Mabadiliko Katiba ya CCM Yamelenga Kumwengua Lowassa

Mabadiliko Katiba ya CCM Yamelenga Kumwengua Lowassa

Kwa nini hawataki Lowassa awe Rais?

Wazalendo wa nchi hii wanaogopa ataiuza nchi ; na kutufanya wananchi hali zetu zirudi kuwa duni zaidi ya enzi ya ukoloni!! He will change the country into a banana/Narco state through his colabolation with the Iranian mafia!!
 
Lowasa is our next president piga, ua, galagaza. Masai ndani ya ikulu.
 
wakimuengua kwa zengwe aingie chama chochote cha upinzani,halafu akishika nchi ndipo ccm watakapo tia akili sasa.Wacha tusubiri tuone nani atakuwa rais kama ccm wataamua kumpa tiketi Migiro au Mwinyi,halafu Lowasa asimame kupitia CCK kwa mfano!
 
Waache wanamagamba wakajizike wenyewe huko pembezoni mbali kabisa na paji la nyuso zetu.
 
Hapa bila kuhusisha tetesi, ni dhahiri kwamba haya mabadiliko ni ya kumbeba Lowasa wala siyo kumuengua. Hawa wazee waliondolewa ni wale wenye msimamo na maamuzi thabiti juu ya kile wanachokiamini. Kuwemokwao ndani ya vikao vya maamuzi kulikuwa kunatia shaka juu ya nini utakuwa msimamo wao juu ya Lowasa. Na sasa wajumbe waliobaki wote Lowasa anawamdu!!!

So, far haijajulikana ni nani na nani ambao wataingia kwenye CC, kikao cha juu kabisa ambacho hufanya mchujo wa majina. Kwa sasa ni mapema sana kusema kwamba wajumbe waliobaki wote Lowassa anawamudu.

Kamati Kuu ijayo itakuwa na wajumbe wachache sana ukilinganisha na hili kundi la sasa. Wenyeviti wa Jumuiya za Chama, Wateule 3 wa JK kutoka NEC, na wengine wanaoingia kwa kofia zao Mwenyekiti wa CCM, Makamu wa Bara na Visiwani, Katibu Mkuu, Naibu wa Bara na Visiwani, Waziri Mkuu na Spika wa Bunge. So, nguvu ya mgombea itategemea sana composition hii mpya.

Kwa hiyo ni mapema sana kusema chochote kwa sasa.
 
There is arguably no replacement for Lowassa to stand for the next presidential elections. However hard they might try to kick him out of the race, they can not shrug off the fact that he (Lowassa) has already won millions of electors hearts. Unless they deploy KGB's ill ways of getting rid of people who appear to pose 'threat', the exercise of preventing EL from contesting next presidential poll might prove to be even harder than an arrangement for an election itself.
 
Lowasa is our next president piga, ua, galagaza. Masai ndani ya ikulu.

Lowassa anaishi na kuongoza tu wamasai ila yeye ni MMERU kwa asili. Ila keshakubalika ndani ya jamii ya kimasai lakini haifuti asili yake. Chukulia mfano kwa historia ya Obama, very alike.
Nawasilisha.
 
There is no replacement for Lowassa to stand for the next presidential elections. However hard they might try to kick him out of the race, they can not shrug off the fact that he (Lowassa) has already won millions of electors hearts. Unless they deploy KGB's ill ways of getting rid of people who appear to pose 'threat', the exercise of preventing EL from contsting next presidential polls might be even harder than arranging an election itself.

A bit of truthness!
 
Wao wanawaza 2015 mwenzao anawaza kuwang'oa kwenye uchaguzi wa chama 2012 . Kazi kweli kweli.
 
Ningekuwa na uwezo wa kuitumbukiza ccm yote ndani ya chupa,ningueifungia humo na kutia muhuri wa hatari juu ya kizibo.
Halafu ningeitupa hiyo chupa chini ya bahari ya kina kirefu kuliko vyote.

Ikala kifungo cha miaka sawa sawa na umri wa nchi hii tangu uhuru.

Bora chama chochote ambacho itakuwa rahisi kukiondoa baada ya miaka mitano au minne(kama hakita deliver) kuliko ccm tena!
 
