Mabadiliko makubwa Ligi Kuu Bara 2014/2015

Mabadiliko makubwa Ligi Kuu Bara 2014/2015

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,687
TFF limesema msimu mpya wa Ligi Kuu Bara, ambao unatarajiwa kuanza Septamba 20, utakuwa na mabadiliko makubwa, zikiwemo mechi za usiku.

"Pia Bodi ya Ligi Kuu imeamua kuongeza askari wa usalama hadi 400 kwa ajili ya kulinda amani siku watani wa jadi Simba na Yanga watakapokutana!"


​


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Bodi ya Ligi, limesema msimu mpya wa Ligi Kuu Bara, ambao unatarajiwa kuanza Septamba 20, utakuwa na mabadiliko makubwa, zikiwemo mechi za usiku.
Ofisa mtendaji wa bodi hiyo, Silas Mwakibinga, amesema wamechukua uamuzi huo kwa ajili ya kuondoa usumbufu wa kuahirishwa kwa mechi bila sababu za msingi, hali ambayo imekuwa ikileta kero kwa wadau wa soka.


Ameongeza kuwa, tayari utaratibu huo umekamilika na mechi hizo zitakuwa katika Uwanja wa Chamazi Complex lakini si Uwanja wa Taifa kutokana na gharama za uendeshaji.


Kwa miaka mingi, kumekuwa na kero ya kuahirishwa kwa mechi kutokana na mgongano wa ratiba, lakini sasa limepatiwa ufumbuzi.


"Msimu huu kuna baadhi ya mechi zitachezwa usiku. Tumeamua kuanzisha kitu kiitwacho ‘match day', yaani mechi za siku husika. Hatutaki msimu huu na kuendelea kuwepo kero ya kuahirishwa mechi pasipo na sababu za msingi.


"Zitakuwa katika Uwanja wa Chamazi na tayari tumekubaliana kuhusu hilo lakini si kwa upande wa Uwanja wa Taifa, una gharama kubwa za umeme, tofauti na Chamazi," alifafanua Mwakibinga.


Akifafanua hali ya viwanja, Mwakibinga alisema viwanja vyote vipo tayari kwa matumizi msimu huu, japo Nangwana Sijaona ambao utatumiwa na Ndanda upo katika hatua za mwisho kabisa katika ukarabati, lakini ndiyo utatumika kwa mechi zake.


Chanzo: SalehJembe
 
Sio mbaya, ila nilijua mabadilijo ya kuongeza timu shiriki hadi kufikia 20 kumbe baadhi ya mechi kuchezwa usiku!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Sio mbaya, ila nilijua mabadilijo ya kuongeza timu shiriki hadi kufikia 20 kumbe baadhi ya mechi kuchezwa usiku!!!!!!!!!!!!!!!!

kuongeza timu ziwe ishirini bila ushindani Wa maana ni sawa na kazi bure
 
kuongeza timu ziwe ishirini bila ushindani Wa maana ni sawa na kazi bure

unafikiri wewe ushindani katika ligi unaletwa na nini umesahau ligi iliyoisha ilivyokua na changamoto kama sio azam kuhonga mechi za mwisho zilikua tamu sana
 
wapiganie Afrika na sie tuwe na klabu bingwa walau ya timu mbili kila league kama ilivyo ulaya wenzetu wanaenda timu 4 uefa sie tumekalia katimu kamojamoja,ushindani utatoka wapi timu chache kila msimu watu walewale na likely timu ni zile zile? unapopeleka timu nyingi unasaidia wachezaji wengi kuimalika na kupata uzoefu mkubwa lakini pia inasaidia kujenga timu za taifa zenye nguvu kufuatia uzoefu wa wachezaji wa vilabu vyao na hata tukienda nje ya bara itatusaidia kuweka ushindani wa viwango walau
 
Ligi haiwezi kuwa bora wakati hakuna ubora kwenye ligi daraja la kwanza na vile vile yarudishwe madaraja ya pili tatu na nne na yaende sambamba na ligi kuu.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom