Kakke
JF-Expert Member
- Dec 4, 2010
- 1,883
- 1,483
Mwandishi Wetu
Toleo la 275
2 Jan 2013
Mbali na kukutana na viongozi hao kwa ajili ya kusikiliza maoni yao kuhusu maudhui ya Katiba mpya, Tume ya Katiba chini ya Mwenyekiti wake, Jaji Warioba pia itakutana na viongozi wa vyama vya siasa. Vikao hivyo vikitarajiwa kuanza Jumatatu, Januari 7, wiki ijayo.
Vikao hivyo vinaanza katika wakati ambao maaskofu wametoa tamko zito la kuitaka Serikali kukanusha kulea udini nchini, sambamba na kutaka hadhi ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere iheshimiwe na kuhifadhiwa, tamko ambalo lilisomwa wakati wa Ibada ya Sikukuu ya Krismasi, mwaka jana, katika makanisa karibu yote nchini.
Sehemu ya tamko hilo inasema; Vyombo vya habari vya kidini vinatumiwa na viongozi (baadhi) wa dini ya kiislamu kuukashifu Ukristo na kuwachochea Waislamu hadharani kupitia vyombo hivyo wakiwataka wawaue Maaskofu, Wachungaji, iwe kwa siri au hadharani.
Japo Serikali imesikia kashfa na uchochezi huo hatarishi, imeendelea kukaa kimya, na kuwaacha wachochezi hao wakiendelea kuhatarisha amani bila kuwadhibiti.
Jambo hili linatia mashaka makubwa juu ya umakini wa Dola kuhusu usalama wa wananchi nchini mwao. Imani kali za namna hii huchochea vitendo viovu vya uasi na hujuma sio tu dhidi ya waamini na viongozi wa dini fulani, bali hata na kwa serikali na viongozi waliopo madarakani, endapo waamini wa dini fulani katika taifa kama Tanzania lililo na waamini wa dini nyingi tofauti, hawataheshimu na kutendeana kiungwana baina yao na wale wasio wa dini na mapokeo yao. Hali hii inapelekea (sababisha) kujiuliza kama je, huu ni wakati mwafaka kwa kila raia au kiongozi wa dini kujilinda yeye mwenyewe na waamini wake dhidi ya wenye imani kali? inaeleza sehemu ya tamko hilo la Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF).
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana wiki hii, vikao vya viongozi wa dini na Tume ya Mabadiliko ya Katiba vinatarajiwa kwa namna fulani kupoza hali ya hewa iliyochafuka kiasi cha kuwatia wasiwasi viongozi wa kidini nchini, ambao baadhi yao, kutoka pande zote za Kikristo na Kiislamu, wamekwishajeruhiwa na watu wasiofahamika kiasi cha kunusurika kupoteza uhai wao.
Katibu wa Mufti Zanzibar, Sheikh Fadhili Soraga aliwahi kumwagiwa tindikali na watu wanaodaiwa kutokujulikana. Tukio hilo lilitokea eneo la Magogoni Msumbiji, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar Novemba, mwaka jana.
Lakini kwa upande mwingine, Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mpendae Zanzibar, Ambros Mkenda, alipigwa risasi maeneo ya Tomondo, nje kidogo ya mji wa Unguja, Desemba, mwaka jana.
Ni matokeo hayo pamoja na mengine yanayowaweka katika hali ya wasiwasi viongozi hao wa kidini nchini, hususan kuhusu usalama wao, waamini wao na mali zao, jambo ambalo linatarajiwa kujitokeza kwa mapana yake katika vikao kati ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na viongozi hao.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, kimsingi, viongozi wakuu wa dini karibu zote wanakubaliana kwamba Tanzania iendelee kutokuwa nchi ya kidini lakini hata hivyo, shughuli za kidini na kiimani miongoni mwa raia wake ziendeshwe kwa kuheshimiana, kuvumiliana na kwa upendo mkubwa.