Lakini ukweli unabaki kuwa Lowassa anaogopwa sana na JK ndio maana wanatafuta kila namna ya kumuengua
 
Hapa bila kuhusisha tetesi, ni dhahiri kwamba haya mabadiliko ni ya kumbeba Lowasa wala siyo kumuengua. Hawa wazee waliondolewa ni wale wenye msimamo na maamuzi thabiti juu ya kile wanachokiamini. Kuwemokwao ndani ya vikao vya maamuzi kulikuwa kunatia shaka juu ya nini utakuwa msimamo wao juu ya Lowasa. Na sasa wajumbe waliobaki wote Lowasa anawamdu!!!
Nakubaliana na wewe. EL atakuwa na nguvu zaidi. Kwa sasa tu wananchi wanamkubali sana huko mawilayani, je, ukileta wajumbe wa NEC 400 badala wa 200 wa sasa, hiyo sample ya wajumbe 400 kutoka huko huko mawilayani si inaonyesha atakuwa na nguvu zaidi, hata kama yeye hatakuwa mjumbe humo NEC. Lakini kumbuka wilaya ya Monduli, wataleta mtu mmoja tu (EL) kwenye CC ili ateuliwe mgombea NEC ("watakosa" mpinzani wa EL). Itakuwaje? Monduli isiwe na mwakilishi? EL ataendelea kuwa ndani ya NEC. Subiri uone.
 
Nakubaliana na wewe. EL atakuwa na nguvu zaidi. Kwa sasa tu wananchi wanamkubali sana huko mawilayani, je, ukileta wajumbe wa NEC 400 badala wa 200 wa sasa, hiyo sample ya wajumbe 400 kutoka huko huko mawilayani si inaonyesha atakuwa na nguvu zaidi, hata kama yeye hatakuwa mjumbe humo NEC. Lakini kumbuka wilaya ya Monduli, wataleta mtu mmoja tu (EL) kwenye CC ili ateuliwe mgombea NEC ("watakosa" mpinzani wa EL). Itakuwaje? Monduli isiwe na mwakilishi? EL ataendelea kuwa ndani ya NEC. Subiri uone.
Issue hapa ni kwamba JK anafahamu Lowassa ukimpeleka NEC na Mkutano Mkuu atashinda kwa kishindo. Mbinu wanayotaka kuitumia ni kulikata jina lake katika hatua ya kamati kuu. Sasa wanajaribu kuwaengua wale wajumbe wenye msimamo mkali kamati kuu ili upinzani wa kumwondoa Lowassa usiwe mkubwa
 
