voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,545
- 11,943
Mabadiliko yaliyofanywa na Rais Samia kwenye baraza la Mawaziri.Ni kiini macho.
Uhalisia ni kwamba Rais Samia alikusudia na anaendelea kujisimika na kujiimarisha kwa mbinu zozote zile ili kujiwekea mazingira ya ushindi wa urais 2025. Hili kumuweka mkwewe kwenye Tamisemi ni mpango rasmi kujipanga na uchaguzi mkuu. Sababu huyo ni mtiifu na mwanafamilia hivyo anaaminika na pia hata Msoga.Maana ni mswahili wa hapohapo pwani.
Rais amemuweka pale nwanafamilia ili kuhakikisha hamuangushi mama mkwe.Na soon kidogo tutaanza kuona mikeka mipya ya ma - RC's na ma- DC's kwa kutegemea nani yuko kundi lipi na mlengo upi ndani ya CCM.
Na Makamba jr,kapelekwa Mambo ya nje kwa mpango maalumu.Despite kwamba Kikwete na kundi lao wanataka kumuandaa na kuweka mtu wa kulinda na kuyaendeleza maslahi yao ifikapo 2030.
Endapo kama watakuwa wameponyoka na kupora tena 2025. Pili Makamba kawekwa pale Mambo ya nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki.Sababu ndiyo wizara pekee ambayo waziri anasafiri mara nyingi kwenda nje kimajukumu tofauti na wizara zingine.
Pia ileweke kwamba Makamba kule Tanesco na kwingineko wizarani "Nishati" ameingiza serikali mikataba mingi mikubwa yenye utata, na tena yenye kugharimu maabilioni kama sio trilioni.Ambapo yeye na washirika wake ni wanufaika wakubwa. Hata kwenye Bwawa la Nyerere kuna harufu kubwa ya ufisadi kutokana na kucheleweshwa kwa ukamilishwaji wa Mradi. Ambapo kisheria ya mkataba.
Mhandisi wa mradi alipaswa na anapaswa kuilipa serikali riba ya ucheleweshaji.Lakini wizara imekuwa bubu hata pale ambapo wabunge wamejaribu kuhoji kupitia vikao vya bunge bila mafanikio. Sasa basi...Kwa kigezo hicho itakuwa rahisi Makamba kufanya monitoring muda wote endapo itahitajika kurekebisha hitilafu vaina ya kundi lao na wapewa tender zenye rushwa huko nje hususan India.
Ni rahisi kwake Makamba kukimbia nje huko na kuyatatua juu kwa juu na kisha kurudi kwa kigezo cha uwaziri mambo ya nje. Nashauri kama kweli bunge lina wazalendo ni wakati sasa Serikali kupitia Bunge iunde tume huru na ikachunguze madudu ya Tanesco chini ya uongozi wa makamba pamoja na Bodi yake aliyoiteua muda mfupi baada ya kuteuliwa kuiongoza wizara ya Nishati.
Na matokeo ya tume yatolewe hadharani Na kusomwa bungeni. Badala ya kumuuzia Biteko mbuzi wa Tanesco kwenye gunia! Serikali ingetimiza wajibu wake kwa maslahi mapana ya ustawi na Maendeleo ya nchi yetu.
Tunachezewa mno.....
Sakata la mafuta liwe kianzio
Nawakilisha!
Ni wakati sahihi kwa watanzania kuamka na kutetea haki zetu na maliasili zetu.