Imekuwa ni kasumba ni kasumba kwa watanzania baada ya kuona watanzania hawaridhiki na mwenendo wa mambo kila mtu anakuja na kuwaahidi watanzania mabadiliko.
wanasiasa hawa wamekuwa kila mmoja anatafuta fikra zake au itikadi ya chama chake na kuamka kuyabeba kwa bendera ya kutaleta mabadailiko.
tumekwisha pitia hatua nyingi ni wakati sasa kutafakari na kusema hakuna mtu mmoja anaweza kuleta mabadiliko katika nchi hii bali watanzania wote kushirikiana ndio inaweza kuleta mabadiliko.
kwa mfumo wa utawala uliopo ni wazi kila kiongozi atakayekuja atalazimisha watanzania kutekeleza mitizamo yake, fikra zake hata kama watanzania hawa watakuwa wanaona vingine.
ili watanzania wote kushiriki katika mabadiliko ya nchi yao ni lazima kuwe na namna inayomwezesha mtanzania aliyepewa jitihada za kuongoza mabadiliko analeta mawazo ya ni kitu gani anataka kufanya na watanzania hawa wanakubaliana naye au wanamkosoa.
hili haliwezi kufanyika bila kuwa na mihimili mitatu iliyo huru na ikisimamiana.
kwa tanzania yetu bado mahakama na bunge ni kama taasisi ndani ya serikali, hakuna anayeweza kusimama kupinga au kukosoa jambo lolote linalofanywa na serikali kama halielekei uleta matokeo mazuri.
wabunge mmoja mmoja watakosoa sana lakini mahusiano yaliyopo baina ya bunge na serikali yanasababisha bunge kwa ujumla likae kimya.
mahakama kwa upande wake imo ndani ya serikali hivyo haionekani kama inaweza kupinga jambo zito lililoagizwa na serikali.
hoja kwa nchi yetu iwe ni kufanya mambo ambayo watanzania wanataka na sio kama viongozi wanavyodhani kuwa watanzania wanatakiwa kufanya wao wanavyotaka.
mfano mzuri tunaotaka katika nchi yetu ni kama kilichotokea marekani juzi, raisi akatoa amri na mahakama ikatengua. hayo ndiyo tunayoyataka kuwa kama baadhi ya mambo wanayotaka kufanya watawala watanzania kama hawariziki vipo vyombi vya kukosoa na hiyo ndiyo mantiki ya kutaka vyombo huru.
mfano : moja ya jambo ambalo linasemekana kukwamisha maendeleo ya nchi yetu ni hulka ya ufanyaji kazi.
watanzania wanatofautiana katika sababu zinazosababisha watanzania wasiwe wachapa kazi.
wapo wanaodhani watanzania watanzania ni wavivu, wapenda kukaa tu na kusubiri kupewa vitu vya bure, na hii ndiyo dhana iliyobebwa na utawala wa awamu ya tano kwa kuhamasisha na kulazimisha watu wafanye kazi.
wapo wanaopingana na dhana hii kuwa uvivu ni matokeo ya mambo mengi. wao wakiamini kuwa mfumo wa maisha wa sasa ulivyo kila mtu anasukumwa na mahitaji yake na familia yake kuhangaika kutafuta kipato. lakini mtu huyu anapokuwa haoni la kufanya atabaki kukaa tu hivyo kusema kukaa tu ni ukosefu wa ajira kwa namna moja na hili linaletwa na mambo mengi.
kwanza ni mifumo ya elimu.
hapa ina maana kuwa mifumo rasmi na isiyo rasmi ya elimu ni nguzo kubwa katika kujenga hulka na tabia za watu katika kazi. Wana jamii kama ukiwalea kwa elimu za kukaa tu kusubiri kupewa, wasipopata basi wajue eti hawakupangiwa na kama wamepangiwa watapata tu unategemea nini juu ya watu kuhangaika kutafuta maisha ukubwani? hivyo wapo wanaoamini mafundisho ya imani yanayoanza kwa watu wakiwa wadogo, wahubiri hawa wakiwaeleza wananchi hawa elimu zao hazina maana, mungu ndiye mtoaji wa kila kitu, hakuna anayeweza kupata chochote bila kuomba, watoto wanaambiwa mali hazigombaniwi bali mtu akae chini aombe.
