwenyekiti wa mtaa. Hio ya balozi ni ngazi za kichama hivyo ni lazima awe ccm sema tatizo ni kwamba wenyekiti wa mitaa wanapoingiza nafasi hio kama inatambulika rasmi ndani ya serikali kama ilivyokua miaka ya 90 mwanzoni kurudi nyuma
 
Naona kuna utaratibu mpya umeanza kwa mtu akitaka kuwa balozi wa nyumba kumi lazima awe kada wa CCM na awe na wanachama hai wa CCM wasiopungua 50.
Je kwa wale ambao si wana CCM ina maana hawatakuwa na mabalozi wa nyumba kumi ? Viongozi wa vyama vya upinzani inabidii muangalie kwa makini suala hili ikiwezekana kuanza kuweka mabalozi wa UKAWA. Mabalozi ni muhimu kwa uhai wa vyama mitaani haswa inapokuja wakati wa uandikishaji wa wapiga kura.
Ukawa ofisi hawana itakuwa hao mabalozi?
Chadema walishawahi kujaribu lakini wamefeli kwa sababu hawana miundo mbinu ya kiofisi kufanikisha mawasiliano.
Kwa mfano chadema wana jimbo na kanda,hawana mikoa na wilaya katika safu zao,inakuwa vigumu sana kufanya utekelezaji au maamuzi kwa kuwa taarifa zina ruka toka shinani hadi jimboni hapa kati wanarukwa watu wengi sana wanaojua mambo ya eneo husika kuliko huyo katibu wa jimbo husika
 
Hakuna cheo cha balozi katika muundo wa serikali za mitaa. Cheo cha chini mwisho ni mwenyekiti wa mtaa. Hio ya balozi ni ngazi za kichama hivyo ni lazima awe ccm sema tatizo ni kwamba wenyekiti wa mitaa wanapoingiza nafasi hio kama inatambulika rasmi ndani ya serikali kama ilivyokua miaka ya 90 mwanzoni kurudi nyuma
Kwanini ukiwa na matatizo Polisi unaaulizwa unapoishi balozi wako anaitwa nani
 
Ukawa ofisi hawana itakuwa hao mabalozi?
Chadema walishawahi kujaribu lakini wamefeli kwa sababu hawana miundo mbinu ya kiofisi kufanikisha mawasiliano.
Kwa mfano chadema wana jimbo na kanda,hawana mikoa na wilaya katika safu zao,inakuwa vigumu sana kufanya utekelezaji au maamuzi kwa kuwa taarifa zina ruka toka shinani hadi jimboni hapa kati wanarukwa watu wengi sana wanaojua mambo ya eneo husika kuliko huyo katibu wa jimbo husika
Kwa mtindo huu wa kutokuwa na structure ya chama toka ngazi ya chini maana yangu mabalozi itakuwa vigumu sana kushinda uchaguzi mkuu.
 
Wanachama wa upinzani wanaouwezo wa kuwa na mjumbe wao kwani kila mmoja anaitikadi yake. Tena hii ndo nzuri sana ktk jamii ili kujuana
 
Hawa walijulikana kijadi na baada ya kuingia vyama vingi inabudi wa kujulikana kwani wana mchango mkubwa ktk kuunganisha watu
 
Kwanini ukiwa na matatizo Polisi unaaulizwa unapoishi balozi wako anaitwa nani
Waulize hao polisi hilo swali au uone kama kuwekewa dhamana itakuja barua ya balozi au mwenyekiti wa mtaa
 
Back
Top Bottom