MABAGA FRESH

MABAGA FRESH

ukwaju_wa_ kitambo

Senior Member
Joined
Sep 15, 2024
Posts
155
Reaction score
182
KUTOKA DISABLED JAY RAPERS GROUP HADI KUJIITA " MABAGA FRESH"..

Katika ulimwengu ambao mara nyingi huhusisha mafanikio na ukamilifu wa kimwili na kiakili, ni muhimu kufahamu kuwa kuna watu wenye ulemavu ambao wameweza kuvuka changamoto hiyo na kutenda mambo makubwa ambayo yanaweza kuwa mfano wa kuigwa katika jamii inayowazunguka na hata dunia yote kwa ujumla..

Katika mahojiano haya na " chritoms mwingira a.k.a "dj snox" tunaenda kuieleza jamii ama kutoa elimu kwa watu mbalimbali wenye mitazamo hasi juu ya walemavu na kuwapa somo..

Kuna watu wengi tu maarufu wenye ulemavu kwenye jamii zetu ambao wamebadili mtizamo na matarajio ya jamii kwamba hawana uwezo , lakini pia wameacha alama isiyofutika katika nyanja zao husika.

Katika Mahojiano haya na chritoms mwingira a.k.a dj snoks tunawaangazia changamoto zao za ulemavu akiwa na Rafiki yake wa karibu ndugu jumanne omary a.k .a jb miaka 1990s ambapo waliweza kubadili changamoto zao na kusifanya kuwa sehemu ya fursa na hatimae hii leo wamepiga hatua kimaisha na hata kimuziki hadi kufikia mafanikio ya hali ya juu katika Nyanja zao. Hasa kupitia sanaa ya muziki ...

Naimani watu wengi mnalikumbuka kundi hili la "Mabaga fresh" kundi la muziki ambalo harakati zake zilianza miaka ya 1990s nadhani kipindi hiki cha miaka 1990s kwa hapa kwetu Tanzania 🇹🇿 , yalianzishwa makundi mengi sana ya muziki hasa kwenye upande wa muziki Aina ya Hip Hop..

Kundi la " Mabaga fresh" ni moja kati ya makundi yalioanzishwa miaka hiyo ya 1990 , kundi ambalo liliundwa na wasanii wawili (2)
Wasanii hao ni Chritoms mwingira a.k.a "dj snoks" na jumanne omary a.ka "jb".

Haya ni baadhi ya majibu ya dj snoks kuhusu historia yake kimuziki kipindi hicho akiwa na Rafiki yake jumanne omary a.k.a jb kwenye Crew yao ya " Mabaga fresh"

Dj snoks :mimi na mwezangu jumanne omary a.k.a jb " mkuu wa majaji " tulikutana shuleni kipindi tupo secondary " shule ya serikali "Yombo" jijini Dar es Salaam mwaka 1992 mimi dj snoks nilikuwa nimehitimu Elimu yangu ya msingi katika shule ya msingi Azania ..

Na wakati mimi Nafika pale Secondari nilimkuta mwezangu "Jb" mkuu wa majaji" ameshaanza kusoma .

Kwa vile mimi pale shuleni Secondari nilikuwa mjanja mjanja sana kwenye upande wa mambo ya burudani Burudani mwalimu wetu wa michezo akawa amenipa mimi Uongozi pale shuleni " nikawa " mwenyekiti" wa mambo ya Burudani na michezo pale shuleni..

Na mwezangu "jb" mkuu wa majaji alikuwa mzuri sana upande wa kuimba kuandika mashairi ikatokea tukawa marafiki kinoma pale shuleni..

Na sisi wakati tupo pale shuleni tulikuwa tufanya sanaa mbalimbali kila mtu kivyake kwa kifupi tulikuwa hatuna kundi mpaka tunamaliza ..

Ila tulipo hitimu elimu yetu mwaka 1994 , maana Ile shule enzi hizo ilikuwa ina toa Elimu ya ufundi kwaajili ya watu wenye ulemavu tu , ( special kwa walemavu elimu ya ufundi) na elimu ya Secondari kwa watu wa aina zote .

Kwa hiyo sisi tulipokuwa tumeenda pale kusoma Secondari ( Elimu ya Secondari) tukajikuta tumesoma pia na ufundi ili tuwe na ujunzi pale tutakapo hitimu elimu yetu pale " Yombo" jijini Dar es Salaam.

Mwezangu " jb" mkuu wa majaji alikuwa anasomea ufundi "seremala" carpentry" na mimi dj snoks nilisomea ufundi "welding " kwahiyo tulipo hitimu pale shuleni.

Mimi nikawa nimepata kazi katika kampuni linaitwa " Quality Group limited " kampuni la kina "Yusuph manji" enzi hizo kampuni hilo akiwa bado analimiki baba yake na yusuph manji..