Kauli ya Jaji Warioba
Katika mazungumzo yake na mwandishi wetu Jumatatu wiki hii, Jaji Warioba alisema tayari Tume yake imekwishakupata msingi wa kuandika Katiba mpya, hata hivyo akasisitiza kuwa, fursa zaidi ya kukusanya maoni ingalipo.
Katika hatua nyingine, Warioba, amepinga uamuzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) uliotangazwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kuhusu wito wa mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1985.
Warioba ambaye kwa sehemu kubwa ndiye aliyekuwa kiunganishi cha kuwapo kwa mazungumzo kati ya ujumbe wa CHADEMA na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu-Dar es Salaam, kuhusu Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo awali ilisusiwa na wabunge wa chama hicho, anasema ...huwezi kubadilisha sheria ya uchaguzi bila kujua mfumo wa uchaguzi utakaotumika.
Msingi wa maelezo hayo ya Jaji Warioba unatokana na maelezo ya Mbowe alipokuwa akisoma uamuzi wa chama chake kwa waandishi wa habari Desemba mwaka jana, akisema Kamati Kuu imependekeza wakati mchakato wa kupata Katiba Mpya ukiendelea, ufanyike utaratibu wa kubadili sheria mbalimbali, ikiwamo ya uchaguzi ya mwaka 1985.
Kwa mujibu wa Mbowe, kubadilishwa kwa sheria hiyo kutaliwezesha Taifa kupata Tume ya Uchaguzi iliyo huru na isiyofungamana na upande wowote na kwamba daftari la kudumu la wapiga kura litaweza kuboreshwa.
Katika kuongeza nguvu hoja hiyo, Mbowe alisema vyama vya upinzani vimekuwa katika wakati mgumu kujiandaa na Uchaguzi Mkuu wa 2015 wakati mfumo wa uchaguzi ujao ni kitendawili kisichofahamika jibu lake.
Lakini katika mazungumzo yake na mwandishi wetu Jumatatu wiki hii, Jaji Warioba anasema mabadiliko ya sheria kwa kawaida misingi yake inatokana na aina ya mfumo ulioridhiwa katika uendeshaji wa jambo husika.
Huwezi kubadilisha sheria ya uchaguzi hadi kwanza ujue mfumo utakaotumia kuendesha uchaguzi. Kwa sasa tupo kwenye mchakato wa Katiba mpya na kwa bahati nzuri mchakato huu umeanzishwa na viongozi lakini umeungwa mkono na wananchi.
Baada ya mchakato kukamilika na Katiba kuwa tayari (Aprili, 2014) tutakuwa na karibu mwaka mmoja na nusu wa kutunga au kubadili baadhi ya sheria, ikiwamo ya uchaguzi kama itahitajika kufanya hivyo. Kwa hiyo, huu si wakati wa kufanya mabadiliko ya sheria ya uchaguzi wakati hata mfumo wa uchaguzi unaozingatia maoni ya wananchi kwa mujibu wa Katiba mpya itakayopatikana bado haujawa tayari.
Mimi nawaomba viongozi waheshimu maoni ya wananchi. Katiba ndiyo sheria mama inayosimamia maisha ya wananchi, sheria hiyo kuu ndiyo inayozaa sheria nyingine. Viongozi wasitazame maslahi yao wenyewe, watazame na kuheshimu maslahi ya wananchi, anasema Jaji Warioba.
Msingi wa Katiba umepatikana
Katika hatua nyingine, Jaji Warioba anasema msingi wa kuandika rasimu ya Katiba Mpya umekwishapatikana kutokana na maoni ya wananchi yaliyokwishakusanywa hadi sasa.
Tumekwishapata msingi wa kuandika Katiba mpya kutokana na maoni ya wananchi yaliyokusanywa, kazi ya kukusanya maoni lakini bado inaendelea na kuanzia Januari 7, tutaanza kuchukua maoni ya taasisi za kidini, asasi za kiraia, vyama vya siasa na wengine katika makundi yao maalumu. Baada ya hapo tutafanya tathmini na kisha kuandika rasimu ya Katiba itakayokwenda kwenye Mabaraza ya Katiba.
