Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) imetoa
waraka uliojumuisha mambo mbalimbali, ikiwa ni
pamoja na kuwataka viongozi kutenda haki,
kutokuwa na upendeleo, kuheshimu Katiba na
sheria za nchi.
Pia jumuiya hiyo imewataka Watanzania kwa
ujumla kuliombea taifa na viongozi wake, ili wawe
walinzi wa Katiba na sheria za nchi kama
walivyoapa.
Waraka huo ulisambazwa jana katika vyombo vya
habari, ukiwa umetiwa saini na Askofu Mkuu wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk.
Fredrick Shoo na Askofu Mkuu wa Kanisa la
Anglikana Tanzania (KAT), Dk. Jacob Chimeledya.
Wengine ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian
Tanzania (KMT), Dk. Isaac Nicodemo na Askofu
Mkuu wa Kanisa la African Inland Church in
Tanzania (AICT), Silas Kezakubi.
“CCT inatoa maelekezo kwa Wakristo wa
makanisa wanachama na Watanzania wote kwa
ujumla, kuendelea kulinda na kuheshimu misingi
ya haki za binadamu na kuliombea taifa na
viongozi wake ili waendelee kuwa na hofu ya
Mungu na waadilifu.
“Watende haki, wasiwe na upendeleo na
waheshimu na kuwa walinzi wa Katiba na sheria
za nchi kama walivyoapa,” ilisema sehemu ya
waraka huo.
CCT ilieleza pia kusikitishwa na vitendo vya
ujambazi na matumizi ya silaha katika jamii na
kukemea matukio ya ukatili na yale ya watu
kupotea katika mazingira ya kutatanisha.
“CCT inasikitishwa na vitendo vya ujambazi na
matumizi ya silaha katika jamii yaliyofikia kiwango
cha kuua askari polisi."
Aidha, CCT inakemea matukio ya ukatili
unaondelea katika jamii.
“Yapo matukio ambayo yamedhihirisha
ushirikiano hafifu kati ya polisi na wananchi na
kuendelea kujitokeza kwa matukio yanayoashiria
chuki za kidini na kikabila.
“CCT inatoa wito kwa Serikali kuhakikisha
misingi ya umoja na mshikamano wa kitaifa
inaheshimika na utawala wa kisheria unafuatwa,”
ilisema taarifa hiyo.
Dawa za Kulevya
CCT ilisema ili vita dhidi ya dawa za kulevya
ifanikiwe, ni muhimu Serikali ikalenga kutokomeza
kiini cha tatizo kwa kuwapata wahusika wakuu wa
biashara hiyo bila kujali wasifu wao na nafasi
walizonazo katika jamii.
Kutokana na hilo, CCT ilisisitiza kuwa Serikali
izingatie misingi ya sheria, haki na usawa katika
kuwakamata, kuwapekua na kuwafikisha katika
vyombo vya sheria bila kuonea mtu wala
kusukumwa na misingi yoyote ya imani au itikadi
ya mtu.
“CCT inaunga mkono vita dhidi ya matumizi ya
dawa za kulevya na viroba iliyoanzishwa na
Serikali. Hata hivyo, CCT inasisitiza kuwa ili vita
hii ifanikiwe, ni muhimu sana Serikali ilenge
kutokomeza kiini cha tatizo kwa kuwapata
wahusika wakuu wa biashara hii bila kujali wasifu
wao, nafasi zao wala nafasi walizo nazo katika
jamii.
“Katika kufanya hivyo, ni muhimu Serikali izingatie
misingi ya sheria, haki na usawa katika

vyombo vya sheria bila kuonea wala kusukumwa
na misingi yoyote ya imani au itikadi ya mtu.
“Ni muhimu kwa Serikali kuendelea kuweka
mazingira wezeshi kwa vijana kupata ajira na
kuendesha shughuli za ujasiriamali ili kujiepusha
na vitendo viovu vikiwemo matumizi ya dawa za
kulevya na unywaji wa pombe kali.
“CCT inayaelekeza makanisa wanachama, wazazi
na walezi kuendelea kuwalea vijana wao katika
misingi ya kidini ili wasijiingize katika matumizi
ya dawa za kulevya na pombe kali.
“Wakati huu wa Kwaresma, tunawaombea na
kuwaomba wale wote ambao kwa njia moja au
nyingine wanajihusisha na dawa za kulevya au
unywaji wa pombe kali, watubu na kuyaacha
maovu yao na Mungu atawarehemu,” walisema
maaskofu hao.
Hali ya Chakula
Kuhusu hali ya chakula nchini, CCT ilisema kuwa
pamoja na mvua kuanza kunyesha, Serikali na
wengine wawezeshe usambazaji wa chakula
kutoka mikoa yenye ziada kwenda mikoa yenye
uhaba wa chakula ili bei ya chakula iweze
kushuka.
“Tunaiomba Serikali kupitia idara yake
inayohusika, iratibu na kusaidia utekelezaji wa
jambo hili, ili wananchi waweze kumudu bei,
mfano mahindi hayo yakisambazwa, bei ishuke
kutoka zaidi ya Sh 100,000 ifikie angalau Sh
60,000.
“Pia tunawaomba wakulima wasitumie njaa hii
kutekeleza usemi ya kwamba ‘kufa kufaana’,
hivyo kwao kipindi hiki kigumu kwa Watanzania
wengine wakakifanya kipindi cha kupandisha bei
ili kupata faida kubwa.
“Sambamba na wito huu, tunawaekeleza
wanachama wetu kupitia vitengo vya maafa na
misaada ya kibinadamu, waendelee kuwasaidia
wananchi wenye upungufu mkubwa wa chakula
wakipate kwa bei nafuu kwenye maeneo yao,”
ilisema.
CCT iliwataka Wakristo wote kuendelea
kumwomba Mungu ili mvua zinazoendelea
kunyesha ziwe za neema na zisilete madhara.
Katika hilo, wameiomba serikali kutoa unafuu wa
bei ya gesi ya kupikia ili wananchi wengi
wapunguze au kuachana kabisa na matumizi ya
kuni na mkaa.
Elimu
CCT ilisema pamoja na nia njema ya Serikali
kutoa elimu bure, lakini iangalie masilahi ya
walimu na kuwe na mpango mkakati
unaotekelezeka wa kuimarisha miundombinu ya
kufundishia.
“Serikali haina budi kuendelea kutoa elimu ya
kutosha kwa wananchi kuhusu dhana ya elimu
bila malipo, ili kuepusha migogoro inayokabili
sekta ya elimu kwa dhana hiyo kutoeleweka kwa
vizuri kwa baadhi ya wananchi.
“Pia mabadiliko ya mitaala na miongozo mingine
ya kufundishia ya mara kwa mara imekuwa
ikiathiri elimu ya Tanzania kwa kila awamu ya
uongozi na kuwafanya wahitimu wetu kukosa
ushindani kikanda na kimataifa,” ulisema waraka
huo.
Kupitia waraka huo, maaskofu waliishauri Serikali
kuwa na será ya elimu isiyobadilika badilika kila
uongozi mpya unapoingia madarakani
CHANZO MPEKUZ BLOG.