matokeo yake ni masikini wanashinda kwenye nyumba za ibada wakiombewa eti ili waachane na umasikini na sio kushinda wakitafuta kazi, je tatizo liko wapi? utaondoaje umasikini kwa matajiri kuwa bize wakifany6a kazi na masikini wako bize wakiomba? utasikia huduma za maombi za kuleta utajiri zinaanzishwa na zinaendeshwa kisheria na wazi wazi. mtu akikwama katika shughuli zake haendi kukaa chini kutafakari kuna tatizo gani kupitia maarifa ya kiuzalishaji au kibiashara bali anakimbilia kwenye nyumba za maombi na waganga wa kienyeji akiamishwa kila kitu anachofanya kiko sahihi isipokuwa kuna mkono wa shetani.
unategemea nini kumuona yule tunayemkabidhi dhamana ya kubadili hulka za kufanya kazi kwa watanzania hawa au anayetaka kupewa fursa anaposhinda kwenye maombi au waganga eti kutafuta nafasi hiyo? unategemea nini unapomsikia huyu kila siku akiwaambia hawa wamuombee kuwa ndio njia ya kutimiza kile anachotakiwa kufanya?
lakini pia wapo anaoamini kabisa kuwa uvivu katika mfumo huu wa maisha yanayosukumwa na biasahara uvivu ni matokeo ya kukosa ajira. moja ya factor kubwa katika biashara ni mzunguko wa pesa. mzunguko wa pesa ukiwa mdogo ajira na ubora wa maisha ya watu unakuwa chini. hawa wanaenda mbali zaidi kwa kusema sio kwamba watu wa mijini wanafanya kazi sana kuliko watu wa mijini, yawezekana watu wa vijini wanafanya kazi zaidi lakini tofauti kubwa baina yao ni mzunguko wa pesa.
unategea nini unapoona yule anayejinasibu kutaka kubadilisha hulka ya watu ya kufanya kazi hatua anazozichukua zinaathiri mzunguko wa pesa unapungua kasi na atharizinaonekana wazi lakini yeye anasema wao ni kwa sababu ni wavivu. wahandisi katika taaluma zao huwa wanasema kama kuna kitu kinatoa huduma katika jamii lakini kikawa kibaya , unapotaka kukiondoa hiki kuweka kitu kizuri ni lazima kwanza utengeneze kitu cha mda cha watu kutumia wakati ukitengeneza kipya, kama ni jengo ni lazima ujue waliokuwa wakitumia jengo hilo watakwenda wapi kwa mda, kama ni barabara ni lazima ujue watumiaji watapita wapi kwa mda. taaluma zote zinatumia principle zilezile, sasa kama huko nyuma tulitengeneza njia haramu zilizotumika kuingiza fedha kwenye mizunguko ya kwenye jamii tulihitaji wataalamu hawa kutueleza kuwa tunapoziba fedha hizi biashara kwenye jamii hazitaathirika kwa maana tunawanyanganya fedha hizi haramu tunawapa fedha hizi halali hivyo mizunguko itakuwa salama. mfano kama watu walikuwa wanachukua posho zisizostahili wanatumia na kudunduliza kwa ajili ya kujenga nyumba basi tunafuta posho lakini tumeandaa mpango wa mikopo ya nyumba hivyo mtu atajenga na kulipa kidogokidogo kiasi kwa bajeti ya mtu aliyokuwa akitumia kwa mwezi katika matumizi ya kawaida haitaathirika, hivyo biashara mitaani hazitaathirika na hatua hizi.
lakini tunachokiona ni wanasiasa kuja anawaza jambo moja katika possibilities nyingi na kulazimisha watu kufuata analowaza yeye.
kwa mazingira yetu nani anaweza kukosoa uongozi, si kwa kuandika mitandaoni bali kwa kulazimisha utekelezaji wa mambo.
tunahitaji mihimili mitatu inayosimamiana na si kutumia mifumo ya mtu mmoja kulazimisha yeye analowaza tu.