Katika Mabaraza ya Katiba uchambuzi utafanyika, wananchi watapima maoni waliyotoa na kile kilichomo kwenye rasimu. Kama kuna maoni muhimu yatakuwa yameachwa, nafasi bado itakuwapo kurekebisha.
Tunatarajia rasimu ya mwisho ya Katiba mpya itatolewa Septemba, mwaka huu na Oktoba na Novemba, Bunge la Katiba kukaa na kujadili rasimu hiyo.
Bunge hili linatarajiwa kumaliza kazi zake Januari, 2014 na baada ya hapo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuweka utaratibu wa kupiga kura za ndiyo au hapana rasimu ya Katiba mpya. Hii ni kazi nzito, Tume ya Mabadiliko ya Katiba itafanya bidii kukamilisha kazi ndani ya muda, anasema Warioba.
Mtazamo wa kisomi
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally, akizungumzia mtazamo wake kuhusu Katiba mpya ndani ya mwaka huu mpya wa 2013 anasema: Wananchi wengi wanatarajia kwamba misingi ya uhuru, uwazi, ushiriki, uvumilivu wa kisiasa na uzalendo itaendelea kuongoza mchakato wa kutunga Katiba mpya kama ilivyokuwa kwa mwaka 2012.
Pamoja na kasoro kadhaa zilizojitokeza mwaka 2012, Tume imefanya kazi nzuri. Bila shaka katika mwaka 2013 wajumbe wa Tume wataendelea kuheshimu viapo vyao na hadhi zao katika jamii.
Hata hivyo, kwa kuzingatia uzoefu wa mchakato wa ukusanyaji maoni mikoani, kazi ya ziada inatakiwa kufanywa na kila Mtanzania ili kuhakikisha kuwa madhumuni ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba yanafikiwa.
Baadhi ya vikundi maslahi vilijaribu kuingilia uhuru wa wananchi wa kujieleza na kutoa maoni. Tishio hilo bado lipo. Vile vile Tume inatakiwa kuwa makini zaidi ili umma wa Watanzania uendelee kuiamini na kuipa ushirikiano.
Tume inatakiwa kuendelea kuwajibika kwa Watanzania kwa kutoa taarifa muhimu kwa umma kwa usahihi na kwa wakati. Umma nao unatakiwa kudai uwajibikaji wa Tume ili rasilimali nyingi za umma zinazotumika wakati wote wa mchakato wa kutunga Katiba zisipotee bure.
Ni muhimu pia Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya 2012 ikaangaliwa upya kwa lengo la kuboresha mchakato wa kutunga Katiba mpya. Tayari Rais ametoa ahadi katika salamu zake za mwaka mpya kwamba majadiliano kuhusu marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba yatafanyika na sheria hiyo itafanyiwa marekebisho na Bunge kati ya Januari na Aprili 2013.
Kwa maoni yangu, sehemu ya tano ya sheria hiyo inayohusu Bunge la Katiba inatakiwa kurekebishwa ili Bunge Maalumu lisiwe chini ya udhibiti wa wajumbe kutoka kwenye vyama vya siasa.
Ikiwa wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar watakuwa wajumbe wa Bunge Maalumu kama sheria ya sasa inavyotaka, itakuwa vigumu sana sauti za wajumbe kutoka makundi mengine ya kijamii kusikika na maoni yao kuzingatiwa.
Hatimaye, mchakato mzima unaweza kuchukua mkondo wa itikadi finyu za kisiasa badala ya kujenga mwafaka wa kitaifa. Muundo wa Bunge Maalumu na mamlaka yake ni masuala nyeti kwa mustakabali wa mchakato wa kutunga Katiba Mpya. Eneo hili linatakiwa kutazamwa upya katika mwaka 2013.
Mchakato wa kutunga Katiba unatarajiwa kukamilika mwaka 2014, na Katiba hiyo mpya kuzinduliwa rasmi Aprili, 2014, wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Toleo la 275
2 Jan 2013
- Jaji Warioba asema msingi wa Katiba umepatikana
- Wasomi: Wabunge wangoke Bunge la Katiba