Maaskofu na fedha ya ESCROW

Maaskofu na fedha ya ESCROW

Incredible

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,031
Reaction score
1,603
Ili padri apewe daraja la uaskofu sharti apewe jimbo. Hivyo askofu ni askofu wa jimbo fulani a.k.a jimbo mahalia.

Askofu Kilaini ni askofu msaidizi wa kanisa katoliki jimbo la Bukoba.

Ukitaka kutoa msaada wako wa fedha au vifaa, unatoa kwa kanisa katoliki jimbo la Bukoba. Kama ni hundi au Telegraphic Transfer a.k.a TT inatumwa kwenye akaunti ya kanisa katoliki jimbo la Bukoba au kama ni jimbo la Dar Es Salaam basi unatuma huko.

Na hata kama unataka kutoa sadaka ya kiwanja, lazima itafanyika transfer kutoka kwenye jina lako na kuwekwa kwenye jina la kanisa. Hauwezi toa sadaka yako kwenda kwa askofu Kilaini au askofu fulani. Huo ndiyo utaratibu wa kanisa katoliki.

Bunge katika mjadala wake, litamke waziwazi kwamba hawa maaskofu wafunguliwe mashtaka ya jinai. Kufanya hivyo siyo kuingilia mhimili wa mahakama kama Mheshimiwa Makinda anavyodai. Tunaona kwamba ni innocent ila tunawapeleka mahakamani ili mahakama either iwa exonerate au iwa convict.

Jambo lingine nikwamba, kanisa langu katoliki Tanzania, halina tena usafi tena wa kuinyoshea kidole serikali sababu watumishi wa serikali wasio waaminifu wanashirikiana na maaskofu wasio waaminifu kuhujumu mali ya umma. Zile pesa za Escrow ni za umma. Kama siyo za umma, kwanini kampuni binafsi inawagawia fedha viongozi wa umma? Ni ujira kwa kazi gani?

Huko nyuma Kilaini aliwahi kupelekwa nje kutibiwa kwa pesa za kiongozi wa serikali. Je kanisa katoliki lilikosa pesa ya kumtibia askofu huyu. Kanisa lijichungeze. Je nikwanini maaskofu hawa waliopokea pesa za ESCROW wote ni wale tu wasaidizi wa Pengo? Japo Kilaini kahamishwa lakini katokea kwa Pengo. Huyu mwingine ni msaidizi wa Pengo. Je Pengo kwanini anapendekeza wasaidizi wenye kasoro kimaadili?

Kanisa katoliki Tanzania tumechafuka
 
... Je Pengo kwanini anapendekeza wasaidizi wenye kasoro kimaadili?
Anapendekeza wasaidizi wasio na maadili au wasaidizi wake wanakosa maadili wakiwa tayari wameshapendekezwa?
 
Kanisa Katoliki lirudishe hela za wakipa kodi. Tuache kumumunya maneno hapa.
Hela waliyopewa maaskofu ni takribani milioni 160. Hiyo ni hela ndogo sana ambayo pengine hata wakiambiwa watairudisha hapo hapo. Tukumbuke Singasinga amechota bilioni 306
 
...
Bunge katika mjadala wake, litamke waziwazi kwamba hawa maaskofu wafunguliwe mashtaka ya jinai. ...
Ili mtu afunguliwe mashtaka ya jinai, lazima kuwepo kosa la jinai. Ni vyema ukaisaidia mahakama kuonyesha kosa la jinai lililofanyika hapo.
Halafu wait a minute, hivi JK hawezi kukabidhiwa hela aifikishe kwenye taasisi fulani, say ya watoto yatima, bila kulazimika kuweka hela kwenye akaunti ya kituo hicho?
 
Watanzania bwana. Mzizi mkuu umewashinda kuung'oa. Sasa mnaanza kuparamia kufyeka majani ya mti. Ng'oeni mzizi mkuu kwanza, hayo majani yatakauka tu automatically. Hebu mshughulikieni aliyegawa hizo pesa kwanza.
 
Askofu no binadam kama wengine kama binadamu tunamapungufu yetu hivyo hawa maaskofu waungame warudishe fedha zetu ...na kimsingi wamepoteza sifa ya Utumishi Vatican iwashughulikie....
 
Jambo lingine nikwamba, kanisa langu katoliki Tanzania, halina tena usafi tena wa kuinyoshea kidole serikali sababu watumishi wa serikali wasio waaminifu wanashirikiana na maaskofu wasio waaminifu kuhujumu manani za umma. Zile pesa za Escrow ni za umma. Kama siyo za umma, kwanini kampuni binafsi inawagawia fedha viongozi wa umma? Ni ujira kwa kazi gani?

