Maandishi haya yanaitaji akili y'all ziada

Rofa

Member
Joined
Sep 19, 2015
Posts
79
Reaction score
126
Anaandika Askofu Benson Bagonza

Jizoeze kuvuta pumzi na kufikiri. Hii itakusaidia kujisikiliza kabla hujategemea kusikilizwa na unaowahutubia. Uwezo wa kujisikiliza hukuwezesha kutambua kweli hizi:

1. Haki na madaraka ya kumpiga mtu haimwondelei mtu huyo haki ya kulia. Kwa hiyo kumchapa mtu kisha ukamwambia "funga mdomo" ni kujipa haki isiyo yako. Iliyo yako ni kuchapa. Mchapwaji ana haki ya kulia na kutolia. Haki hii haiondolewi na mamlaka yoyote ya duniani wala kuzimu. Jadili hata kama huwezi kubadili chochote.

2. Mtawaliwa ana haki ya kulalamika. Katiba itamke au isitamke, maadam kuna mtawala na mtawaliwa; basi kulalamika ni haki isiondolewa ya mtawaliwa.

3. Hali kadhalika, mtawala ana haki ya kulalamikiwa isiyotegemea kuwemo au kutokuwemo ndani ya katiba. Mtawala asipolalamikiwa anakuwa ameonewa na kunyimwa haki yake. Kuzuia kulalamikiwa si kujionea tu, bali ni kukwepa kupokea haki ikupasayo.

4. Mtawala kupongezwa, kuombewa na kusemwa vizuri si haki ya kikatiba. Hizi ni fadhila zisizolipiwa.

5. Kulalamikiwa si kigezo kuwa mtawala ni mbaya. Ni raia wanatekeleza haki yao ya msingi isiyohitaji katiba.

6. Kusifiwa si kigezo kuwa unafanya vizuri. Ni upatikanaji wa fadhila zisizolipiwa bila kudaiwa.

Hoja hufungwa kwa hoja, si kwa kifungo wala mahabusu. Hoja yenye nguvu haihitaji dhamana mahakamani. Tuwahi foleni.

Askofu Benson Bagonza.
 
Nashukuru sana Baba Askofu kwa bandiko lako lenye Rundo ye hekima.
 
Hakika umenena baba Askofu
 
Back
Top Bottom