Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imemtia hatiani Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni(KUB) Freeman Mbowe kwa kudharau mamlaka ya spika.
Halima Mdee pia ametiwa hatiani na kamati hiyo kwa kudharau mamlaka ya Spika na kutoa lugha ya matusi bungeni
Akisoma uamuzi huo, mjumbe wa kamati, Almasi Maige amesema Bunge lijadili na kutoa uamuzi.
Amesema wote wawili walikiri kwenye kamati na kuomba radhi.
Kwa kuwa Mbowe ni kosa la kwanza, aliitikia wito bila usumbufu na aliomba radhi, Bunge limeazimia kumsamehe.
Kuhusu Mdee, kamati imependekeza azuiwe kuhudhuria vikao vyote vilivyobaki bunge la bajeti.
Kwa hisani ya Mwananchi
=======
UPDATES;
Baada ya Bunge kujadili taarifa ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Haya hapa chini ndio uamuzi Uliochukuliwa;
=> Bunge limeazimia kumsamehe Mhe Mbowe baada ya kukiri kosa la kutoa kauli za kudharau Bunge.
=> Bunge limetoa karipio kali kwa Mhe Bulaya, baada ya kukiri kosa la kudharau Mamlaka ya Bunge.
=> Baada ya majadiliano, Bunge limeazimia kuwa Mhe Mdee asamehewe kwa masharti kwamba akirudia kosa anadhibiwa bila kupelekwa Kamati ya Maadili.
=> Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam na Mkuuwa Wilaya ya Arumeru Alexanda Mnyeti pia wamesamehewa bila masharti yoyote.