MAARIFA YA MUNGU YANAVYOWAZIDI KETE KIZA NA KIFO.

MAARIFA YA MUNGU YANAVYOWAZIDI KETE KIZA NA KIFO.

simba songea

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2016
Posts
1,496
Reaction score
1,219
Mungu ndo muweza yote yeye ndo kila kitu katika uso wa dunia na ulimwengu. Hakuna amtumainiye akapotea. KUT 3;14, Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO;akasema,Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli;MIMI NIKO amenituma kwenu.

Hakuna alipangalo Bwana Mungu akashindwa. Yeye ndo ufanya vitu vyote visivyo wezekana viwezekane.

Unapotaja KIZA nA KIFO bila ubishi utakubaliana nami kwamba kwamba MUNGU ndo muweza wa yote kwa hao wote. MUNGU alimshinda KIZA kwa kumfungia. Pia MUNGU huyu huyu aliushinda umauti pamoja na kifo kupitia BWANA YESU KRISTO.

Wakuu wa giza wachawi waganga vibwengo umtumia KIZA kupata nguvu za giza, ujaribu kumtumia mtu aliye kifungoni ili awape nguvu tena mbaya zaidi wapigane na watu wa MUNGU ambaye yuko hai. Wachungaji, mapadiri, masheikh hutumia nguvu za MUNGU ili kupambana na nguvu za giza na ushinda, hii uonesha namna gani MUNGU wetu alivyo na nguvu.

MUNGU anaushinda umauti kwa kumtoa mwanae sadaka, Bwana Yesu anakufa lakini anafufuka anamshinda KIFO. Kwa akili za kawaida tutaona simpo lakini tunaambiwa kuzimu kulikuwa na vita kati ya MUNGU na KIFO. KIFO anataka kumuua MUNGU lakini kutokana na nguvu alizonazo MUNGU anamshinda KIFO. (YOHANA 16;33) “Jipeni moyo! Mimi nimeushinda ulimwengu.” Alimaanisha nini kwa maneno hayo ya ujasiri? Alimaanisha hivi kwa sehemu: ‘Maovu ya ulimwengu hayakunitia uchungu wala kufanya nitake kulipiza kisasi. Sikuruhusu ulimwengu unibadili nifuate njia zake. Nyinyi pia mnaweza kufanya hivyo.’ Mambo ambayo Yesu aliwafundisha mitume wake waaminifu saa chache kabla ya kufa yangewasaidia pia waushinde ulimwengu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom