Maaskofu watema cheche Ijumaa Kuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maaskofu watema cheche Ijumaa Kuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Apr 8, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Waandishi Wetu
  VIONGOZI wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo nchini jana walitumia Siku ya Ijumaa Kuu kukemea rushwa, matumizi ya mabavu na kuhamasisha waumini wao kukataa kupitishwa kwa sheria zenye lengo la kuhalalisha uovu katika taifa.

  Kadhalika, viongozi hao waliishukia Serikali na taasisi zake za dola kwa kushindwa kutumia sheria kudhibiti uovu kama vile rushwa na ufisadi na kuonya, hali ikiichwa kama ilivyo italifikisha taifa pabaya.

  Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati, Thomas Laizer alisema rushwa ambayo sasa inaitwa ufisadi imekuwa kero kubwa kwa wananchi na kuwakosesha haki zao za msingi. Pia alieleza kukerwa na tabia za wanaogombea nafasi za uongozi kupiga kampeni kwa kutumia lugha za matusi dhidi ya wagombea wengine badala ya sera na kwamba tabia hiyo haina tija kwa wananchi.

  Naye Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Arusha, Josephat Lebulu alikemea matumizi ya mabavu yanayofanywa na wenye mamlaka dhidi ya wanyonge. Alisema kamwe viongozi wa kanisa hawawezi kukaa kimya katika hilo kwa sababu wao ni sauti ya kinabii ya kutoa mwelekeo wa mambo yanayoendelea.

  Katika Ibada ya Kitaifa ya Ijumaa Kuu, iliyofanyika katika Kanisa Kuu Katoliki Jimbo la Morogogo, Askofu wa Jimbo hilo, Mhashamu Telesphor Mkude aliwataka Watanzania kupiga vita utoaji mimba ambao alisema kuwa ni tatizo kubwa nchini.

  Askofu Mkule alisema licha ya tatizo hilo kukithiri katika jamii ya Watanzania, vitendo hivyo pia ni chukizo kwa Mungu na kwamba mwenye uwezo wa kukatisha maisha ya mwanadamu ni Mungu pekee.

  Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania, Alex Malasusa amewataka washarika wote kujenga hofu ya Mungu katika maisha yao ya kila siku.Alizungumza hayo alipokuwa akiongoza ibada hiyo katika Kanisa la Azania Front, Dar es Salaam.

  “Iwe Ijumaa Kuu kwelikweli. Viongozi wafanye mambo yanayompendeza Mungu maana wanapenda kufanya mambo yanayowanufaisha wao. Uhuru wa nchi si uhuru wa kiroho unaweza kuishi katika nchi yenye demokrasia lakini kama unatenda dhambi haisaidii,” alisema Malasusa

  Rushwa, mabavu, mimba

  Katika ibada ya pamoja Mjini Arusha, Askofu Laizer alisema pamoja na mafundisho, mahubiri na semina zinazotolewa na viongozi mbalimbali, bado rushwa imezidi kuwanyanyasa wanyonge kwani wao ndiyo waathirika wakubwa na huku wachache wakinufaika kutokana na ubinafsi.

  “Rushwa katika uchaguzi huko ndiyo usiseme, ni wiki moja sasa uchaguzi wa Arumeru Mashariki umefanyika, hakika umetufundisha mengi. Nataka nitoe somo lisilo somo, tumefundisha sana lakini bado rushwa inatolewa hadharani huku Takukuru na Usalama wa Taifa wanaona," alisema.

  Askofu Lebulu kwa upande wake, alisema matumizi ya mabavu ambayo alisema vikundi vya watu vinakaa kwa siri na kupanga mbinu za kumwangamiza mtu asiye na hatia na wakati mwingine hata kuhonga mahakama zipotoshe hukumu dhidi ya mnyonge.

  “Haya mabo yanafanyika ili kumwezesha mwanadamu kupata mambo matatu; mali, bila kujali anatumia njia gani kuzipata, pili; mamlaka ambayo watu wengine wako tayari amkanyage mtu ili ayapate na tatu; ni anasa ambazo sehemu ya Watanzania wametawaliwa nazo.”

  “Ni kweli tunataka amani, lakini haijengwi juu ya mchanga, bali kwenye haki na upendo kwa watu wote na si kundi la watu wachache wenye uwezo wa kutumia rasilimali za nchi huku wananchi wengine wakipata shida katika kupata mahitaji ya msingi.”

  Askofu Mkude katika mahubiri yake aliwatahadharisha Watanzania kutokubali kuwepo na sheria ya kuruhusu utoaji mimba licha ya kuwepo kwa nchi duniani zinazounga mkono…. “Kama Hayati Mwalimu Julius Nyerere, mama yake angeamua kutoa mimba yake je, angeweza kuwa Rais wa mfano na kutangazwa mwenye heri?”

  Alisema kuwa Baba Mtakatifu Benedict wa 16 mwaka jana alimtangaza Nyerere kuwa mwenye heri kutokana na kwamba alijitahidi kuishi kama mkristo katika maisha yake ya uongozi.

  Ubinafsi
  Paroko Msaidizi wa Kanisa Katoliki Chang'ombe, George Sayi aliwataka waumini wa kanisa hilo kutumia siku ya mateso na kifo cha Yesu kujifunza kuacha ubinafisi na kuhimiza upendo miongoni mwao na jamii.

  Akihubiri kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu alisema katika kipindi chote cha maisha yake hadi kifo chake alifanya kazi iliyompendeza Mungu huku akifundisha kwa vitendo upendo wa kweli na watu kuacha chambi.
  http://mwananchi.co.tz/habari/-/21790-maaskofu-watema-cheche-ijumaa-kuu
  Padri Sayi pia alikumbusha umuhimu wa wazazi kuwalea watoto wao katika maadili mema kama ilivyokuwa kwa familia ya Yesu, Maria na Yosefu.

  Habari hii imeandikwa na Filbert Rweyemamu - Arusha, Lilian Lucas - Morogoro, Geofrey Nyang'oro na Dotto Kahindi - Dar.
   
 2. R

  Ray2012 JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 215
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  tunawataka viongozi wetu hawa wa dini kusimamia ukweli, haki na ustawi wa jamii yetu hii iliyokata tamaa
   
 3. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  MAASKOFU MTASEMA SANA MPAKA MPASUKE NDIMI ZENU LAKINI KAMA HAMJUI UKWELI KUWA CHANZO CHA MAOVU YOTE MNAYOYAKEMEA NI KULAANIWA KWA NCHI YETU KWA KITENDO CHA KUTOLITAMBUA TAIFA LA ISRAEL. Tanzania inatumiwa vibaya sana na nchi za kiarabu katika kuchukuia raia na taifa la Israel bila ya sababu. Kama nyie maaskofu mnajua ukweli wa biblia , basi piganieni nchi yetu iwe na uhusiano mzuri sana na Taifa la Israel.

  Adhabu ya kuwachikia waisrael haina kinga. mungu akimwambia Abrahamu kuwa nitampenda yeyote atakayekupenda na kumlaani yeyote atakaye kuchukukia. Ona kiuchumi sisi na Kenya, Nigeria, Ghana na Botswana. wametacha pabaya sana.
   
 4. N

  Nhundu Member

  #4
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 41
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwenye masikio na asikie
   
Loading...