Maaskofu wapingana na pinda

Maaskofu wapingana na pinda

ndiyomkuusana

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
668
Reaction score
426
Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini wameitaka Serikali kutumia njia ya mazungumzo kumaliza migogoro, badala ya kutumia jazba na nguvu. Vilevile, wamesema kuwa hawako tayari kukaa kimya huku wakiona amani na utulivu nchini ikivurugika, badala yake wataendelea kusema ili amani na utulivu viweze kurejea.

Kauli hiyo imekuja baada ya Rais Jakaya Kikwete, kuwataka maaskofu hao na viongozi wengine wa dini nchini kuendelea kuisaidia Serikali katika kuimarisha amani na upendo miongoni mwa wananchi.

Akizungumza wakati wa kuadhimisha Jubilee ya miaka 25 ya uaskofu wake kwenye sherehe zilizofanyika jana katika Seminari ya Mt Peter mjini Morogoro, Askofu wa Jimbo la Morogoro, Telesphor Mkude, alisema meza ya mazungumzo ni lazima itumike katika kuimalisha amani na upendo wa Watanzania badala ya kutumia jazba na nguvu.

Mkude alisema kwa hivi sasa kumeibuka mivutano ya kidini na kisiasa na kutoa mfano wa vurugu zilizoibuka wilayani Sengerema mkoani Mwanza juu ya nani ana haki ya kuchinja au kutokuchinja kati ya waumini wa madhehebu ya Kikristo na Waislamu.

Pia vurugu za mikutano ya kisiasa, makanisa kuchomwa, mapadri na watumishi wengine kuuawa na kuteswa, kutupwa kwa mabomu katika mikusanyiko ya watu ikiwamo makanisa na kwamba yote hayo yangeweza kumalizwa katika meza ya mazungumzo.


  1. Vurugu kubwa zilitokea Jumamosi iliyopita mjini Arusha baada ya mtu ambaye bado hajajulikana, kutupa bomu katika mkutano wa CHADEMA wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika katika viwanja vya Soweto na kuua watu wawili na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa.
  2. Mei 2, mwaka jana, Mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daud Mwangosi aliuawa kwa kulipuliwa na bomu na askari polisi katika vurugu zilizotokea katika eneo la Nyololo mkoani Iringa.
  3. Februaria 18, mwaka huu, Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Minara Miwili, Mji Mkongwe, Zanzibar aliuawa kwa kupigwa risasi asubuhi wakati akienda kuendesha misa katika Kanisa la Mtakatifu Theresia eneo la Mtoni. Mtuhumiwa wa tukio hilo, Omar Musa Makame, anaendelea na kesi mahakamani kujibu tuhuma za mauaji.
  4. Tukio lingine ni lile la watu wawili kuuawa na polisi mjini Songea, Februari 22, mwaka jana, wakati wakizuia maandamano ya wananchi wenye hasira kali waliokuwa wakipinga mauaji yanayohusishwa na imani za kishirikiana.

Hivi karibuni maaskofu hao walitoa tamko la kuitahadharisha Serikali, kudhibiti vurugu za kidini na kisiasa nchini. Walionya kuwa iwapo vurugu hizo hazitadhibitiwa huenda nchi ikaingia katika machafuko.
 
Ni hoja nzuri!... Vinginevyo polisi wakipiga na raia nao watalipa kisasi kwa kuwapiga polisi au kuvamia familia zao!...
 
Polisi wakiamriwa KUFANYA HIVYO, NA RAIA WAKIJIBU MAPIGO MWISHO WAKE ITAKUWA NINI? Au inadhaniwa kuwa wananchi hawana uwezo wa kukabiliana na upizani wa vyombo vya dola? Kumbukeni Tunisia, Libya na Misri hivi karibuni. Wananchi walishinda vyombo vya dola. Nawaunga Maaskofu mkono kuwa si polisi au raia wanaoruhusiwa kujichukulia sheria mkononi. Maelewano au muafaka ni njia sahihi zaidi.
 
Sijawahi kuona au kusikia nchi yoyote duniani yenye askari wengi kuliko raia!

Watawala tafakarini hili na kujirudi, vinginevyo inaweza kufika wakati mtawatawala askari wachache wakaokuwa wamesalia baada ka wengi kuuliwa na raia na raia wote kuuliwa na askari! Tuepushieni watanzania vurugu mnazotaka kuzileta kwa tamaa zenu!
 
Kauli hiyo imekuja baada ya Rais Jakaya Kikwete, kuwataka maaskofu hao na viongozi wengine wa dini nchini kuendelea kuisaidia Serikali katika kuimarisha amani na upendo miongoni mwa wananchi.
sina uhakika kama hizi kauli huwa za kwake binafsi au ndiyo msimamo wa serikali.
 
Hayo yametokea kwa sababu wanao tawala wanauwezo mdogo kuliko wanaotawaliwa tutaendelea kubanana hivyo hivyo!
 
Yote dugu moja

"To know the enemy is half the victory"
 
Back
Top Bottom