kwa sababu ni fisadi namba moja tz

WANAOSEMA LOWASSA NI FISADI KWA SABABU YA RICHMOND SAGA, HAMKUONA HII TAARIFA NILIYOIONA MAHALI?
EDWARD LOWASSA ALISAFISHWA NA MWAKYEMBE ​
Sasa ni wazi kwamba baada ya waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa kujitetea mbele ya kikao kilichopita cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) mjini Dodoma, wajumbe wengi wa kikao hicho, na wachambuzi wa mambo ya kisiasa nchini wanakubaliana kwamba mbunge huyu wa Monduli amekuwa akisakamwa na baadhi ya viongozi ndani ya chama chake na watu wengine, si kwa sababu yeye ni fisadi au kuna tuhuma za ukweli za ufisadi dhidi yake, bali ni kwa sababu ya mbio za urais za mwaka 2015.
Ingawa yeye mwenyewe hajakubali wala kukanusha nia yake ya kugombea urais mwaka 2015 kupitia chama chake, lakini zimejengeka hisia kwamba ana nia hiyo, lakini kinachoumiza wengi si hiyo nia tu, maana na wengine wengi tu ndani ya chama hicho wanaelezwa kuwa na nia hiyo. Kinachowasumbua watu wasiompenda ni kwamba kati ya hao wanaodhaniwa kuwa na nia
Inawezekana kumbukumbu za watu wengi zimechakachuliwa kiasi cha kutokumbuka kwamba Kamati Teule ya Dr. Harrison Mwakyembe iliyokuwa inachunguza sakata la mkataba wa kufua umeme baina ya TANESCO na kampuni ya Richmond ilimsafisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kwamba hakuwajibika na kujiuzulu kutokana na ufisadi wake katika sakata hilo, bali aliwajibika kisiasa kwa makosa ya watu waliokuwa chini yake.
Inashangaza pia kwamba hata wajumbe wa Kamati hiyo, akiwemo mwenyekiti wao, Dr. Mwakyembe, wanashindwa kumtetea Bw. Lowassa anapoendelea sasa hivi kusakamwa na baadhi ya wanasiasa na wanajamii kwamba ni fisadi kutokana na kashfa ya Richmond, na hawajitokezi kumtetea na kurejea hitimisho la ripoti yao ndani ya Bunge. Lakini mbaya zaidi hata baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu kabisa wa chama chake hawakumbuki hitimisho la ripoti hiyo na wameng'ang'ania kwamba kujiuzulu kwa Lowassa uwaziri mkuu hakutoshi na inabidi chama kimtose zaidi kutokana na kashfa ya Richmond.
Kwa kweli suala la tuhuma dhidi ya Edward Lowassa kwamba ni fisadi kutokana na tuhuma za Richmond, mtu unaweza kusema huu ni unafiki na chuki za kisiasa zilizopita kipimo. Suala la Richmond ni moja kati ya kashfa hapa nchini ambazo zilichunguzwa kwa makini sana na Bunge kupitia Kamati Teule na matokeo na hitimisho la uchunguzi huo yakamsafisha Lowassa kwamba alijiuzulu siyo kwa sababu alihusika moja kwa moja na kashfa hiyo bali aliwajibika kwa makosa yaliyotendwa na watu wa chini yake.
Tarehe 15 Februari 2008, kwa mujibu wa taarifa rasmi za majadiliano Bungeni (Hansard), Dr. Harrison Mwakyembe, wakati akihitimisha hoja ya Kamati Teule iliyochunguza suala la Richmond, alisema:
"Mheshimiwa Spika, ninaomba nianze na utangulizi mfupi na rahisi; uwajibikaji kwa viongozi waandamizi katika nchi zinazolinda na kuenzi demokrasia kama vile Tanzania, una sura mbili; sura ya kwanza, kiongozi anawajibika kwa makosa yake mwenyewe ya kiutendaji. Kiongozi anafanya maamuzi mabaya, pengine kwa kishawishi cha pesa, maamuzi yake yakaleta hasara au kiongozi ameshindwa kutoa ushauri mzuri kama kiongozi, kwa kukiuka kanuni, kukiuka taratibu na kadhalika, matatizo yakatokea, anawajibika. Sasa sura hii ya uwajibikaji, inahusisha uvunjwaji wa maadili, kanuni, sheria, miiko ya uongozi na kadhalika. Chini ya uwajibikaji wa aina hii, kiongozi anaweza akashitakiwa, akaadhibiwa mbali na kuachia ngazi. Nitarejea kwenye sura hii hivi punde. Suala la msingi hapa ni kuwa, kuna element ya adhabu katika sura hii ya kwanza.
"Sura ya pili; kiongozi anawajibika kwa makosa ambayo si yake moja kwa moja ila yaliyofanywa na watendaji chini yake. Kitendo cha kuwajibika kwa aina hii, kunaijengea Serikali au taasisi heshima na imani ya pekee katika jamii, kunatoa picha ya kwamba, uongozi unajali, unalielewa tatizo kwa kubeba lawama wao wenyewe. (Makofi)
"Mheshimiwa Spika, katika suala hili la Richmond, viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini na Waziri Mkuu, walikuwa wanakabiliwa na uwajibikaji wa aina hizo mbili. Kwanza, uwajibikaji unaotokana na makosa ya viongozi wenyewe katika maamuzi yao, maelekezo yao, maagizo yao na kadhalika. Mawaziri wote wawili wa Nishati na Madini; aliyetangulia na aliyefuatia baadaye, Katibu Mkuu na Kamishina wa Nishati, wote tukawaona wana makosa ya moja kwa moja, waliyoyafanya wao kwa njia moja au nyingine. Kwa kuwa uwajibikaji wa aina hii, unatokana na ukuikwaji wa kanuni, taratibu, maadili, sheria na kadhalika, Kamati Teule ikahakikisha inawahoji wote ili kusikia their side of the story kabla ya kutoa pendekezo la kuwawajibisha kwa makosa waliyofanya. Ndiyo maana baada ya kuwahoji, tumependekeza hatua za kuchukuliwa dhidi yao.
"Hali haikuwa hivyo kwa Waziri Mkuu; Kamati teule ilikuwa na ushahidi wa mawasiliano ya karibu kati ya Waziri Mkuu na Uongozi wa Wizara. Ushahidi huo haukutosha kwa uwajibikaji wa sura ile ya kwanza wa kiongozi kukutwa na makosa ya moja kwa moja, aliyoyafanya yeye mwenyewe kwa njia moja au nyingine, lakini ushahidi huo ulitosha kwa uwajibikaji wa sura ya pili, ambao hauhitaji mahojiano, kusikilizwa wala utetezi. Unawajibika kwa makosa ya watendaji walio chini yako. Hiyo ndiyo demokrasia. Wabunge wengi wametoa mifano mingi hapa, ukiwemo wa Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi, alipokuwa waziri wa Mambo ya Ndani; aliwajibika kwa makosa ya askari huko Shinyanga wakati yeye alikuwa Dar es Salaam; hatukumsikia akidai apewe nafasi ya kusikilizwa na hata kama angepewa, bado angewajibika yeye mwenyewe. (Makofi)
"Mheshimiwa Spika, Kamati Teule inatamka ukurasa wa 37 wa taarifa yake kuwa, ninanukuu ‘Ushiriki huu wa karibu wa Waziri Mkuu katika kila hatua ya zabuni ya umeme wa dharura si lazima uwe ushahidi wa kwamba, kiongozi huyo wa Kitaifa alihusika katika kuibeba Richmond. Unaweza pia ukawa ushahidi wa style yake ya kawaida kabisa ya Waziri Mkuu katika kufuatilia masuala yote ya Kitaifa kwa karibu sana, tukizingatia kwamba, nchi wakati huo ilikuwa katika kipindi kigumu sana cha ukosefu wa umeme….."
Nina wasiwasi kwamba baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa na wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM ama wamesahau kauli hii ya Dr. Harrison Mwakyembe, ama kwa makusudi wanataka kupotosha watanzania. Akina Nape Nauye na John Chiligati wanamjumuisha Edward Lowassa kwenye kundi la mafisadi kutokana na suala la Richmond. Lakini Chiligati alikuwa Bungeni wakati Mwakyembe akihitimisha hoja ya Kamati yake Teule, na alimsikia Mwakyembe akimsafisha Lowassa kwamba makosa yake hayakuangukia kwenye sura ya kwanza ya uwajibika, ya kiongozi kuwajibika kwa makosa yake mwenyewe. Sura hii ndiyo unayoweza hata kumwita mtu fisadi. Lakini Lowassa aliwajibika kwa makosa ya watendaji walio chini yake, hata kwa mujibu wa Dr. Mwakyembe. Anayewajibika kwa aina hii ya pili huwezi kumwita fisadi. Akisifu aina hii ya Edward Lowassa kuwajibika, Dr. Mwakyembe anasema, "…Kitendo cha kuwajibika kwa aina hii, kunaijengea Serikali au taasisi heshima na imani ya pekee katika jamii, kunatoa picha ya kwamba, uongozi unajali, unalielewa tatizo kwa kubeba lawama wao wenyewe". (Makofi). Mwakyembe anakwenda mbali na kuhusisha uwajibikaji huu wa Lowassa na ule wa Mzee Ali Hassan Mwinyi.
Naye Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiwasilisha utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu suala hilo tarehe 28 Agosti 2008 alisema yafuatayo kuhusu azimio na. 16 la Waziri Mkuu kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huo, "Mheshimiwa Naibu Spika, hatua zilizochukuliwa ni kwamba, Azimio hili lilitekelezwa mwezi Februari, 2008 kwa kuwa aliyekuwa Waziri Mkuu aliamua kujiuzulu kwa kuwajibika kisiasa kwa maslahi ya Taifa." Hivyo ni wazi hata Serikali inakubaliana na Kamati Teule kwamba Mhe. Lowassa aliwajibika, siyo kama fisadi bali aliwajibika kisiasa kwa maslahi ya Taifa. Ndiyo maana Azimio na. 16 linalomhusu Waziri Mkuu halikuendelea kujadiliwa Bungeni. Hata wanaodai kwamba baadaye Spika aliondoa hoja hii Bungeni kabla halijakamilika, wajue kwamba suala la Waziri Mkuu kuwajibika (Azimio na. 16) halikuwemo tena, na kwa hiyo hata hoja ingeendelea kuwa Bungeni Lowassa asingeguswa tena.
 