Nilifanya kazi pale mwaka 1994, mpaka 1995 wakati uchunguzi wa vyama vingi unafanyika Hayati "Benjamini wiliam mkapa" akiwa amechukua form ya kugombea Urais kupitia chama cha mapinduzi ( Ccm) mimi nilikuwa katika kampuni la "Quality Group limited " ila upande wa ufundi ( Quality Gereji). Nilikuwa fundi nilikuwa nachukua contractor maana enzi hizo ulikuwa ukifika katika hiyo kampuni kama umetoka katika chuo cha Ufundi ( Veta) ulikuwa uajiriwi lakini unapewa tu contractor ( unafanya kazi kwa mkataba) ukimaliza kazi hapo hapo unapewa haki yako ( malipo) kutokana na Aina ya kazi ulioifanya na makubaliano yenu kwenye upande wa malipo ( fedha)..

Nakumbuka pia kipindi kile sisi tupo pale shuleni, ile shule pamoja na chuo kilikuwa kina wathamani na kanisa la katoriki na watu kutoka huko ughaibuni " watu kutoka taifa la Norway 🇳🇴 ( norland) sasa watu wa fani mbalimbali pale shuleni waliokuwa wanasomea ufundi waliwezeshwa na wathamini hao wawili (2) ( norland & kanisa katoriki ) kwa kupewa vifaa pale tu wanapo hitimu mafunzo yao ya ufundi pale chuoni...

Kwa mfano walisomea mambo ya "carpentry " walipewa vifaa lakini kwa sisi tuliosomea mambo ya " welding " kidogo akawa ni changamoto kupewa vifaa maana kwa kipindi vifaa vya welding vilikuwa vina ghalama kubwa lakini pia vilikuwa vichache kwa hiyo ilikuwa ni ngumu kupewa kitu chochote sisi tuliosomea ufundi wa "welding " tunapo hitimu pale chuoni..

Kipindi kile cha uchanguzi mimi nilikuwa nakaa kigongo maeneo ya kigamboni na jb mkuu wa majaji alikuwa anakaa mwembe Yanga maeneo ya Temeke..

Kipindi hicho mambo ya Hip hop yanachimbukia chimbukia huku muziki Aina ya Taarabu umepiga kasi .

Kwa hiyo Jb mkuu wa majaji aliporudi kwao na mimi nikarudi kwetu na ndicho kipindi makundi mbalimbali ya Hip hop yame chimbukia chimbukia ..

Makundi kama lwp " live with purpose " na Gwm " Gangster with Matatizo "

Mkuu wa majani (jb) akawa amenitafuta "Eeeh Bwana eeeh" kipindi hicho shuleni tulikuwa tunafanya mambo ya ushairi shairi nini..!!

Hata lilikuwa likitokea jambo lolote kuhusu sanaa hasa kwenye mambo ya ushairi sisi ndio tulikuwa tunapewa kipaumbele kuwakirisha shule kwenye upande wa mambo ya sanaa,

Jamaa yangu naomba tuunde Crew ( kundi) kipindi hicho tulipo kutana na jb mkuu wa majaji alikuja na jamaa yake tukawa tumeunda crew ya mtu tatu (3).

Huyu rafiki yake na jb mkuu wa majaji alikuwa ni mtu mfupi ( mbilikimo) ila baadae alikuja akazingua tukawa tumeachana nae ..

Kipindi hicho sisi tulikuwa tunajiita.. D stars jay Rapers Group" Yaani ilikuwa ina maanisha kundi letu zote ni la walemavu ( disabled JAY Rapers Group) .."

Huyu jamaa yetu mfupi alikuwa anaitwa "stacha cool " harafu mimi dj snoks "zungu la Unga" na jb mkuu wa majaji..

Ndio maana tukaweka kama hivi.

D - DISABLE
STAR - STACHA COOL ( MTU MFUPI)
ZU - ZUNGU LA UNGA ( DJ SNOKS)
JAY - JB ( MKUU WA MAJAJI)

Alipozingua mtu mfupi ( stacha cool) tukawa tumeachana na D stars 🌟 jay Rapers Group na kuamua kuunda Crew ya mabaga fresh..

Lakini mabaga fresh enzi hizo lilikuwa na maanake yake na kwenye miaka ile ya 1990s mtu mwenye ulemavu Dar es Salaam ukienda kwenye Duka la mtu yoyote kununua kitu na wewe ni mlemavu ( kwenye maduka ya wahindi) ukiingia mule na wewe ni mlemavu wale wamiliki wa maduka ambao ni wahindi walikuwa wanahisi sisi ni "omba omba" ( masikini).

Itaendelea..

MABAGA_FRESH
Jumanne Omary 'JB'
Chritoms Mwingira 'DJ SNOX'

Mtu mbili kama milioni mbili..

MABAGA FRESH, kuhusu ukaribu wao na Juma Nature?..

Ukizungumza na Sir Nature umuulize safari yake ya mafanikio kimuziki kamwe hawez wasahau hawa MABAGA FRESH kwani wao ndio waliomtoa 'SKONGA' na kumpa collaboration la kwanza.

Ukwaju wa kitambo
0767 542 202
images.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom