Mabadiliko yanaanza na sisi

Lighton

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
881
1,636
Ndugu wapendwa nawasalimu kwa jina la jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Huu ni mtazamo wangu...

Tofauti kati ya mataifa tajiri na mataifa masikini duniani siyo umri wa Taifa fulani. Ushahidi huu unadhihirishwa na mfano wa nchi kama India na Misri ambazo zina zaidi ya miaka 2000 na bado ni nchi masikini huku Canada,Newzealand na Australia ambazo kwa takribani miaka 150 iliyopita zilionekana ni nchi masikini sana lakini leo hii ni nchi zilizoendelea na ni nchi Tajiri Duniani.

Tofauti kati ya nchi tajiri na nchi masikini haihusiani hata kidogo na uwepo wa rasilimali zilizopo, Japan wana maeneo makubwa %80 ni milima ambayo siyo maalum kwaajili ya makazi,kilimo lakini ni nchi ya tatu yenye uchumi mkubwa Duniani.

Ukubwa wa uchumi wa nchi fulani unategemea uwepo wa viwanda vya kutosha,kuingiza malighafi kutoka katika nchi mbalimbali na kuexport bidhaa zilizotengenezwa nchi mbalimbali Duniani.

Switzerland hailimi cocoa lakini ni nchi inayotengeneza chocolate nzuri zaidi Duniani. Pamoja na kuwa na maeneo madogo kwaajili ya kufuga,kulisha mifugo na kufanya kilimo switzerland ni nchi inayoongoza kwa kufuga na kuvuna mazao kwa kipindi cha miezi minne tu kwa mwaka na bado ndo nchi inayoongoza kwa kutengeneza bidhaa bora kabisa za maziwa Duniani, ni nchi ndogo sana yenye mifumo imara ya kibenki na ya usalama Duniani.

Mfano mwingine ni Korea, haina mafuta lakini ina kiwanda kikubwa zaidi Duniani kwaajili ya kusafisha mafuta ya petroli na kuyasambaza Duniani kote. Ni nchi isiyokuwa na mtapo wa madini lakini ni nchi yenye kutengeneza meli kubwa Duniani. Haina madini ya copper lakini ni most electrically and electronically wired country.

Utendaji kazi wa watu wa mataifa yaliyoendelea hauhusishwi moja kwa moja na elimu ya watu wa nchi hiyo, wala sababu ya rangi ya watu wa nchi fulani haidhihirishi faida hiyo

Wahamiaji wengi kutoka katika nchi masikini walilazimishwa kuwa wazalishaji katika nchi za magharibi.

Sasa Tofauti ni jini?

Tofauti ni mitazamo ya watu,urekebishwaji wa mifumo ya elimu wa muda mrefu,utii,uwajibikaji na utamaduni.

Kama ukiorodhesha miongozo ya watu kutoka katika nchi tajiri na zilizoendelea Duniani utaona wengi wanazingatia kanuni zifutazo,

1. Tabia ya maadili kama kanuni muhimu.

2. Uwajibikaji.
3. Kuheshimu sheria na kanuni.
4. Heshima ya viongozi wa nchi kwa raia wake(demokrasia)
5. Kupenda kazi
6. Nguvu ya akiba na kuwekeza
7. Msukumo wa kuwa mzalishaji mali
8. Uadilifu
9. Na usahihi.

Katika nchi masikini ni wachache mnoo hufuata kanuni hizi muhimu katika maisha yao ya kila siku. Sisi siyo masikini kwasababu uhalisia ulitukatili.

Sisi ni masikini kwasababu tumekosa mitazamo,tumekosa msukumo wa kufuata na kufundishana kanuni za kufanya kazi ambazo jamii za nchi zilizoendelea zinajivunia.

Tupo katika dola hii kwasababu tunataka kutumia madhaifu ya wenzetu kwaajili ya maslahi binafsi.

Tupo katika dola hii kwasababu kuna wakati tunaona mambo yanaenda tofauti na tunasema "Acha iwe hivyohivyo kama ilivyo kwasababu ndivyo ilivyokuwa tokea awali.

Ni lini tutaibadilisha dola hii tuliyonayo kwa sasa kuwa kama dola zilizoendelea? Muda ni sasa. Wa kuibadilisha Tanzania ni mimi,wewe na yule.

Naomba kuwasilisha
 
Maoni so lazima yatoke kwa kiongozi mkuu,maono hata yako binafsi yanaweza kubafili fikra za watu na wakafanya hatua kubwa ya maendeleo na serikali ika ku support ma ikawa mfano wa kuigwa, mfano mtu Kama ruge,mo,dangote wakipatikana watu wa namna hiyo wakawa hawana ubinafsi wawepo hata 25 ktk taifa na bila ubinafsi kwnn taifa lisisonge mbelee, kiongozi nae no binadam,na kuwa kiongozi sio lazima uwe na maono,wapo watu wanapata fursa pasipo maono,so maono yako saidia jamii ipige hatua hata kwa ngazi ya familia
 
Hakika, tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
Ni kweli kabisa mkuu ndiyo maana nikasema mabadiliko yanaanza na sisi wenyewe, kila mmoja kwa nafasi yake. So utaona hapo hata viongozi wanahusika.
 
Maoni so lazima yatoke kwa kiongozi mkuu,maono hata yako binafsi yanaweza kubafili fikra za watu na wakafanya hatua kubwa ya maendeleo na serikali ika ku support ma ikawa mfano wa kuigwa, mfano mtu Kama ruge,mo,dangote wakipatikana watu wa namna hiyo wakawa hawana ubinafsi wawepo hata 25 ktk taifa na bila ubinafsi kwnn taifa lisisonge mbelee, kiongozi nae no binadam,na kuwa kiongozi sio lazima uwe na maono,wapo watu wanapata fursa pasipo maono,so maono yako saidia jamii ipige hatua hata kwa ngazi ya familia
Ni kweli mkuu mabadiliko yanaanza na sisi wenyewe, kama kichwa cha habari kilivyojieleza. Japo viongozi nao wanahesabika kama sisi wenyewe kwasababu ni wawakilishi wetu kwenye dola.
 
Back
Top Bottom