Mabadiliko Baraza la Mawaziri: Prof. Palamagamba aula, Mwakyembe achukua nafasi ya Nape Nnauye

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,588
11,668
C7lJ_j7VUAAZgnE.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 23 Machi, 2017 amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri.

Katika Mabadiliko hayo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Aidha, Mhe. Dkt. Magufuli amemteua Dkt. Harrison George Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Uteuzi huu unaanza mara moja.

Wateule wote wataapishwa kesho Mchana tarehe 24 Machi, 2017 Ikulu, Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

23 Machi, 2017
 
Back
Top Bottom