Nilikuwa nazungumza na mtu mwenye cheo cha juu sana ccm akaniambia mabadiliko ya katiba ya CCM ni moja ya mikakati ya kumwondoa Lowassa katika kinyanganyiro hivyo akina Nape wameshinda round ya awali. I

Kwamba Lowassa ana nguvu sana na ukimpeleka Halmashauri kuu na Mkutano mkuu atashinda. Mkakati ni kumwondoa katika ngazi ya kamati kuu lakini kisiki alikuwa Mkapa na viongozi wengine wastaafu akiwamo Karume. hivyo kuwaondoa hawa Wazee kamati kuu ni kuondoa nguzo ambazo zingemtetea Lowassa wakati wakijadili jina lake likatwe. Na pia anasema mkapa ndie kiongozi mwenye nguvu na msimamo zaidi ndani ya chama hivyo ilikuwa muhimu kumwondoa katika nafasi za maamuzi. Akabainisha jinsi Nyerere alivyoingila mchakato wa kumpata Mkapa ni kwa kuwa alikuwa mjumbe wa vikao vya maamuzi otherwise asingefanya hivyo.


Kwa wale wanaokurupuka watasema ni hadithi ya kutungwa, sawa tu ila anayeweza kuwaza vizuri ataona mantiki ya taarifa hiyo
Mkuu kwa hali ilivyo uliyoyasema hapo yana vimelea vya ukweli kwa zaidi ya asilimia tisini.
 
Back
Top Bottom