Mi nadhani tuanzie hapa. Je walilipwa ujira gani? Hili hamna aliyetayari kujibu maana itatibua siasa na kuweka uhalisia. Ndiyo maana haisemwi alilipwa bali zito anasema waligawana. pia hawasemi account ni ya nani bali waliogawiwa hamna document inayotaja account name bali namba na majina ya wqnayoiservice. wenye ushahidi wa hili ni mabenki husika na wenye waliotajwa kugawiwa fedha.

Kuhusu kanisa nadhani ni swala la kujiuliza tu ni kanisa linaendeshwaje? Basi na si zaidi.

Swala la Kilaini kwenda kutibiwa sishangai kwani yeye ndiye kiongozi wa dini pekee kutubiwa kwa fedha za srrikali? Au kwasababu alisema JK ni chaguo la Mungu kwa mujibu wa maelezo ya humu? Swala la eskrow linaendeshwa kisiasa na litaisha kisiasa.
 
Kosa la jinai la maaskofu hawa ni kukwepa kodi. Mapato yoyote apatayo mtu lazima yalipiwe income tax to the tine of 30%
 
Kanisa langu Katoliki limechafuka na kuonesha mifumo yake imefeli kutuondolea huu upuuzi.......tunasubiri hatua kali na si ujanja ujanja.......
 
Kanisa Katoliki lirudishe hela za wakipa kodi. Tuache kumumunya maneno hapa.

Kuwa makini na kauli zako..Kilaini sio kanisa katoliki aisee...na ndo mana unaona kanisa lipo kimya..
 
Kanisa langu Katoliki limechafuka na kuonesha mifumo yake imefeli kutuondolea huu upuuzi.......tunasubiri hatua kali na si ujanja ujanja.......

Kanisa halikurupuki katika maamuzi yake wewe...unafahamu ni kwa nini kilaini alihamishwa jimbo kuu la dar? Kilaini ni tatizo
 
Kanisa langu Katoliki limechafuka na kuonesha mifumo yake imefeli kutuondolea huu upuuzi.......tunasubiri hatua kali na si ujanja ujanja.......

Nimekua makini kufuatilia ila mpaka mwisho nimegundua kitu kimoja tu ambacho huenda kinaleta mkanganyiko kidogo. Hivi bungeni kuna sehemu umeona wanasema pesa za Rugemalira ni haramu?
Zaidi wengine wameishia kumpongeza kwa jinsi alivyolipa kodi na mengineyo. Kwa njia hiyo pesa yake haina tatizo lolote zaidi ya sisi wananchi kupiga kelele tu. Na mpaka hapo kama ni skendo limwangukia singasinga ambaye najua serikali haiwezi kumfanya lolote.

Sasa kinachonipa utata kama pesa za Rugemalira ni halali na hazina tatizo lolote inakuwaje waliopewa pesa na tajiri huyo waingie hatiani? Nisaidieni ufafanuzi kidogo.

Hapa naona mwenye kosa zaidi ni Bank ya Mkombozi kufanya miamala mikubwa kinyume na sheria. Kwani sheria iko wazi hauruhusiwi kutoa cash ya kuanzia milion 10 na kuendelea.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Wamekua mabingwa wa kutoa matamko kumbe wanavuta Nyuma ya pazia, ingekuwa bakwata ndio wamevuta mshiko hui, ijumaa ijayo waislam wangeandamana kwenda kuwatoa na bakora.
 
Ili mtu afunguliwe mashtaka ya jinai, lazima kuwepo kosa la jinai. Ni vyema ukaisaidia mahakama kuonyesha kosa la jinai lililofanyika hapo.
Halafu wait a minute, hivi JK hawezi kukabidhiwa hela aifikishe kwenye taasisi fulani, say ya watoto yatima, bila kulazimika kuweka hela kwenye akaunti ya kituo hicho?

pesa nyingi hivo za kubebwa kwenye magunia...kuna maana gani kubeba mzigo wote huo wakati mabank yapo na kutransact haichukui hata nusu SAA
unazipush tu then unatembea mwepesiii...Fumbua macho kaka.
 
Tangu lini maaskofu wamekua watakatifu nchi hii? Nimafisadi wakubwa na ndomana hawataki mkaguzi mkuu wa serikali achunguze matumizi ya fedha za ruzuku wanazopewa na serikali. Wanafanya ufisadi kweny misamaha ya kodi kweny taasisi za kidini
 
Hela waliyopewa maaskofu ni takribani milioni 160. Hiyo ni hela ndogo sana ambayo pengine hata wakiambiwa watairudisha hapo hapo. Tukumbuke Singasinga amechota bilioni 306

Wizi wizi tu haujalishi ni kiasi gani kimechotwa bado watabaki kuwa wezi tu maana hakuna asiyejua kwamba serikali ya Tanzania kwenye mkataba uliosainiwa na Lowassa mwaka 1992 Februari 21, utagundua ufisadi ulishatengenezewa njia na wapita njia hii ni mawaziri na viongozi hao
 
Back
Top Bottom