Maaskofu Walihusika Vipi na Mgomo wa Ma-dr?

Shinto

JF-Expert Member
Dec 6, 2010
1,781
96
Jana kwenye hotuba ya JK alisema, madaktari walienda kwa maaskofu kabla ya kupelekwa na maaskofu hao hao kwenye mazungumzo na Pinda usiku wa manane. Nataka kujua tu nini ilikuwa role ya maaskofu kwenye sakata hili? Kwa nini madaktari walienda kwa maaskofu kwanza kabla ya kwenda kwenye mazungumzo? Kwa nini maaskofu walilazimisha na wao wawepo kwenye mazungumzo hayo?
 
hivi ni madaktari walienda kwa maaskofu au maaskofu walienda kwa madaktari walipotoka kwa pinda?? Anyways they were MEDIATORS.
 
Mi sikusikiliza hii hotuba, lakini if that is the case,
Iawezekana maaskofu walijaribu ku-mediate mazungumzo yafanyike ili maisha ya watanzania yaokolewe!!

kumbuka pia kwamba Bugando na KCMC ni mali ya makanisa, kwahiyo, walikuwa na direct interest na kumalizika kwa mgomo kwa nia ya mazungumzo.
 
Mkuu, Rais alisema Maaskofu waliwafuata madaktari na kuzungumza nao na kuwa wasuluhishi (mediators) na sio kuwa madaktari waliwafuata maaskofu.
 
Mi sikusikiliza hii hotuba, lakini if that is the case,Iawezekana maaskofu walijaribu ku-mediate mazungumzo yafanyike ili maisha ya watanzania yaokolewe!!kumbuka pia kwamba Bugando na KCMC ni mali ya makanisa, kwahiyo, walikuwa na direct interest na kumalizika kwa mgomo kwa nia ya mazungumzo.
Nakuunga mkono, ktk hospitali kuu nne za rufaa zilizokuwa ktk mgomo, mbili ni za serikali (Muhimbili na Mbeya) na hizo mbili ni za kanisa. Hatujawa na ya Islamic bado.
 
Jana kwenye hotuba ya JK alisema, madaktari walienda kwa maaskofu kabla ya kupelekwa na maaskofu hao hao kwenye mazungumzo na Pinda usiku wa manane. Nataka kujua tu nini ilikuwa role ya maaskofu kwenye sakata hili? Kwa nini madaktari walienda kwa maaskofu kwanza kabla ya kwenda kwenye mazungumzo? Kwa nini maaskofu walilazimisha na wao wawepo kwenye mazungumzo hayo?

Maaskofu wanahusika sana kwenye sakata hilo maana karibu hospitali zote za rufaa ndiyo wanazisimamia. kwa lugha ya sasa maaskofu ni wadau muhimu kwenye tasnia ya afya, fikiria kwa Arusha tu karibu karibu vituo vyote vya afya ni vya kanisa huoni kuwa ni muhimu kwa kanisa kuhakikisha kuwa suluhu inapatikana? "UKIENDA KWENYE MSIBA UTAMJUA TU MFIWA"
 
CCT walimuomba mh Pinda waongee na madaktari...Pinda akawaruhusu wakaonana na madaktari na kuwasihi madaktari wakakubali kuongea na Waziri Mkuu, then wakampigia simu pinda kumpa feedback kisha wakaomba wawepo kwenye kikao ............

hayo ndiyo aliyoyasema pinda....

sioni cha ajabu cha kudiscuss hapa..... kila mmoja ni mdau katika sekta ya afya kwa njia moja au nyingine...iwe mmiliki wa hospitali au la.... kama unanaweza kuconvinse drs wakarudi kutibu na kuokoa maisha ya watu kwa nini wasifanye hivyo???

big up to maaskofu, big up to drs, pig up to jakaya....
 
Maaskofu wanahusika sana kwenye sakata hilo maana karibu hospitali zote za rufaa ndiyo wanazisimamia. kwa lugha ya sasa maaskofu ni wadau muhimu kwenye tasnia ya afya, fikiria kwa Arusha tu karibu karibu vituo vyote vya afya ni vya kanisa huoni kuwa ni muhimu kwa kanisa kuhakikisha kuwa suluhu inapatikana? "UKIENDA KWENYE MSIBA UTAMJUA TU MFIWA"
Kuna watu humu bado wana mawazo ya kibakwata bakwata, Mwanzoni nilidhani Waislamu ni tabaka la wajinga na watu duni, lakini tangu nigunduwe kwamba Agha khan ni ya waislamu na Jamathini ni ya waislamu na mabohora wote ni waislamu ndipo nilipokuja kupata conclusion kumbe tatizo siyo dini ya kiislamu kumbe tatizo ni shura ya maimamu na Bakwata, ukitaka kujadili maendeleo jadiliana na waislamu wanaotoka nje ya jumuiya hizi Bakwata, shura ya maimamu na Baraza la ulamaa.
 
Watu waliokufa kwa kukosa matibabu hawakuwa wa dini moja, walikuwa kutoka dini zote hapa nchini. Watu waache kuangalia majanga ya kitaifa katika sura ya kidini. Bali katika sura ya utaifa.
 
Back
Top Bottom